Wapi naweza kujifunza lugha ya Kichina?

Wapi naweza kujifunza lugha ya Kichina?

Sammo Hung

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2017
Posts
1,165
Reaction score
1,355
Wadau kama kichwa cha uzi huu kinavyojieleza, nimevutiwa sana kujifunza lugha ya Kichina cha kuongea na kuandika kwasababu zifuatazo;

1) Nchi yetu imekuwa ikipokea wageni wengi sana kutoka China ambao ni wataalamu katika nyanja mbalimbali hususan suala zima la ujenzi wa miundombinu, hivyo kuna fursa ya ukalimani ili kuweza kuwaunganisha wataalamu hawa na vibarua wao(Watanzania).

2) Miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi ni China hivyo kadri siku zinavyozidi kwenda hakutakuwa na namna ya kukwepa kufanya biashara na Wachina, bila kufahamu lugha yao basi biashara itakuwa ngumu sana.

3) Wingi wa bidhaa kutoka China zenye maelezo ya namna ya kutumia na tarehe za kuharibika pamoja na malighafi zilizotumika kutengeneza bidhaa hizo kwa lugha ya Kichina, bila kujua lugha ya kichina unaweza kubambikwa bidhaa iliyokwisha muda wa matumizi au iliyotengenezwa kutumika kwa muda mfupi alafu ikala kwako.

Kutokana na maelezo hayo basi, ningeomba wadau mnifahamishe ni wapi naweza kujifunza lugha hii, gharama za kujifunza na itanichukua muda gani hadi kuweza kuzungumza na kuandika Kichina kwa ufasaha.

Nawasilisha
 
Nenda UDSM pale usiogope kuuliza Mkuu pale ndio utapikwa na kukijua vizuri na hata utaambulia CHeti chako kinachotambulika na sio huko kwingine Makwasukwasu
 
Njoo Ardhi kichina kinafundishwa bure
 
Anza mazoezi ya kula kwa vijiti pia itasaidia sana kuelewa mapema (utani)
 
Nenda UDSM pale usiogope kuuliza Mkuu pale ndio utapikwa na kukijua vizuri na hata utaambulia CHeti chako kinachotambulika na sio huko kwingine Makwasukwasu
Sawa mkuu asante sana kwa ushauri.
 
Kuna siku nilienda udsm nikakuta watu wanafundishwa kichina
 
Nadhani UD kichina ni free Kwa Mwanafunzi wa pale, Ila kama sio itakutoka Kati ya laki 3 mpka laki 4
 
Hongera mkuu kwa kutaka kwenda mbali zaidi wakati wengine tunaendelea kujikongoja na is the... Is the....is the .....
 
Back
Top Bottom