Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma(CDA) imetoa notisi kwa wapangaji wa nyumba zake 174 zilizopo Kikuyu Mjini hapa ambazo ni za ghorofa mbili kuhama ili kupisha ukarabati mkubwa wanaotaka kufanya.
Akizungumza leo Ofisa habari na mahusiano wa CDA, Angela Msimbila amesema, walishatoa notisi ya siku saba ya kuwataka wapangaji wote kuhama ili kupisha ukarabati mkubwa unaotakiwa kufanyika kwenye nyumba hizo ukiwemo wa majengo, mifumo yote ya umeme, vyoo na majitaka.
Amesema awali wapangaji hao walikuwa wakilipa kodi ya Sh. 18,000 kwa nyumba yenye vyumba viwili na sebule, kodi ya Sh 20,000 kwa nyumba yenye vyumba viwili, sebule na sehemu ya kulia chakula, kodi ya Sh 22,000 kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule na sehemu ya kulia chakula.
“Hata hivyo mwaka 2008 CDA ilifanya mabadiliko ya kodi za nyumba katika maeneo mbalimbali ikiwepo nyumba za Maghorofa ya Kikuyu, mabadiliko hayo yaliongeza viwango vya kodi katika nyumba hizo kwa kuzingatia uwiano wa kodi katika soko” amesema Msimbila na kuongeza kuwa, “Ongezeko hilo la kodi lilitaka wapangaji kulipa kodi kati ya Sh. 50,000, Sh,55,000 na Sh. 65,000 jambo ambalo wapangaji wetu hawakukubaliana nalo na kwenda kufungua kesi mahakamani
Amebainisha kuwa baada ya ukarabati kodi katika nyumba hizo zitapanda na kuwa Sh, 120,000, Sh 130,000 na Sh l50,000 na wapangaji watakaokuwa na vigezo watapangishwa nyumba hizo na mamlaka.
Msimbila amesema mwaka 2008 wapangaji walipeleka kesi mahakamani (Baraza la Ardhi) kupinga kupandishwa kwa viwango vya kodi na kesi hiyo ikaanza kusikilizwa ambapo tangu kipindi hicho kumekuwa na mwendelezo wa kesi mbalimbali za kupinga ongezeko la kodi mpaka mwaka 2016
Ameeleza kuwa kutokana na kesi hizo wapangaji zaidi ya 150 waligoma kulipa kodi tangu wakati huo na kuisababishia mamlaka hasara kubwa.
Msimbila amesema CDA imekuwa ikikusanya kodi jumla ya Sh. 3.4 milion kwa mwezi bila kodi ya ongezeko la Thamani(VAT) na ukitoa kodi hiyo mamlaka imekuwa ikipata Sh. 2.9 milion.
“Tuna deni la Sh 345,257,000 kuanzia mwaka 2008, kila siku wanazua kesi mpya ili wasilipe kodi na hizi nyumba huwa zinahitaji ukarabati na haziwezi kukarabatiwa watu wakiwemo ndani kwani ukarabati unatakiwa kufanyika ni mkubwa ” amesema msimbila
CDA imetenga fedha za ukarabati wa majengo hayo katika mwaka wa fedha 2015/2016, ilitangaza zabuni na kumpata mkandarasi wa kufanya ukarabati ambapo kwa sasa mamlaka hiyo imejipanga kufanya zoezi la kuwaondosha wapangaji watakaokaidi ilani ya kuwataka kutoka ndani ya siku saba kwa kutumia dalali.
Hata hivyo mwenyekiti wa wapangaji wanaoishi kwenye maghorofa yanayomilikiwa na CDA
Kikuyu, John Shelukindo alisema kuwa ongezeko la kodi ni kubwa mno kwao ambalo hawawezi kulimudu.
CHANZO: Mwananchi