Wapenzi Wa Movies na Netflix

Wapenzi Wa Movies na Netflix

Kaputupu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
1,486
Reaction score
1,179
Technology inaenda kwa kasi sanaa..
Naomba niongee kitu kuhusu wapenzi wa movie na Netflix,
Nimekuwa mtumiaji wa netfllix almost 2 years now!!
Japo sio mtumiaji sana lakini, kwa sababu nina Apps nyingine za kutosha kwa ajili ya kudownload na kuangalia movies pia..

Kuhusu matumizi ya Netflix unapaswa kulipia kila mwezi kulingana na package unayotumia,,
Kuna basic standard pamoja na premium!!
Kila package ina maximum users!!

Nalipia premium kila mwezi elfu 30,000
(12.99$)
Bt maximum users ni watu watano

Mtu mwingine anaweza akakushanga kulingana na uchumi wa nchi yetu etc!
“Unalipa elfu 30,000 kila mwezi kwa sababu ya Netflix tuuu!!!?
Aahh mkuu basi una hela!!”

Siri iko hivi
Ni kweli nilikuwa Nalipa mwanzo, lakini baadae nikapata marafiki ambao
Pia wanapenda movies kama mimi!!
Kama tunaweza kuwa watu watano..
Kwa nn tusipitishe mchango wa elfu saba saba kila mwezi tukapata 35,000
Na tukailipia netflix yetu..
Kweli tumefanikisha hilo

“Tulitengeneza group la WhatsApp
Tukajiweka humo lakini sisi tukafanya hivi mwezi huu analipa, mwezi huu analipa huyu hadi hadi mzunguko wa watu watano unaisha””
Mnaweza kuwa watu watano kwenye account moja kila mmoja akawa na option ya kutengenza list ya movies zake etc..

Changamoto iko hapa
Kwenye kufanya malipo netflix wanataka visa au MasterCard..
Wabongo wengi sisi ni waoga sana,
Mtu anasema siwezi ku Add Account yangu ya bank, watanikata hela hukoo kila siku., mara oohh its not safe etc..
Lakini VODACOM wametuletea Mpesa Mastacarard.

So Problem solved..
Tengeneza account yako ya M-Pesa mastacard then details unazopewa Ndo details zinazotakiwa na netflix unapotaka kulipia Account yako..
(Kadi namba, mwezi na mwaka wa ku expire kadi pamoja na CVV)


NB: huu uzi wangu sio kufanya tangazo la Netflix wala mastacard kutoka vodacom..
Ila ni kuwajuza wapenda movies wenzangu.
Asante..

IMG_5649.JPG

IMG_5649.JPG

IMG_5650.JPG

IMG_5647.JPG
 
Netflix ndiyo entertainment ya kulipia hela ndogo kuliko zote kwa kipimo cha money value.

For the price of one lunch you can watch movies for a month.

Of course it depends on your situation.

Mimi niko sana kwenye Plex na Kodi servers, Netflix si kwa sana siku hizi. Ila nimekuwa member mfululizo tangu 2002. Tangu tunaletewa vibahasha vyekundu vyenye DVD by mail.

Ila kwa sasa kila wiki sikosi kumuangalia Hasan Minhaj katika "Patriot Act".
 
Kiranga,

Sure Jamaa anajua sanaaa
Hivi ni anatoa kila weeek au!!!

Mm nimemaliza collection ya Travor Noah
Juzi!!

Leo asubuhi nimeanza ka series kamoja kazuri sanaa
Kanaitwa YOU!!!
 
Sure Jamaa anajua sanaaa
Hivi ni anatoa kila weeek au!!!

Mm nimemaliza collection ya Travor Noah
Juzi!!

Leo asubuhi nimeanza ka series kamoja kazuri sanaa
Kanaitwa YOU!!!
Trevor ni chizi.

"YOU" niliitazama ilivyotoka. Ilikuwa bonge la gumzo. Nafikiri ilivunja rekodi za Netflix kwa kutazamwa sana.

Hasan Minhaj yupo kwenye season sasa anatoa show mpya kila week.

Kesho kutakuwa na show mpya sitakosa kuiangalia. The guy is funny and smart.
 
Mimi ni mmoja wapo wa Netflix maana napenda sana kuangalia movie pamoja na series. Uzuri wa Netflix unaweza kuangalia kwenye simu/ iPad tv na malipo ninayolipia ni hayo hayo. Na wana international movie nyingi tu. Ila tatizo lao movie zikiwa mpya Netflix huwa hawana. Na series nyengine zinachelewa kutoka new season kama queen of the south kuna new season inakaribia kuisha wakati Netflix bado. Nina app nyengine ya tea tv movie zikitoka haichukui muda unapata tea tv.
 
Daah nilikuwa mpenz sana wa Netflix but kulingana na hali ya uchumi nimejiondoa huko ila nakiri kabisa kuwa nakuwa mpweke sana wadau.
 
Mimi ni mmoja wapo wa Netflix maana napenda sana kuangalia movie pamoja na series. Uzuri wa Netflix unaweza kuangalia kwenye simu/ iPad tv na malipo ninayolipia ni hayo hayo. Na wana international movie nyingi tu. Ila tatizo lao movie zikiwa mpya Netflix huwa hawana. Na series nyengine zinachelewa kutoka new season kama queen of the south kuna new season inakaribia kuisha wakati Netflix bado. Nina app nyengine ya tea tv movie zikitoka haichukui muda unapata tea tv.

Hiyo tea tv ni ya kulipia au inapatikana vipi mkuu...?

Na pia, Netflix ina kipi cha ziada ukilinganisha na apps nyingine kama vile Showbox etc
 
Shida naona sio kulipia hyo package ya netflix,ila ipo kwemye kumudu gharama za kustream hzo movie.ukizingatia wabongo wengi huwa tunatumia mobile data,naona kwa wale wanaomitumia broadband kuna unafuu kidogo.
 
Kwa Hiyo ukilipia Netflix bado Tena inatakiwa ununue vifurushi vya Internet?
Ndio ila mimi Nina broadband. Internet ni masaa yote inakuwa nafuu maana starehe yangu kubwa ni movie . Na movie zake nazi katikati zinaonyesha safi tu
 
Ulipie kwa mwezi kisha ulipie mb kuangalia.Ukiangalia unaiacha hukohuko humpi rafiki nae aangalie

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea umechukua package ya aina gani. Kuna nyengine unampa pin namba mwenzako na wao wanaona. Kama unaona mb zinakula una download. Ila kwenye ku download sijui mpaka utumie Wi-Fi hapo sina uhakika
 
Inategemea umechukua package ya aina gani. Kuna nyengine unampa pin namba mwenzako na wao wanaona. Kama unaona mb zinakula una download. Ila kwenye ku download sijui mpaka utumie Wi-Fi hapo sina uhakika
Wakuu tusaidieni hapo kwenye ku download aisee wengine ni wapenzi wa offline aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom