Wapenzi wa mpira wa Miguu; Hii hapa Fursa katika Soccer ambayo ulikuwa huidhanii!

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
Kufanya biashara ya kuonesha mpira wa miguu; Fursa pekee iliyoko nyuma ya pazia!

Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana hapa duniani. Ni mchezo pekee ambao unawashabiki wengi tena wa Lika zote has hasa vijana wakiongoza.

Hapa nchini Tanzania; Wanaume ndio wanaongoza kwa kushabikia mpira kuliko wanawake. Hapo zamani; simba na Yanga zikicheza; ulikuwa unakuta watu wengi kwa makundi wakisikiliza mpira huo kwenye radio. Walikuwa wakipata burudani kwa njia ya masimlizi na si kutazama.

Kwa miaka ya sasa baada ya technologia kukuwa na utandawazi wake; mambo yamebadilika. Kwa sasa radio si ishu tena kusikilizia mpira imebaki ziliendwa! Kwa maeneo mengi sana ya mijini na vijijini mpira huangaliwa kwenye Luninga ( TV).

Kwa sasa; watanzania hufatilia kwa ukaribu lingi maarufu sana na pendwa zenye virabu vikongwe na vikubwa duniani. Ligi hizo ni kama :

1. Ligi za wingereza:
  • Premier Ligi
  • Championship ligi
  • ligi one
  • ligi two
  • Community ligi . etc
2. Ligi za hispania:
  • Laliga
  • 1st segunda
  • 2nd segunda
  • 3rd secunda . etc
3. Ligi ya Ugermani
  • Bundasliga. etc
4. Ligi ya ufaransa
  • Ligue 1
  • ligue 2
  • National conferance. etc
5. Ligi ya Italiano
  • Serie A
  • Serie B. etc
6. UEFA Champion Ligue
Haya ni mashindano ambayo hukutanisha virabu vikuu ( top 4) za kila ligue la nchi fulani barani Ulaya. Kumbe UEFA huchezwa na virabu vilivyopo barani Ulaya kwa sharti kuwa kira kirabu kitakachoshiriki ligi hii lazima kiwe kwenye top 4 kwenye ligi ya nyumbani. ( kwenye nchi za wingereza)

Kwa sharti hili; EUFA huwa mashindano matamu na ya hasa kuangalia kwani hukutanisha virabu vyenye uwezo mkubwa wa kusakata kandanda ( Big clubs) hivyo kuleta big matches.

Mashindano hayo toka yanaanza yanakuwa na hamasa kubwa sana mpaka yanatia nanga mwezi wa tano.

Wapenzi wengi wa mpira kwao bora wakose chakula kuliko kukosa kuangalia kwenye TV mechi hizi hata kama zinacheza mida mobovu ya usiku mida ya saa tano ila utakuta watu wakifurika maeneo ya kuoneshea mpira.

7. Ligi kuu bara. ( Simba Vs Yanga)
8. Cecafa tournerment
9. Europa championship
10. Copa America Centanerio
11. World Cup ( Kombe la Dunia)

N.k

Ndugu Msomaji; kama urikiwa ujui ni kwamba kupitia mpira wa miguu watu wengi hutengeneza sana pesa kila Week end ( juma mosi na juma pili) kwani virabu vyote nilivovitaja hapo juu hushuka viwanjani kila week end. Na watazamaji hulipa kwa kawaida sh. 500 kwa mechi ndogo yaani mechi isiyo na ushindani au mvuto kwa mfano: Barcelona VS Eiber; Chelsea VS QPR au PSG vs Rennes.

Kiingilio cha sh. 1000 hutozwa kwa big matches yaani timu mbili kubwa zinapokutana. Kwa mfano: Barcelona VS Real Madrid; Arsenal VS Man U; Man City VS Liverpool au Germany VS Brazil.

Watazamaji hufulika sana kwenye vibanda vya kuoneshea mpira. Iwe mchana au usiku wa manane. Watu huacha familia zao na kwenda kuangalia mpira.

Kwa sasa mpira umekuwa starehe kuu kwa jamii. Mpira umekuwa burudani kuu kwa jamii za kitanzania.

Ujio wa kamari wa Kubashiri ( betting) nako kimenogesha sana mapenzi ya mchezo huo. Watu wengi kwa sasa hubeti ( betting nayo fursa nyingine) na wanapokuwa wamebeti wengi hupenda kwenda kutizama mechi walizozibetia.

Kama una ndoto za kufungua kibanda ( Soccer academy) ya kuoneshea mpira; basi fata hatua hizi:

1. Andaa mtaji wako yaani budget.
2. Chagua jina zuri na la mvuto la kuita Center yako. Hii inaitwa Brand Name. waweza kuita centa yako majina kama haya: Amsterdam Academy; Soccer Academy; Laliga; Football Academy; Old Traford; Jina la sehemu ulipo ikifatiwa na Academy; Soccer Academy. Mfano: Kyela Soccer Academy; Mererani Soccer Academy; Tandale Soccer Academy; Arusha Academy; Bukoba Academy n.k.
3. Tafuta sehemu ya kujenga banda la kuoneshea mpira. Eneo hilo lazima liwe center au liwe la kufikika na la usalama.
- Banda lako lazima liwe la kisasa lenye kuingiza na kutoa hewa. Weka Fane kila mahal; Viti waweza kutumia vya plastic au ukatumia banch. Epuka kuwa na upungufu wa viti maana wateja wanaposiama huchoka maana mpira unachukua zaidi ya lisaa moja na nusu. Weka sakafu nzuri chini na ukiweza weka marumaru ( tiles)

  • Vifaa.
- Nunuwa Flat Screen TV 2; 3; 4 au 5 kubwa kubwa ( pana na kubwa kwa ajili ya utazamaji mzuri) na ziweke mahara pa kuonekana kwa wote. Unaweza ukaweka nyingine kati kati ya ukumbi ili kuwawezesha watazamaji wa mbali kuona vizuri. Lipia king'amzi chako na inasauliwa kutumia DST decorder na lipia king'amzi chako kwa wakati

- Nunuwa Generator kwa ajiri ya emergency ya katizo la umeme.

  • Vitu vingine vya ziada
- Weka vinywaji baridi kama vile:maji na soda.
- Uza Vocha hasa hasa za Halotel kwani watazamaji wengi hukuta wako bize wakichezea simu zao upande wa Internet wakicheki taarifa za mpira hivo huhitaji Data zaidi na walowengi hutumia mtandao wa halotel.
- Mwanga wa kutosha uwepo maeneo ya sehemu ya kuangalia mpira kuepuka vibaka usiku maana mechi nyingi huchezwa usiku.

Mbinu na mikakati ya kuwashika wateja.

  • Toa free matches.
Yaani kama kuna big match ambayo itacheza saa 12 na kuanzia saa tisa saa kumi kuna match ndogo inacheza basi wateja usiwatoze pesa. wache waangalie hiyo mechi huku wakijiandaa kuangalia hiyo big match inayofata. Kwa mfano: Kama saa moja na nusu usiku kuna mechi kati ya Arsenal Vs Barcelona na kuanzia saa kumi na mbili kunacheza mechi baina ya Celtic vs Porto basi wateja walokuja kuangalia mechi ya Arsenal vs Barca waache waingie na usiwacharge pesa waangalie hiyo mechi huku wakisubili kuangalia mechi ya Arsenal.

Vile vile kama saa 11 jioni kuna mechi baina ya Chelsea na Man United na huku kuanzia saa kumi kuna mechi ya Crystal palace vs Burnley inacheza basi wateja waruhusu waingie waangalie hii mechi bure huku wakisubiri mechi inayofata ya Chelsea.
N.b Epuka kukaba kila kona hata penati! Maana yake Epuka kuonesha kuwa wewe una uchu wa pesa na unakaba kila senti. Vimechi vingine wala havina mvuto na mashabiki hivo toa kama free entry kwa wateja.

