Waoaji wapo ila hawana hela

Gulio Blog

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,056
Reaction score
4,124
Nashangaa kuona wanawaķe wengi siku hizi wanasema wanaume hatuoi tunachezea napingana na hii kauli wanaume waoaji wapo wengi tu wana mapenzi ya dhati kabisa kuwa na mwanamke mmoja.

Wana malengo na ndoto kubwa za mafanikio, wana ahadi zisizo kuwa na uwongo
pamoja na hayo mengi lakini bado kwa wanawake wengi wa sasa hawapendi sampo hizo za wanaume ambao hawana kitu au maisha ya kawaida.

Wengi wanapendi wakute mwanaume tayari ana gari na nyumba maisha kutolewa out kila siku shopping kila siku bila kujua huyo mwanaume unaehitaji kuwa nae ameangaika vipi mpaka kufikia hapo kama upo na mwanaume huyu hapa tegemea kuzalishwa na kuachwa hapo hakuna ndoa
 
Hamna muoaji asiyekuwa na hela bana.

Hata vitabu vya dini vimesema kuna condition ya kuoa ambayo ni kuwa na uwezo.

Unaweza amua kupiga deshi but mtoto wa watu atakula nini? Atavaa nini na atalala wapi?

Raha ya mke kutunzwa bwana. Asikuambie kitu. Umewekwa zako ndani, unakula, unakunywa, unavaa na mumeo kabisa anajipiga kifuani with that 'she's covered' look.
 
Raha ya mke kutunzwa, na huwezi oa huna chakuanzia kuishi na mke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…