Wao na sisi

ngalyas_t

Senior Member
Dec 5, 2012
172
57
Nilitafakari bila majibu, nikijaribu kutafakari utofauti wa yule mgonjwa, aliyeko kwenye hospitali ya kisasa na ile ya kijijini kule Makoja/Ngarenanyuki. Maana wote wakifa wanaelekea sehemu moja.

- Nikakumbuka kamsemo ka kimombo, "THIS IS RIDICULOUS",ikabidi niwafuate huko huko kuwauliza.
Waliponiona wakafurahi, wakasema
- Bora umekuja!!

= Mimi: Sijaja mniulize maswali, bali nimekuja ninyi mnipe majibu.
= Wao: Uliza tu...
= Mimi: Hivi hawa Wabunge wakimaliza muda wao, huwa wanaenda kuishi wapi?

Wakanitazama kwa mshangao, wakanijibu; hapa hapa nchini. Kwani kuna tatizo?
= Mimi: mi naona hivyo, kwa mifano michache nitakayo wapeni, natumai mtanipa majibu.
= Wao: Haina taabu maana sisi ni zaidi ya ENCYCLOPIDIA.

= Mimi: Ok, MFANO
# 1.
MATHAYO 27:22
Pilato akawauliza, “Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?” Wote wakasema, “Asulubiwe!”
**Walitumia wingi wao kumshinda Pilato, swali;je baada ya kumsulubu Yesu, miji yao ilipata maendeleo yoyote?**

#2.
DANIEL 6:4,6-8
"4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.
7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.
8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika."
**Kwa wingi wao na nguvu ya ushawishi walionao, wanapitisha maamuzi kumkomoa Daniel, SWALI; je mwadhirika wa maamuzi hayo ni Daniel peke yake?**

# 3.
MATENDO 7:54, 57-58
" Basi, waliposikia mambo hayo wakahisi wamechomwa mioyoni mwao na kuanza kumsagia meno yao. 57 Ndipo wakapaaza sauti ya juu na kuweka mikono yao juu ya masikio yao, wakamrukia wote pamoja. 58 Na baada ya kumtupa nje ya jiji, wakaanza kumtupia mawe. Na wale mashahidi wakaweka chini mavazi yao ya nje miguuni pa kijana aliyeitwa Sauli."
**Ni kwasababu ya wingi wao, na wao ndo wenye mamlaka; wakaona kumuua Stephano, ndo suluhu ya wao kuishi vyema. SWALI, Je maamuzi yao yameisadia JAMII wanayoishi?*

= Wao: Wakanikatiza, wakasema; "inatosha, kwani umewaza nini?"
= Mimi: Wakiwa kwenye viti(utawala), wanafanya maamuzi kana kwamba wataishi milele. WANAFANYA MAAMUZI KUMKOMOA MMOJA/WACHACHE, ILI WANEEMEKE SASA NA SIYO BAADAYE. Haya nipeni majibu.

= Wao: Mtazamo wako uko sahihi, sie hatuna majibu.
= Mimi: Duh! Kwahiyo safari yangu kwenu haikuwa na maana?, bora nikapumzike.
 
Wewe mzee aisee yaani umenilazimisha kusoma neno la Mungu bila kupenda, haya nashukuru
 
Wewe mzee aisee yaani umenilazimisha kusoma neno la Mungu bila kupenda, haya nashukuru
Hahaha . Bwana yule alisema "tutubu", lakini wao wakaona anawaambia wao tu. Kibaya wakaangalia walipo wakasahau kuwa kesho nao watakuwepo tulipo sisi.
 
Back
Top Bottom