Wanyonge wameungana na mabeberu wamewasikiliza

Mzee Mapenzi

Senior Member
Jan 9, 2019
122
439
Kwa mara ya kwanza nimeanza kuona Watanzania wamechoka na matamko yenye kuwaminya. Watanzania wamechoka kutumiwa kwa kudanganyiwa unyonge.

Unaweza kukubali ama kukataa, lakini nimeona na nimesikia, idadi kubwa ya Watanzania wanyonge wamefurahi nchi yao, kunyimwa mkopo na Bank ya Dunia.

Watanzania hawa hoja yao kubwa ni kubaguliwa kwa mtoto wa kike kupata elimu, huku mkopo ukilenga kuboresha elimu. Wengi wamehoji elimu ipi inayoboreshwa ikiwa mtoto anaepata mimba na kuzaa, anaishia kubaki mbumbumbu yeye na kizazi chake.

Wengine wametolea mfano wa mabinti waliobakwa ambao kupata mimba si kupenda kwao, wengine wanasema mtoto kupata mimba na kuendelea na masomo, kulipunguza vifo vya watoto wanaojaribu kutoa mimba, kwa nia ya kuendelea kusoma na kutokuonekana malaya, kama ilivyokuwa ikitafsiriwa.

Wapo pia waliosema wanadanganywa ili waendelee kuwa wajinga, ikiwa watoto wa vigogo wanasoma private school, baada ya kujifungua.

Kwa mitazamo hiyo michache, inaonesha sasa watanzania si wajinga tena. Wanajua jema na baya, wanajua wanahujumiwa na wimbo mzuri 'UNYONGE'.

Kuna mtu kaita jopo la watu anaowaamini ili kujadili hili jambo. Lakini binafsi nataka kumwambia hilo jopo halitamshauri, wala halitampa ukweli wa kwa nini mkopo umezuiliwa.

Lakini ukweli ni kwamba; mdomo wake unamponza na unawaponza wanyonge wake wote. Miaka yote tangu tuwe huru, hakuna serikali iliyosema inarudisha wanafunzi wajawazito shuleni bali, walikaa kimya na walioachiwa kuwafukuza ni walimu wa wanafunzi hao, pia mwanafunzi mwenyewe alijifukuza baada ya kupata mimba, kwa sababu alijua hawezi kusoma tena.

Kauli yake ya wazi imeleta yote haya, imewafunua wanyonge akili zao, nao wamejua Elimu ni haki ya kila mtu na, kibaya zaidi, wamejua mkopo wanalipa wao.

Hii si ishara nzuri kwa mtawala yeyote mwenye nia yake kwa wanyonge. Mmoja wa watawala ni Sabaya, nimeona wananchi wamemkataa palepale mkutanoni baada ya kuongea utumbo wake kwa kuwahusisha waganga wa kienyeji na mimba za utotoni.

Sinema ukiichoka huwa haiwezi kukuvutia, hata kama ikitangazwa kutazamwa bure.

Asilimia tisini wamefurahi kunyimwa mkopo. Asilimia tano ni MATAGA ambao wameishia kulaani vibaraka wa mabeberu kuwashawishi mabeberu kuwanyima mkopo.

Hawa wao wanakauli ya hatusomeshi wazazi. Wengine wanasema tumesalitiwa..

Kifupi hawajui wasimamie lipi kwenye hili kwa sababu, wanajua mkopo haungepelekwa mashuleni, bali kuwanufaisha wao.

Asilimia tano nyingine, hawa ni wale ambao wapo wapo, wao wanaamini kauli ya mtu mkubwa ni kauli ya mwisho na haipingwi, japo hata wao wanapenda watoto wao wasome. Wapo kishabiki tu na pengine hawajui kama mkopo ulikuwa ni kwa ajili ya elimu.

Nawakumbusha tu; Mabeberu hawaji kuwapanda mabinti zetu ili kuwapa mimba, tunawapa wenyewe kisha tunavimba kuwafukuza mashuleni.
 
Lakini ni vema tujiulize jambo moja.. Kama taifa na kwa umri wake bado ni sahihi kuliakulia na mambo ya mikopo na misaada wakati raslimali nyingine tunazotoa kwa mikataba kama ile ya chief Mangungo wa Msovero?

Jr
Jamaa hata haeleweki, kwenye majukwaa anajisifu pesa ipo, na tajiri huwa hakopi, bali analipa cash, huku anataka kuona kama mkopo ni haki yake tena!!! Mala tusiwategemee mabeberu!! Sasa ngoja WB, watoe taarifa kuwa mkopo hakuna tena, MATAGA, utawasikia watakavyobadirisha gear angani!!! Ooh wamesema tukubali ushoga!! Na sisi ni nchi huru bora wabaki nazo tu!!! Nchi hii ni rahisi sana kuiongoza!!
 
Nilichojifunza katika mada yako ni jinsi ambavyo umeonyesha kiwango chako cha ujinga!

Unaleta namba za asilimia kutoka kwenye akili yako ''kisoda'' bila kufanya utafiti halafu unatoa hitimisho la kijinga!

Kumbuka Ujinga sio sifa kama ilivyo upumbavu! Mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi!

Wewe unachohitaji ni elimu ili uelimike!
Na wewe anzisha uzi wako.. Usimuamulie cha kuandika.
 
Nilichojifunza katika mada yako ni jinsi ambavyo umeonyesha kiwango chako cha ujinga!

Unaleta namba za asilimia kutoka kwenye akili yako ''kisoda'' bila kufanya utafiti halafu unatoa hitimisho la kijinga!

Kumbuka Ujinga sio sifa kama ilivyo upumbavu! Mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi!

