Wapenzi wanaweza kukopeshana hela?

Wanaweza ndio hasa wale wa kishumundu na machame
 
Mi nashangaa kila mtu anasema kusaidiana. Hivi mimi tu ndiye ninayeishi dunia nyingine au?

Mimi mpenzi wangu namkopesha sana tu na yeye analipa, anakuja na shida ya kufungua business anahitaji kiasi flani ninamkopa, baadaye anairudisha hela yote. Imetokea mara nyingi na hatuna tatizo kabisa, sasa hivi ana biashara anajitegemea hana hata shida ya kuniomba hela tena, na mkopo wote asharudisha. Utapata wapi mkopo mzuri namna hii usiokuja na riba yoyote wala timelimit.

Kusema umsaidie mtu ni kumfanya awe mvivu tu, mtu akikuomba pesa ukasema umpe yote kama msaada inamuongezea moyo wa kuitumia vibaya maana hamna consequences zozote zitakazompata hata ikiisha, sanasana atakuja kuomba nyingine alafu ujifanye bwege umpe kweli.

Honestly sipendi mwanamke anayeombaomba hela ale bata, huyo simalizi naye wiki. Anayekuja kuniomba hela tufanye biashara ili aweze kujitegemea huyo nampenda sana, mfano kuanzisha food business kama fastfood, kulima, kuimport products na kuuza, namtafutia hadi market kabisa, mwisho wa siku anajitengenezea pesa, na mimi ananitengenezea vilevile maana equity lazima iwepo, nakua ka investor.
 
[emoji109] [emoji109] [emoji109]
 

Kwa kweli mie akiniambia ananikopa nadai uso ukiwa mkavu kabisa no aibu. Na mie nikimkopa namrudishia hela yake. Kama unataka msaada be straight sema ni smaada hurudishi and i do the same. Hapa tunaongelea mume [emoji4][emoji4]
Tusitaniane kwenye pesa kabisa..
 
Kukopeshana kupo, ila wanawake huwa hawalipi nishapitia hali kama hii. Na kilichofuatia alileta visa nikamwacha, saivi kaanza kunitafuta tokea jumatano sijamwuuliza chochote kuhusu deni langu naweka naye ukaribu haswaa ila akiingia tu kingi akaja maskani deni litalipwa tu
 
ha ha ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…