Wapenzi Wa Game PC

mabakila1

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2020
Posts
482
Reaction score
614
Kama kichwa cha Habari kilivyo wengine sio ma expert sana jinsi ya kupakua game kali online
Ila mie natafuta wajuz na wapenz wa hili game la "FOOTBALL MANAGER " nataka nijue jins la kulipata free tena hii version mpya kingine nataka ufaham wa kutumia hii "Game Pass" kwenye Microsoft store ni kwa ajili ya Xbox tu?
 
Latest ni 22 ila ina gb 50 ichek CPY na sijajua kama washatoa crack au la.
FOOTBALL MANAGER 20 ya pc ichek fitgirl repacks lakini ina gb kama 35 kutegemea na mirror utakayotumia.
ila kwa ushauri kwanini usichukue pes maana gameplay yake ni friendly kuliko FM NA fifa.
 
Mi natumia gamepass, na nacheza football manager 2022, nunua code ya miezi 3 kama 5000 hivi kwa 3rd party seller then paste tu hio code kwenye xbox app. Kuna magame zaidi ya 100 utacheza kwa bei hio hio
 
Sio lazima uwe na console ya Xbox App ndo uchezeee
 
Mzee GB 50 niandae bando la kutosha sasa
 
Mie napenda Football Manager sana napenda mpira mnoo napenda kua Manager 😂😂
 
mimi napenda kikifika kipindi cha usajili tu kutumia hela yan unapiga cheat moja matata unakuwa na mpunga ambao unasajili mchezaji wowote yule unayemtaka halafu wengine unawapigisha bench wanaanza kuandamana eti hawana furaha kama binadamu kweli vile utasema dah dawa yao nawapiga transfer list na loan lost wote kidomodomo kinaisha hawawez kunipangia kikosi wakati mm ndiye boss wao [emoji23][emoji23]mm ndiye napanga nani acheze nani asicheze hutaki sepa
 
Mi natumia gamepass, na nacheza football manager 2022, nunua code ya miezi 3 kama 5000 hivi kwa 3rd party seller then paste tu hio code kwenye xbox app. Kuna magame zaidi ya 100 utacheza kwa bei hio hio
mbona kwangu gamepass inazinguaa
 
Naipataje mkuu izo code naomba muongozo

Sent from my SLA-AL00 using JamiiForums mobile app
Site mbalimbali kama Kinguin ila nimecheki sasa hivi hamna.

1. Unaingia Kinguin unasearch pale juu Gamepass

2. Unatafuta ya bei rahisi most of time chini ya 5000 kwa miezi 3. Inakuja kama Euro 1 ama 2.

3. Angalia nchi uliyonunulia inaweza kuwa gamepass ya UK, USA, Uturuki, etc.

4. Tumia Vpn fungua account ya microsoft ya hio nchi, redeem code.

5. Login na hio code kwenye app ya Xbox ya windows, vpn inatumika ku redeem tu code hapo juu, kudownload games na kucheza hakuna haja ya vpn.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…