Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Imekuwa kawaida ya serikali hii ya magamba kila wakati wa kutangaza bajeti eneo peke yake wanalolionea kulikamua ni kwa wanywaji bia na wavutaji wa sigara, nadhani ni vyema tukawaambia magamba kuwa tumeonewa kiasi cha kutosha.
Hii serikali badala ya kuchukua kodi kwenye migodi ambao wanatuibia kwa kutuachia shilingi 4 tu katika kila 100, sasa wao wametung'ang"ania wanywaji bia na wavuta sigara, ni vyema tukaiga mfano wa wanywaji wa Kibuku kitu ambacho waliwahi kukifanya mwanzoni mwa miaka ya 90, ambapo hatimaye serikali ilisalimu amri kwa kushusha bei ya kibuku!
Mkakati ni rahisi tu ni vyema zikatumika simu zetu za mkononi na kuwa-sms wale mnaowaona ni mashabiki wa bottle na kwa kuwa hata wabunge wengi wamekerwa sana na mtindo huu wa serikali yetu kujiendesha kwa pesa ya wanywaji wa bia na wavuta sigara tu naamini watapoona bia hazitoki watasalimu amri kwa kushusha bei ya vileo!!