Wapendwa naomba jibu

EPORA

Member
Apr 8, 2012
83
16
Heri ya pasaka,kwa kifupi nahitaji msaada wa mawazo,nilikuwa na mchumba mpendwa ktk Bwna kama mimi,na tangu mwanzo tulikubaliana sisi kama wakristo hatutakiwi kufanya tendo la ndoa hadi wkt wa ndoa,hilo lilipita bila kupingwa,na ktk kipindi hicho alisema mwk 2012 angeenda kujitambulisha na kwa bahati baba yake kamjibu hadi arudi nchini december,
Sasa ni hv majuzi niligundua kitu,nilikutana nae maeneo ya mlimani city,wkt nipo nae best yangu akawa amenipigia cm kwmba amekuja dar,cm yangu haikuwa na hela nikaomba yake niitumie kumjibu best,nikajikuta inbox nikapigwa na butwaa kwa kuona msg zinaonesha ametoka kufanya uzinzi siku 2 nyuma.
Niliamua kumuuliza ili aniambie ukweli na alikiri kwmba shetani alimpitia anaomba nimsamehe kwa uzinzi wake,ila nimeshndwa kumsamehe na uchumba nimeuvunja je?wapendwa nipo sahihi?naombeni mawazo yenu!
 
pole samehe kama una kifua cha kusamehe,otherwise songa mbele magonjwa mengi siku hizi ,lol mind you muonja asali haonji mara moja.......
 
mi kwa kweli ningempongeza kwa kujua ni kidume cha mbegu.....mwanaume asiye na skendo hata moja hafai.....
 
Mtu hataishi kwa mapenzi ya nadharia tu, kuku wako mwenyewe umchunguze wa nini?

Anyway, kakuona weye labda waif matirio akaona aende na jinsi unavyotaka huku yeye naye anajilia pembeni kwa siri maana inaonekana wewe ndo hutaki kumpa chezo.

La pili, yawezekana anakulia time, ukimpa chezo anasepa fasta.

Uwe mbayuwayu maana wewe ndo unamfahamu, sie tunahisi tu.
 
mi kwa kweli ningempongeza kwa kujua ni kidume cha mbegu.....mwanaume asiye na skendo hata moja hafai.....

hahahahaha! Tena bora ameanza kupata maujuzi pembeni asije akatia aibu ndani ya ndoa.
 
Kamwe usitarajie mahusiano yaliyonyooka! Umefanya kosa kuvunja uchumba, kumbuka hata Petro alifanya maasi mengi, ila alipewa ukuu wa kanisa kwa kuwa alikuwa ANASTAHILI. Jitahidi kujua kama anaendelea na huo mchezo mchafu. Inawezekana aliingia dhambini kwa kushawishiwa na si kushawishi.
 
Heri ya pasaka,kwa kifupi nahitaji msaada wa mawazo,nilikuwa na mchumba mpendwa ktk Bwna kama mimi,na tangu mwanzo tulikubaliana sisi kama wakristo hatutakiwi kufanya tendo la ndoa hadi wkt wa ndoa,hilo lilipita bila kupingwa,na ktk kipindi hicho alisema mwk 2012 angeenda kujitambulisha na kwa bahati baba yake kamjibu hadi arudi nchini december,
Sasa ni hv majuzi niligundua kitu,nilikutana nae maeneo ya mlimani city,wkt nipo nae best yangu akawa amenipigia cm kwmba amekuja dar,cm yangu haikuwa na hela nikaomba yake niitumie kumjibu best,nikajikuta inbox nikapigwa na butwaa kwa kuona msg zinaonesha ametoka kufanya uzinzi siku 2 nyuma.
Niliamua kumuuliza ili aniambie ukweli na alikiri kwmba shetani alimpitia anaomba nimsamehe kwa uzinzi wake,ila nimeshndwa kumsamehe na uchumba nimeuvunja je?wapendwa nipo sahihi?naombeni mawazo yenu!
Tupa kule huyo, mimi natafuta mchumba..au unasemaje!.
 
Mimi ni mkristo na naamini katika utatu mtakatifu lakini nikiri kabisa kwa dunia hii ya leo hii notion ya sex baada ya ndoa ina challenges nyingi.Sitaki kuleta malumbano mengine nje ya hii thread lakini mkuu jiulize maswali kwamba je wakati mnapatana kuhusu kufanya mapenzi kabla ya ndoa wote mlikuwa bikira?Je mli-consider udhaifu wa kibinadamu kati yenu?Ukipata majibu ya maswali hayo naomba give him/her another chance.
 
