Wapi CUF, TLP na UDP? Au vimepewa BAN?

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,287
Kila siku ni habari za vua gamba vaa gwanda,yaani ccm na cdm tuu! Vile vyama vingine tulivyokuwa tunafundishwa kwenye civics vimepotelea wapi? Au havina wagombea nini. G9t
 
SI MWENYEKITI KESHALAMBA CHAKE kule magambani..unafikiri atasema kitu bana...
kwisha habari yao hawa
 
cuf mke wapili wa ccm,nccr mageuzi mke wa tatu wa ccm.wengine aidha kwa kuogopa ndoa ya mkeka wamelala mbele kimebaki kidume chadema hakitaki mke wala mshenga kinataka haki kwa kila mtanzania.

IUNGE MKONO CHADEMA KWA UKOMBOZI WA TANZANIA.
 
aisee kumbe
 
Mbona mi sijafikisha miaka 18 bado jamani.Nitajiunga cdm muda ukifika

18 ni umri wa kupiga kura, lakini unaweza kujiunga hata ukiwa na umri chini ya hapo....mbona mtoto wangu amepiga gwanda angali mama yake hajafika labour? Yuko tumboni lakini anagwanda.....huo ndio UZALENDO.....KUWA NA UCHUNGU NA NCHI YAKO HATA KABLA YA KUZALIWA......WATASEMA KWELI MWAKA HUUU!!!!!
 
CCM imefanikiwa kuviletea mgogoro kama YANGA. UDP huwa sio chama ni entreprise ya Cheyo!
 
18 ni umri wa kupiga kura, lakini unaweza kujiunga hata ukiwa na umri chini ya hapo....mbona mtoto wangu amepiga gwanda angali mama yake hajafika labour? Yuko tumboni lakini anagwanda.....huo ndio UZALENDO.....KUWA NA UCHUNGU NA NCHI YAKO HATA KABLA YA KUZALIWA......WATASEMA KWELI MWAKA HUUU!!!!!

nimekubali mkuu! Tanzania bila gambaa.........!
 
yaani umenikumbusha nilishavisahau, mrema anaangalia wagonjwa kcmc na kupeleka majeruhi,., mbatia yk nccrccm, cheyo kama una kumbukumbu angalia arumeru vilikuwa vyama vingapi. nilifanikiwa kumuona mgombea mmoja sikumbuki chama gani akisukuma gari utawaona tena 2015
 
Hamtaisha kutukana, sijui ni nini, kiburi cha mafanikio?
Someni basi angalau Tanzania daima la leo
NCCR-Mageuzi wazidi kuishambulia CCM

na Mwandishi wetu, Mtwara

amka2.gif
VIONGOZI wa kitaifa wa Chama cha NCCR –Mageuzi, walioko mjini hapa, wameendelea kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwataka wananchi wasikichague katika uchaguzi wowote.
Wamesema kama wananchi wanataka maendeleo ya kweli, na njia pekee ya kuwafikisha mahali hapo ni kukihama chama hicho tawala kwa kuwa ndicho kimesababisha maisha magumu yanayowakabili.
Mashambulizi hayo yalitolewa jana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Danda Juju na Salum Msabaha walipokuwa wakihutubia mikutano ya hadhara katika Majimbo ya Mtwara Mjini na Nanyumbu.
Akihutubia katika Jimbo la Nanyumbu, Juju alisema umefika wakati sasa wananchi wa Mtwara kuonyesha kwa vitendo jinsi wanavyochukia maisha magumu yanayosababishwa na CCM kwa vile bila kufanya hivyo maisha bora kwa kila Mtanzania hayatapatikana.
"Ndugu zangu, wakoloni tuliwakataa na kuwataka watuachie nchi yetu kwa sababu walishindwa kutufikisha mahali tulipokuwa tukitakiwa kufika ikiwamo kutotoa demokrasia ya kweli.
"Wakoloni tuliwakataa kwa sababu hatukuona sababu ya kuendelea nao, lakini kwa bahati mbaya baada ya watu hao kutuachia nchi yetu, wamekuja wakoloni wengine ambao ni CCM, hawa nao sasa wanatakiwa kutupisha.
"CCM hawana tena chao, waambieni tumechoka, waambieni hatuwataki tena kwa sababu hao CCM ndio wanaosababisha zao la korosho linakosa bei na hao hao ndio wanaosababisha maisha magumu kwa kila Mtanzania.
"Maisha kila siku yanakuwa magumu, yaani nawahakikishia kama mtaendelea kuichagua CCM ipo siku mtaanza kula mlo mmoja kwa siku ingawa sasa wengi wetu tunaishi maisha ya kubahatisha," alisema Juju.
Naye Msabaha alisema kama viongozi wa serikali wataendelea kutumia vibaya rasilimali za taifa, chama hicho kitaitisha maandamano ya aina yake kwa wananchi kuzingira nyumba za viongozi hao, ili kuwashinikiza wajiuzulu.
"Korosho mnakopwa kila siku halafu mnapolipwa mnakatwa makato yasiyokuwa na maana, nawaambia kama viongzi wataendelea kuwanyanyasa wananchi, sisi NCCR tutakuja na maandamano mapya na ya aina yake.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom