Nafasi ya Timu zingine kwenye Mpira Tanzania

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Wanakamati, hadi muda huu ikiwa timu zote zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi licha ya kupigiwa promo sana ni mechi mbili pekee zimejaza uwanja, Mechi iliyochezwa na Yanga na nyingine ni mechi ya jana iliyochezwa na Simba na JKU. Hii inatupa ujumbe gani?

Tutakubali kuwa Simba na Yanga zinabeba mpira wa Tanzania kwenye mashindano yote zinazoshiriki, ya ndani na nje. Azam na Singida Fountain Gate licha ya ukubwa wao mechi zao hazikuwa na watazamaji wengi, hata hii inayoendelea sasa ya Azam na Vitalo uwanja ni mtupu kabisa.

Mechi zinapigiwa Zenji na hata zimecheza timu za Zenji pia watazamaji walikuwa wachache.

Kuna msemaji mmoja wa Timu moja hupenda kujipachika kundini, lakini hebu sasa aone nafasi yao halisi kwenye vichwa na mioyo ya wapenzi wa Kandanda.

Tusiogope kuzipa maua yao Simba na Yanga na tuzitambue kama utambulisho wa mpira wa Tanzania. Yaani hata ile mtu ukiwa Morocco unaweza kujitambulisha kuwa unatoka Tanzania inakotoka Simba Sports Club!
 
Hapo ndio ujue uzalendo watu wanazaliwa nao haukopwi wala kufundishwa na wanasiasa uchwala.

Ulaya kila mji unashangilia timu iliyopo kwenye mji wake. Ndio maana timu kama Leeds , Newcastle na Aston villa zina mashabiki wake na zinajaza uwanja.

Hapa kwetu watu kutoka Geita au Dodoma jiji timu ikicheza na Simba au Yanga za kariakoo wanashabikia hizo.
 
Back
Top Bottom