mapesa yamejaa
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 1,404
- 3,420
Vijana wa sasa wamekuwa waoga sana wa kudai haki zao tofauti na kizazi kile cha wapigania uhuru kama kina Nyerere, Obote Kenyatta Kamuzu Banda, Mugabe nk.walitetea haki kwa nguvu zao zote waziwazi hadi wakawatoa wakoloni wakarudi makwao.
Cha ajabu hiki kizazi kilichozaliwa kuanzia miaka ya 70s hadi90s(nguvu kazi) ni kizazi cha waoga sana.hawajali hata wakinyimwa haki zao.Mfano tozo za simu tuliahidiwa ifanyike kwa mwaka mmoja lakini imekuwa endelevu na hakuna hata mmoja wa kuhoji
Mikataba ya kilaghai inaumiza wananchi.Mfano gesi ya mtwara tuliambiwa ingepunguza bei ya umeme nchini lakini imekuwa kinyume chake.Hivyo hivyo na huu mradi wa uchakataji na usindikaji wa gesi (LNG)na wenyewe tutapigwa tu.Mkataba wa kujadiliana na watu wawili hapo si ndo kupigwa kwenyewe.
Pamoja na hivyo, hamna hata mmoja amehoji.wasaidizi ni kusifu tu.uoga umezidi sana tofauti na wakina nyerere walipinga hadharani hii mikataba ya kilaghai pamoja na kodi za kihuni kama hizi. watawala waliojifanya wagumu cha moto walikiona.hawakuogopa cha policcm wa enzi hizo wala chombo chochote cha dola.
Kwa sasa huduma zote za umma ukianzia hospitali,shule nk.zote niza kusuasua.watawala wao hawaziboreshi kwa kuwa haziwahusu.Wao hutumia kodi zetu kwenda nje pamoja na watoto wao kupata huduma hata ambazo hazisitahili(malaria kwenda kutibiwa ulaya).yote haya yamesababishwa na aina ya jamii yetu kuwa ya waoga sana tofauti na jamii ya enzi za nyerere
Wewe mdau karibu tushauliane tufanye nini ili tuwe na watu jasiri na wazalendo kama wa enzi za wapigania uhuru?Maana kwa kizazi cha sasa ni cha kusifia tu hata pale pasiposifika.
Sent using Jamii Forums mobile app