Ulichokifanya kinaweza kikawa ni sahihi kama kuna mwanaume ambaye yuko perfect on ur way
 
Mimi ni mkristo na naamini katika utatu mtakatifu lakini nikiri kabisa kwa dunia hii ya leo hii notion ya sex baada ya ndoa ina challenges nyingi.Sitaki kuleta malumbano mengine nje ya hii thread lakini mkuu jiulize maswali kwamba je wakati mnapatana kuhusu kufanya mapenzi kabla ya ndoa wote mlikuwa bikira?Je mli-consider udhaifu wa kibinadamu kati yenu?Ukipata majibu ya maswali hayo naomba give him/her another chance.

hamna udhaifu wa kibinadamu,mbona hatubaki kuku???yote inaongozwa na brain....ukiiambia akili yako usifanye ngono hufanyi ng'o!
 
angekuwa mume ningefikiria ila mchumba hapana siwezi,magonjwa mengi sikuhz

Dada pole, kwa sababu naweza imagine jinsi moyo unavyovunjika ukigundua hilo. Kwa mimi naona ulimshirikisha Mungu kulingana na masharti mliyowekeana Ila kumbuka hivi;
a)BWANA ASIPOILINDA NYUMBA AILINDAYE AFANYA KAZI BURE..kweli ulitakiwa umuombee na sio kusearch cmu yake kwa sababu wewe ni binadamu tu na hata hizo msgs angezifuta usingehisi kitu.
b) Kama ndiye mume Bwana amekupa hata kama kaanguka (Kumbuka in the face of light kuanguka si kuzini peke yake-wewe mwenyewe unaweza kuwa umemuudhi Mungu in one way or another, msamehe na mrudishe kundini huyo kondoo aliyepotea), He is still the best for you. Na ukienda kwa mwingine you will be settling for the second best while you had the best.

c) Sikuambii umrudie ila unatakiwa uchunguze kwanza 'Is he your ideal husband?'

d) Kwa kukusaidia tu on preliminary analysis huyo jamaa mwizi mzoefu kwa sababu (i) kama alipitiwa na shetani angekuwa anajifeel guilty na hata kama asingekuambia ungehisi change of behaviour akikuona (ii) Angefuta hizo msgs ili zisionekane na sio na wewe tu, bali hata kwa mtu yeyote coz c tabia yake..
 
mwanaume akikwambia "sawa hatufanyi mapenzi mpaka ndoa" ogopa...sio kwamba hafanyi mapenzi kabisa...la hashaaa...ni kwamba hafanyi mapenzi na wewe...
 
mm ningependa kukushauri kuwa uachane naye kwani kama ameshindwa kuwa mwaminifu sasa hv asikudanganye kuwa atakuwa mwamininifu siku nyingine. mtu asipokuwa mwaminifu kwa mambo madogo hawezi kuwa mwaminifu kwa mambo makubwa. Tena huyo siyo Mkristo ni kahaba ambaye amekuja kanisani kuvuna mabinti innocent kama wewe. take care hata Yuda hakuishia kupokea vipande vya fedha tu bali aliendelea akamsaliti Yesu Kristo na kisha akajinyonga

huo ni mtego alioutega shetani ili akikunasa, akuoe, akuambukize magonjwa na uishie kufa kabla ya wakati wako

kumbuka mke/mme mwema hutoka kwa Mungu
 
ivi kakwambia shetani alimpitia, ati alimkuta wapi vile hata akampitia?

kumbuka zinaa inafanywa kwa hiari ya mtu mwenyewe wala hakuna cha kupitiwa na shetani kwani alimkuta amekaa wapi hadi amupitie? kwani shetani hakuona watu wengine wa kuwapitia hadi ampitie yeye tu? shtuka achana naye
 
mm ningependa kukushauri kuwa uachane naye kwani kama ameshindwa kuwa mwaminifu sasa hv asikudanganye kuwa atakuwa mwamininifu siku nyingine. mtu asipokuwa mwaminifu kwa mambo madogo hawezi kuwa mwaminifu kwa mambo makubwa. Tena huyo siyo Mkristo ni kahaba ambaye amekuja kanisani kuvuna mabinti innocent kama wewe. take care hata Yuda hakuishia kupokea vipande vya fedha tu bali aliendelea akamsaliti Yesu Kristo na kisha akajinyonga

huo ni mtego alioutega shetani ili akikunasa, akuoe, akuambukize magonjwa na uishie kufa kabla ya wakati wako

kumbuka mke/mme mwema hutoka kwa Mungu

Umemaliza. Watu ambao si clean huwa wa kwanza kwa kutafuta watu walio clean!
 
Back
Top Bottom