Waombaji 25532 wa mikopo elimu ya juu wapata awamu ya kwanza

inasikitisha, inaumiza na inafurahisha pale mtu unapokuwa na hamu ya kujua mkopo umepataje afu unakuta umepata 4000 wakati school fees ni 1.3 M.
 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa mikopo kwa wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza 25,532 kati ya 41,000 walioomba kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Oktoba 17, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema dirisha la upokeaji wa maombi lilifunguliwa Mei 5 hadi Oktoba 10, 2018.

Amesema walioomba na kukamilisha kwa usahihi ni 67,000 na waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) walikuwa 49,000.
Mkurugenzi huyo amesema kati ya hao 49,000 waliodahiliwa na TCU, 41,000 waliomba mikopo.

Amesema kati ya hao 41,000 ni wanafunzi 25,532 wa awamu ya kwanza wamepata mikopo yenye thamani ya Sh88.36 bilioni huku wanafunzi 69 wanaosoma nje nchi nao wakinufaika na mikopo hiyo.

Badru amesema kati ya idadi hiyo, 16,085 wa kiume na 9,447 ni wa kike.

Mkurugenzi huyo amesema kwa mwaka huu 2018/19, Serikali imetenga jumla ya Sh427.5 bilioni ikiwamo hao wa mwaka wa kwanza.

Amesema hiyo aliyoitangaza ni awamu ya kwanza na awamu ya pili itatangazwa baada ya TCU kuwa imewadahili wanafunzi wengine na wale watakaokuwa wamekata rufaa.

Bodi hiyo imesema kuna wanafunzi wanaoendelea na masomo nao wataendelea kupata mikopo lakini kwa masharti ya vyuo vyao kuwasilisha matokeo ya mitihani huku ikieleza vyuo kumi havijawasilisha na kuvitaka kufanya hivyo haraka.

Chanzo: Mwananchi
Na warejeshaji wa mikopo
 
Majina hayo naona ni ya mwaka wa kwanza tu continous students VP yao yanatoka separate au
 
Hapa ndipo CHADEMA Inatofautiana na ccm. SERA ya Chadema ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wote waliodahiliwa kuingia vyuo vikuu tena bila ya ukaguzi.
 
Back
Top Bottom