Wapi naweza kufanya kipimo cha DNA hapa Dar es salaam?

mtalisi

Member
Sep 17, 2010
56
79
Eti wakuu ni wapi naweza kufanya kipimo cha DNA kwa hapa Dar es salaam, kuna ishu inanisumbua nahitaji suluhisho....

Kama unafahamu sehemu husika naomba taarifa au mawasiliano.

Ni muhimu saaaaaana....
 
Eti wakuu ni wapi naweza kufanya kipimo cha DNA kwa hapa Dar es salaam, kuna ishu inanisumbua nahitaji suluhisho....

Kama unafahamu sehemu husika naomba taarifa au mawasiliano.

Ni muhimu saaaaaana....
Mkuu kama umeamua kuleta tatizo humu we funguka tu
Tuna ma dokta na wataalamu wa akili humu ili wakusaidie
 
Hao madokta wanajua vipimo vya DNA bila kupima mkuu? , madokta wako wanatia shaka mkuu.......ama wewe ndiye unatia shaka....
Hahaha mkuu.
Ni hivi ,huyo bwana hapo ilibidi atililike kidogo ili watu wajue wanamsaidia vipi kwa sababu ni wazi ana wasiwasi mtoto si wake

Je akienda huko akapima DNA akakuta si wake alafu akamchinja mtoto ? So ni vema angetoa hint ya tatizo
 
Nimemwambia afunguke vizuri humu asaidiwe
Anaeza ua mtu huko
Acha kukimbiakimbia kujibu swali lililoulizwa kwa kutoa maelezo meeeengi yenye dhana ambazo hazijajadiliwa,

Namna unavyohandle stress ni tofauti kabisa na jirani yako hapo nyumba ya pili tu, hivyo dhana za kwenye maisha yako hazifanyi kazi kwa kila mmoja...
 
ujiandae kisaikolojia pia kwa matokeo yeyote ukishafanikisha
Watu wenye uchumi unaoleweka wanapima kila siku ziendazo kwa mungu na hatusikii hayo matukio ya kuuana, hizi ni dhana zilizo jaa kwenye mioyo yetu ya uswahilini ya kudhani kuwa ukweli wowote mkali huwa unaleta mauaji au fujo,

Tuondokane na hizi dhana za uswahilini, sisi watu masikini tunapenda sana maisha ya kibabaishaji na kukwepa ukweli eti tu kwa vile ukiujua utakuumiza, nasema no, ni lazima tujifunze kuukubalu ukweli na kuuchukulia positive kama ulivyo,

Why uue wakati mtoto sio wako, kwani watoto wote waliopo ni wako?

Hebu nipeni majibu ya swali langu kama munayo tafadhali....
 
Kwa tz mkuu ni process ndefu sana..ila nairobi ni kamq unaenda kupima choo tu fasta majibu unapata
 
Kwa tz mkuu ni process ndefu sana..ila nairobi ni kamq unaenda kupima choo tu fasta majibu unapata
We mbona unatoka nje ya mada, mkuu anaomba apate process ya kupima dna Tanzania hii, wewe unasema nairobi km huna mchango weka emoji tupige like
 
Watu wenye uchumi unaoleweka wanapima kila siku ziendazo kwa mungu na hatusikii hayo matukio ya kuuana, hizi ni dhana zilizo jaa kwenye mioyo yetu ya uswahilini ya kudhani kuwa ukweli wowote mkali huwa unaleta mauaji au fujo,

Tuondokane na hizi dhana za uswahilini, sisi watu masikini tunapenda sana maisha ya kibabaishaji na kukwepa ukweli eti tu kwa vile ukiujua utakuumiza, nasema no, ni lazima tujifunze kuukubalu ukweli na kuuchukulia positive kama ulivyo,

Why uue wakati mtoto sio wako, kwani watoto wote waliopo ni wako?

Hebu nipeni majibu ya swali langu kama munayo tafadhali....
mbona Mimi sijaongelea kuuana mahali aisee
 
Mtoa swali una hasira kama mnywa visusio kha! Ndo stress au? Kama huijui jf ndivyo ilivyo, hadi upate jibu labda page ya 5.
Mimi sijui wanakopima wala process za dna . Thanks
 
Mtoa swali una hasira kama mnywa visusio kha! Ndo stress au? Kama huijui jf ndivyo ilivyo, hadi upate jibu labda page ya 5.
Mimi sijui wanakopima wala process za dna . Thanks
Asante mkuu tupo pamoja, at least kama hujui basi ongea utumbo ila mwishoni useme kuwa hujui jibu.......

Ila sio kuongea utumbo tu halafu unataka kuficha kutokujua kupitia utumbo wako!!!

Similar Discussions

Back
Top Bottom