Wapendwa,habari za mchana

Wapendwa,habari za mchana

Lengo ni nini hasa?

(A) Kumdhuru aliyekutapeli ?
(B) Au aliyekutapeli akurudishie hela yako.?.

Jibu Kama ni A nenda kwa waganga wa kienyeji na ikukupendeza zaidi msamehe tu karma it will pay you all debts.
 
Kwakweli hiyo zaburi 109 Ukiisoma kwa siku 31 hiyo kitakachompata ni hatari zaidi maana yenyewe inasema hivi

ZABURI 109
1. Usinyamaze, ee Mungu ninayekusifu!

2. Watu waovu na wadanganyifu wanishambulia,
wanasema uongo dhidi yangu.

3. Wanasema maovu juu yangu,
na kunishambulia bila kisa.

4. Ingawa niliwapenda, walinishtaki,
hata hivyo niliwaombea dua.
5Wananilipa uovu kwa wema wangu,
na chuki kwa mapendo yangu.

6. Umweke hakimu mbaya dhidi ya adui yangu;
na mshtaki wake ampeleke mahakamani.

7. Anapohukumiwa apatikane na hatia;
lalamiko lake lihesabiwe kuwa kosa jingine.

8. Siku za maisha yake ziwe chache,
mtu mwingine na achukue kazi yake!

9. Watoto wake wawe yatima,
na mke wake awe mjane!

10. Watoto wake watangetange na kuombaomba;
wafukuzwe katika magofu ya nyumba zao!

11. Anayemdai kitu amnyanganye mali yake yote;
na wageni wanyakue mapato ya jasho lake!

12. Pasiwe na mtu wa kumwonea huruma,
au Kuwatunza watoto wake yatima!

13. Wazawa wake wote wafe;
jina lake lisahauliwe katika kizazi kijacho!

14Mwenyezi-Mungu aukumbuke uovu wa wazee wake,
dhambi za mama yake zisifutwe kamwe!

15. Mwenyezi-Mungu azikumbuke dhambi zao daima;
lakini wao wenyewe wasahauliwe duniani.

16. Mwovu huyo hakujali kabisa kuwa na huruma,
ila aliwadhulumu maskini na fukara,
kadhalika na watu wanyonge mpaka kifo.

17. Yeye alipenda kulaani watu,
laana na impate yeye mwenyewe.
Hakuwatakia wengine baraka,
basi, asipate baraka yeye mwenyewe.

18. Kwake kulaani ni kama kuvaa nguo,
basi, laana hizo zimloweshe kama maji,
zimwingie mifupani mwake kama mafuta.

19. Laana zimfunike kama nguo,
zimzunguke daima kama ukanda.

20Mwenyezi-Mungu awalipe hayo hao watu wanaonishtaki,
naam hao wanaosema mabaya dhidi yangu.

21. Lakini ee Mwenyezi-Mungu, Bwana wangu,
unitendee kadiri ya hisani yako;uniokoe, kwa sababu ya wema wa fadhili zako!

22. Mimi ni maskini na fukara;
nimejeruhiwa mpaka moyoni mwangu.

23. Natoweka kama kivuli cha jioni;
nimepeperushwa kama nzige.

24. Magoti yangu yamenyongonyea kwa mfungo;
nimebaki mifupa na ngozi.

25. Nimekuwa dhihaka tupu kwa watu;
wanionapo hutikisa vichwa vyao kwa dharau.

26. Unisaidie, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu;
uniokoe kadiri ya fadhili zako.

27. Waoneshe watu kuwa ndiwe uliyetenda hayo,
wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe uliyefanya hivyo.

28. Waache walaani, lakini wewe unibariki;
wanaonishambulia waaibike, nami mtumishi wako nifurahi.

29. Maadui zangu na wavishwe fedheha;
wajifunike aibu yao kama blanketi.

30. Nitamshukuru sana Mwenyezi-Mungu kwa sauti;
nitamsifu kati ya kundi kubwa la watu,

31. kwa maana yeye humtetea maskini,
humwokoa wakati anapohukumiwa.

Nadhani hii ni zaidi ya albadri
 
Maombi au sala kama hiyo ilikuwa sahihi wakati wa Agano la Kale. Wakati huu wa Agano Jipya sio sahihi kwa Mkristo kuomba kama mwandishi wa Zaburi 109 alivyoomba. Hiyo ni sala ya laana (imprecatory psalm). Mwandishi wa Zaburi hiyo aliomba Mungu awaadhibu vikali adui zake.

Yesu Kristo alituletea Agano Jipya. Ndio sababu Yesu na mitume wake walifundisha mtazamo tofauti juu ya adui.

Yesu anatufundisha kuwapenda adui zetu. Kwa mantiki hiyo alibadilisha mtazamo wa kulipiza kisasi kwa kuhimiza upendo na msamaha:
Mathayo 5:44 – “Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.”

Katika Agano Jipya, Paulo anatuhimiza pia kuwabariki hata wale wanaotutesa badala ya kuwaombea mabaya:
Warumi 12:14 – “Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msiwalaani.”

Katika Agano Jipya tunatakiwa kumwachia Mungu. Yeye ndiye atakayelipa kisasi:
Warumi 12:19 – "Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”

Hata Yesu aliwasamehe waliomtesa. Alipokuwa msalabani, hakuwalaani watesi wake kama katika Zaburi 109, bali aliomba Mungu awasamehe:
Luka 23:34 – “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.”

Zaburi ya 109 inatufundisha tu jinsi zamani ilivyokuwa sawa kumuombea adui mabaya. Lakini kwa sasa tunafuata mafundisho mapya ya msamaha, upendo, na kuwaombea baraka maadui zetu. Kwahiyo, usiitumie Zaburi hiyo kama mwongozo wa sala yako. Ukisali au ukiomba hivyo utakuwa unaomba kinyume na mapenzi ya Mungu, na kwa sababu hiyo maombi hayo hayatajibiwa.
Mpaka hapo naamini Mwanamke wa mithali 31 amepata jibu sahihi.
 
Ahsante nimekuelewa
 
Kazi nzuri
 
Back
Top Bottom