Wapenzi wa dhati wa CCM - Ushauri Makini ni huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapenzi wa dhati wa CCM - Ushauri Makini ni huu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anaruditena, Oct 18, 2010.

 1. A

  Anaruditena Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanachama wote wa CCM ambao ni wapenzi wa dhati kweli kweli - wa chama cha wakulima na wafanyakazi, cha misingi ya Azimio la Arusha, basi October 31, ni kuchagua Chadema ili tupate nafasi ya kurudisha chama chetu toka mikononi mwa mafisadi wachache- chama kimetekwa nyara na watu wachache wenye pesa.

  Mwakani tuanze mchakato wa kupata Mwenyekiti na katibu safi na uongozi kwa jumla na sio uongozi wa familia mbili ( JK na Makamba) na tuanze kujenga chama chetu na ifikapo 2015 mafisadi wote nje ya chama.

  Tukubali matoke kwa faida ya chama chetu CCM, ama sivyo hali yetu ya mbeleni itakuwa mbaya sana - kama KANU. Watanzania wengi wamekuwa waelewa ya hatima ya maisha yao; weekend hii nimeongea na ndugu walio kijijini sana na hata Dr. Slaa hajafika huko lakini wanasema watachagua Dr. Slaa kama raisi wao. Mimi nimeshakata tamaa kwa mwelekeo unavyokwenda.
   
 2. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hili nalo neno, Slaa for President
   
 3. dazenp

  dazenp Senior Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hahahahaha Malaria Sugu hahahahahahahahahahahahah..hahahahahah..............inaelekea kimekuuma
   
 4. Mtuflani

  Mtuflani JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 323
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  We Malaria sugu hiki ni kizazi kipya hatuwezi kuishi kwa mitazamo ya wazee,zama walizoishi sio sawa na sasa.Tunahitaji mawazo mapya!!!!!!!!!!!Go Slaa ikulu is yours.
   
 5. L

  Lorah JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  hahahahahahah mweleze, nilisikiaga kwamba jina la mtu huwa linahusiana sana na maisha yake sikujua kwamba hata majina ya utani nayo pia


  Malaria sugu yani wewe mada zako kwa kweli ni za kimiujiza yani utafikiri Mdogo wa makamba......

  poor you, Maleria haiwezi kuisha mpaka CCM iondoke madarakani, Nenda Muhimbili, Dodoma General, uone wamama wanavyoteseka hakuna vifaa vya kuzalishia halafu uje uongelee CCM....

  Kampeni zangu sasa hivi nafanya Hospitalini Kitanda kwa kitanda, Nauliza Mgonjwa toka uje umepata dawa bado, kwa nini dawa hamna, Basi ni muda wa Mabadiliko Kikwete BASI, Kaka na Kitambaa cha kichwa sio Kipimo cha uongozi bora ..... nawavuna kweli .... Sasa Maleria Sugu lazima upone....
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Malaria Sugu ni mzee wa mwaka 1947,yeye ni wale ambao wamekunywa maji ya bendela!ukiwaulliza kuhusu CCM watakwambia CCM ndiyo Baba,ndiyo mama.Tusijisumbue kuomba kura yake!
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Good idea,Hongera kwa kuona mbali maana kama wanaccm watamchagua Kikwete halafu akashinda basi ndo mwisho wa ccm,maana ahadi alizo ahidi ni za kuichimbia ccm kaburi,hawezi kutekeleza na analijua hilo.Ila kwa sababu anajua hatorudi kwa wananchi 2015 basi zigo litakuwa kwa ccm na wagombea wao wakati huo.Huyu jamaa yenu ni mbinafsi kweli.

  "OKOA CCM KUTOKA KWA MAFISADI KWA KUMCHAGUA DR. SLAA."
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  KINYIMA KURA CCM MWAKA HUU, SIO KUICHUKIA, BALI NDIO KUIJENGA, ILI IKAE PEMBENI IYANGALIE NA UBUNIFU WA WENGINE, MAANA SIWEZI KUPIGIA KURA CHAMA AMBACHO, WAO KILA JAMBO ZURI WANASEMA HALIWEZEKANI, MFANO ELIMU BURE NA MATIBABU BURE. HILI HALIITAJI DEGREE KULIONA KWAMBA NI VITU VINAVYOWEKANA. REJEA MIMI NIMEANZA PRIMARY SCHOOL MWAKA 1985, LAKINI MPAKA MADAFTARI TULIKUWA TUNAPEWA BURE, DAFTARI MBELE LIMEANDIKWA HALIUZWI. MWAKA HUU MIMI BINAFSI KAMA KUNA SHARTI LA MACHAGUO MAWILI KATI CCM AU KIFO, BASI MIMI NITACHAGUWA KIFO. NI HERI UFE UKIWA UNAPAMBANA, KULIKO KUFA UKIWA UMEPIGA MAGOTI.:A S thumbs_up:
   
 9. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  natamani kujua hawa watu wanaochangia mada humu ndani kwa majina yao halisi kabisa ningefurahi.
   
Loading...