Ukwaju
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 13,384
- 11,281
Wanyarwanda wapiganaji wa M23
31 Julai, 2013 - Saa 12:53 GMt
Raia wanne wa Rwanda wameambia BBC kwamba walilazimishwa na jeshi la nchi hiyo kujiunga na waasi wa M23 Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wanne hao wamesema walitoroka mapigano na kwamba wanajaribu kuomba hifadhi katika nchi jirani ya Uganda.
Mmoja wa Wanyarwanda hao wamesema asili mia 90 ya wapiganaji wa M23 ni wanajeshi wa Rwanda.
Mwenzake ambaye ni mwanafunzi wa utabibu amesema amewahudumia wapiganaji 300 waliojeruhiwa kwa risasi.
Serikali ya Rwanda imekanusha kuunga mkono waasi wa M23. Msemaji wa jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita amesema wanne hao wanatumia kisingizio cha kulazimishwa jeshini ili kupata hifadhi.
Wanyarwanda wapiganaji wa M23 - BBC Swahili - Habari
My Take kutokana na habari za BBC Swahili ni kweli hawa jamaa saa hizi hawatajificha tena ni wao wanaoisumbua DRC na wamo vitani kwahiyo Paul Kagame kumtishia Jakaya Kikwete janja yake kwisha, waondoke tu DRC kabla ya masaa 48 waliyopewa wasalimishe silaha