  • Weka mapaparazi. ( wanapropaganda)

Chagua vijana watano washabiki wa ligi za uingereza au wanaojua vizuri mpira na waache wawe wanaingia bure kila siku. Vijana hao chagua washabiki wa: Arsenal, Chelsea; Man U; Liverpool; Barcelona; Real Madrid ; PSG; n.k wale ambao ni wakereketwa wa timu zao. Kwa kufanya hivo unakuwa umetengeneza wakaribisha wateja kwenye center/ Acadeny yako. Hao vijana watakufanyia kazi nzuri tu ya kukusanya wateja mitaani. Pia wapenzi wa mpira wa miguu walowengi hupenda kwenda kuangalia mpira sehemu ambapo kuna makelele na mabishano. Ndo maana utakuta mechi fulani inaoneshwa bure kwenye Runinga za kawaida majumbani ila utakuta bado watu wanaenda kibandani kulipia mpira sh. 1000 au 500 ilhali nyumbani angeangalia bure tena akiwa na familia yake!
Makelele na Tambo za mashabiki ndo huwavuta wengine kuja kuangalia mpira kibandani.Usione noma kupoteza hiyo 5000 ya kiingilio cha hao watu 5 huku umeingiza Laki moja na nusi kwa mechi moja

Utapataje Faida

Kama kawaida; kifurushi champira kwenye DST huanzia elfu 80 hadi 150000 kwa mwezi.

Kwa wanaofanya biashara ya kuonesha mpira hii pesa huirudisha kwenye kiingilio cha mechi moja tu. Hebu ona kwa mfano: Mechi ya Manchester united Vs Arsenal. Utapata watazamaji zaidi ya 150. Na kwa kuwa hii ni big mechi basi kila mmoj atatoa kiingilio cha sh 1000 hivo basi utapata zaidi ya laki na nusu. Na hapo ni Mechi moja kwa siku. Sasa mwezi mmoja una big mechi ngapi? Una mashindano mangapi maarufu!?

Kwa taarifa yako; Wanaofanya biashara ya kuonesha mpira siku za Week End ( Jumamosi na Jumapili) kwao ni siku za mavuno kianzia mchana hadi usiku. Pia kati kati ya wiki kunakuwaga pia na mashindano mbali mbali hivo huvuna mapesa pia maradufu.

Nb:
Pengine una mtaji na hujaona ufanye buashara gani; basi usiwaze kununuwa bajaji; kununua Noah; kujenga nyumba za kupangisha au kufungua duka n.k. Biashara nzuri na ambayo haina ushindani mitaani ni biashara ya mpira. Ili kufungua biashara hii yakupaswa kuwa na mtaji wa Milioni 7 hadi 10 kama kweli utakuwa umedhamilia kuifanya vizuri na kisasa hii biashara. Nakuhakikishia hii hela yako utairudisha ndani ya muda mfupi sana. Fungua biashara kisasa ili upate wateja wengi na wa kisasa ambao wako smart.

Hapa nchini biashara nyingi ni za kuigana. kwamba mmoja akifungua duka hapa na mwingine anafungua tena duka hopo hapo jirani. Mmoja akifanya hiki na mwingine anaiga anafungua the same business pembeni hali ambayo inapelekea uhasama na kununiana mpaka naenda kwa waganga wa kienyeji kufanyiana mbaya. Nakuhakikishi; biashara ya mpira iko special na si ya kuigana maana waliowengi hawajui hii fursa na kwa taarifa yako watanzania hatujajua kuwa mpira ni biashara bali hujua kuwa mpira ni burudani.

Viva Football!
 
Iko poa sana hii
 
Back
Top Bottom