Wewe unachohitaji ni elimu ili uelimike!
Bahati mbaya sana umekuwa mjinga zaidi yangu.
Umeshindwa kutumia akili ndogo tu, kujua upo kwenye asilimia tano ya wale ambao wapo wapo, hawajui wasimamie wapi; kwa mabeberu ama kwa MATAGA.

Tuwape elimu bila kuwabagua.
 
Lakini ni vema tujiulize jambo moja.. Kama taifa na kwa umri wake bado ni sahihi kuliakulia na mambo ya mikopo na misaada wakati raslimali nyingine tunazotoa kwa mikataba kama ile ya chief Mangungo wa Msovero?

Jr
Kama taifa tuko hapa kwa sababu sisi ni wajanja kupitiliza na wale werevu hawatakiwi kwenye jopo la wanjanja waliopitiliza na ambao ndiyo wamekalia keki.

Tutabaki masikini daima.
 
Lakini ni vema tujiulize jambo moja.. Kama taifa na kwa umri wake bado ni sahihi kuliakulia na mambo ya mikopo na misaada wakati raslimali nyingine tunazotoa kwa mikataba kama ile ya chief Mangungo wa Msovero?

Jr
Mtu mwenye fedha utamfahamu kwa kuona namna anavyohusumia watu wake,hawa watawala wetu wanajimwambafy lakini hawana fedha.Kama zipo mbona wanalalamika kukosa mkopo?Hali yao ni mbaya ndiyo maana elimu bure inaanza kuwashinda,ajira hakuna,mishahara haiongezwi,huduma za afya bado ni duni,kazi kujenga na kununua midege no.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichojifunza katika mada yako ni jinsi ambavyo umeonyesha kiwango chako cha ujinga!

Unaleta namba za asilimia kutoka kwenye akili yako ''kisoda'' bila kufanya utafiti halafu unatoa hitimisho la kijinga!

Kumbuka Ujinga sio sifa kama ilivyo upumbavu! Mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi!

Wewe unachohitaji ni elimu ili uelimike!
Za kwako ziko wapi we vuvuzera?Ni kesho tu utabadili kauli yako ikiwa mwenyekiti atakubaliana na hoja nzuri ya mabeberu sababu wew ni vuvuzera unafuata mdundo wa tonge!So far ni nan mnufaika na masharti ya binadam hawa tunaowaita mabeberu kwenye hili suala la mabinti zetu?Nawaita wazungu binadam kwa sababu viongozi wa kiafrika ni self centred and humanless,mabinti wengi wanapata ujauzito aidha kwa kubakwa au kushawishiwa kutokana na hali duni ya kimaisha ya wazaz wao!Hivi mtoto wa Kabudi na Jpm atashawishiwa wapi na kwa lipi wakat anaatembea huku amekaa,nyumbani ulinzi mkali,anasoma shule za kisasa hvyo hawawez kuwa na uchungu na watoto wa uswahilini wanawaona ni viherehere vyao,hao ndio binadam wa kiafrika anapojitokeza mtu mwema kuwasaidia hawa watoto waliopata ujauzito kwa kubakwa wanashupaza shingo kwa sababu sio watoto wao,huu ni ubinafsi wa kishetani!
 
Sabaya hata polisi wamemchoka rejea ishu ya mataluma ili apige toka kwa wamiliki Wa mabasi in bashite style alivoumbuka.Mnaongozwa na vilaza mna hasara
 
Ni kweli kabisa bwana mkubwa anatakiwa ajitathmini kwa Nini watanzania wamefikia hatua waliyofikia Sasa ya kuandika barua kuomba nchi isipewe msaada, kikubwa wahusika wasitoe majibu mepesi just ya Jambo hili badala yake wanatakiwa wajihoji kwa Nini wameamua kufanya hivyo walivyofanya, lakini pia wajiulize Hawa watu wanaotoa taarifa hizi chanzo chake Nini. Kujimwambafai kwa kutoa majibu mepesi tu ya kwamba waliotoa taarifa hizo wapuuuzwe haitatusaidia Kama taifa
 
Jamaa hata haeleweki, kwenye majukwaa anajisifu pesa ipo, na tajiri huwa hakopi, bali analipa cash, huku anataka kuona kama mkopo ni haki yake tena!!! Mala tusiwategemee mabeberu!! Sasa ngoja WB, watoe taarifa kuwa mkopo hakuna tena, MATAGA, utawasikia watakavyobadirisha gear angani!!! Ooh wamesema tukubali ushoga!! Na sisi ni nchi huru bora wabaki nazo tu!!! Nchi hii ni rahisi sana kuiongoza!!

Kuna jambo rahisi sana .....tena la shule ya mtoto wa chuo mwaka wa kwanza kwenye social studies...mikopo na misaada ya nje iko attached na masharti so sisi waombaji ni juu yetu kuminywa humo, ni matarajio yangu kuwa wote wanaowaponda mabeberu wanajua hilo!
 
Ni kweli kabisa bwana mkubwa anatakiwa ajitathmini kwa Nini watanzania wamefikia hatua waliyofikia Sasa ya kuandika barua kuomba nchi isipewe msaada, kikubwa wahusika wasitoe majibu mepesi just ya Jambo hili badala yake wanatakiwa wajihoji kwa Nini wameamua kufanya hivyo walivyofanya, lakini pia wajiulize Hawa watu wanaotoa taarifa hizi chanzo chake Nini. Kujimwambafai kwa kutoa majibu mepesi tu ya kwamba waliotoa taarifa hizo wapuuuzwe haitatusaidia Kama taifa
Utakuja shangaa baada ya WB, labda kukataa kutoa mkopo huo, waliotufikisha hapo watakuja na majibu ya ki MIPASHO!!! badala ya kujiuliza hali hii imekuwaje kama taifa tukafika hapo.
 
Back
Top Bottom