Wapambanaji tukutane hapa

Kuna mganga mmoja wa kweli. Ila masharti yake sasa! Utayaweza? Kama unadhani utayaweza niambie nikuelekeze.
 
Huyo fundi wa image kilolo ni mwamba ? Huo wa kidonda sugu unakuaje?
Huyu Fundi wa Kilolo ni wa moto haswaa,madereva wengi wa miaka ya nyuma wanamjua huyu mwamba,alikua anawapa midoli yake hiyo hata suka achape usingizi ila chuma unakuta iko kibati na ina overtake.

Siku hizi anatoa ule wa Mtungi kwenye Kona na kifimbo.
 

Mtungi kwenye kona nakifimbo ndo upoje
 
Mtungi kwenye kona nakifimbo ndo upoje
Huo unaambiwa utenge chumba maalum cha kuweka huo mtungi wako,unatengwa katika pembe ya tatu ukihesabu kutoka kushoto kwako kwa mlango.

Huo mtungi kila kukikucha utakuta pesa imejaa mpaka imefulumia juu(imeumka,imetuta),so wewe kazi yako ni kwenda kufanya leveling kwa kutumia kile kifimbo.
Unalevel kupunguza kale kanundu/kamlima ka pesa pale juu ya huo mtungi. Kifuatacho hapo ni kutumia hiyo pesa iloanguka hapo chini mpaka iishe siku hiyo,na kesho tena unafanya hilo zoezi.
 
Dah unatumia hela hio kula au kufanyaje sasa na vipi kama ni nyingi sana😅 au inakuwa ndogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…