Wanyarwanda kupigana tena?

Wanyarwanda kupigana tena?

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,212
Wanyarwanda wengi wakimbilia Uganda


31 Julai, 2013 - Saa 13:44 GMT
121127133311_rwanda_mapatano_demokrasia_304x171_bbc_nocredit.jpg


Idadi kubwa ya raia wa Rwanda wameendelea kukimbia nchini mwao na kuomba hifadhi katika nchi jirani ya Uganda.
Licha ya juhudi za Rwanda kutaka raia wake walioko ugenini kurejeshwa nyumbani wakiwemo waliokimbia nchi mwaka wa 1958, kufuatia mapinduzi ya Ufalme, Wengi wa Wanyarwanda wangali na hofu ya usalama wao.

Waziri wa Uganda anayehusika na wakimbizi amesema wamepokea maombi 1800 kutoka kwa raia wa Rwanda. Afisa wa Shirika la Kimataifa linalowashughulikia wakimbizi-UNHCR, ameambia BBC kwamba wakimbizi hao waliingia Uganda mwezi Mei mkwaka huu.
Huenda idadi hii imeongezeka baada ya raia wengine kudaiwa kukimbia Rwanda katika siku za karibuni.Afisa wa serikali ya Uganda amesema raia wa Rwanda wameendelea kuomba hifadhi Uganda kwa madai ya kutishwa na serikali kutokana ma misimamo yao ya kisiasa, baadhi wanadai kuwepo na ukiukaji wa haki za binadamu.
Hata hivyo siyo wote walioitikiwa maombi yao.Miezi miwili iliyopita, wanafunzi 16 wa Rwanda walitorokea Uganda kwa madai ya kulazimishwa kujiunga na wapiganaji wa M23 wanaoendesha harakati zao Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Baadhi ya wakimbizi wamedai kutoroka makundi ya waasi baada ya kulazimishwa na serikali kujiunga nayo.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa, Marekani na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wamelaumu Rwanda kwa kuwafadhili waasi wa M23, lakini mamlaka ya Rwanda imekanusha madai hayo na kutaka ushahidi kutolewa kudhihirisha wanaunga mkono M23.
Takriban wakimbizi 20,000 wa Rwanda wanaishi nchini Uganda wengi kutoka jamii ya Wa-Hutu. wanadai kudhulumiwa na utawala wa sasa wenye Wa-Tutsi wengi.

SOURCE: BBC, Wanyarwanda wengi wakimbilia Uganda - BBC Swahili - Habari


My Take:

Ukiangalia kwa haraka haraka utabaini kuwa tayari wahutu na watusi wapo katika hali ya sintofahamu, huku wahutu wakiamini ya kwamba wenzao watutsi wanapendelewa, na wamepewa nafasi zaidi serikalini huku wao wakiwa bado kwenye hali mbaya. Na inaelekea jaribio lolote la wahutu kujaribu kuhoji juu ya hali ya mambo nchini Rwanda, inahatarisha maisha yao. Na kwa haraka haraka, ionaonyesha kwamba wanyarwanda wengi hasa wahutu hawaungi mkono mpango kagame wa kuishambulia Congo DR.

Je hii hali ya kuendesha nchi kwa hali ya upendeleo haitairudisha tena nchi kwenye machafuko? Ikumbukwe kuwa hata vita ya 1994, ilianzishwa kutokana na wahutu kutoridhishwa na mwenendo wa watusi katika masuala ya uongozi.

Lakini kama hali hii itaendelea hivi, huku Kagame akiendelea kumtunishia misuli Kikwete, na pengine kutaka kupigana na Tanzania, ni dhahiri hiyo itakuwa ni hatari kubwa sana kwake, maana kwa vyovyote vile wahutu watasimama upande wa Tanzania iwapo hiyo vita itapiganwa.

Nafikiri ni wakati mzuri kwa Kagame kung'atuka au kuirejea katiba na kuruhusu uchaguzi huru ili ikiwezekana, Rais mwingine mwenye vision tofauti na yake aiongoze Rwanda.
 
Kagame anaogopa kung'atuka kwa sababu ya maovu aliyoyafanya, ambapo kwa sasa anajaribu kujificha kwenye kivuri cha kuijenga Rwanda na kuleta maendeleo huku akiididimiza demokrasia na kukumbatia siasa za kibaguzi.
Ila akumbuke yatakayompata atateseka nayo yeye mwenyewe, wale anaowapendelea watakaa pembeni na kama wataamua kusaidia hawataweza.
 
Mkuu mimi naona cha muhimu ni kuwaombea sana kwa Mungu Wanyarwanda bila ya kujali makabila yao, tatizo lao kubwa hawajifunzi chochote kutokana na historia, wabishi kupindukia!! Duniani kote hakuna binadamu wanao kubali kutawaliwa na minority forever-hakuna, unaweza kutumia mabavu, vitisho lakini hiyo itasaidia kwa muda tu, kadiri muda unavyo sogea kuna siku kibao kitagehuka 4 worst. Rwanda ingetumia mbinu za Mzee Mandela za kumaliza tofauti zao kistaarabu mimi nisingekuwa na wasi wasi wa kufikili mauuaji mabaya zaidi yanaweleza kujirudia tena NCHINI RWANDA muda si mrefu. Hili kupunguza mambo ya jazba na kufikilia visasi nashauri Watutsi wa-tone down rhetoric ya kurudia rudia kila wakati kusema sema mauaji ya halahiki, wahache vile vile kila siku kulahumu mpaka vizazi vya Wahutu ambavyo vilikuwa havijazaliwa wakati wa mauuaji - kuna faida gani kuwafanya Wahutu ambao hawahusiki na mauaji wajione guilty na wanyonge masaa yote, alafu na nyinyi mnakwenda ku-commit mauaji kama hayo hayo kwenye makambi ya wakimbizi wa Kihutu huko DRC. Hebu tufafanulie sisi wana JF nyinyi Wanyarwanda jarani zangu hivi visasi vitawafikisha wapi? Suppose Wahutu walio ukimbizini wakipata mwanya wa kushika madaraka tena, unafikili kutatokea nini nchini RWANDA! Si mauuji ya 1994 yataonekana yalikuwa minor case kabisa, na safari hii Wahutu watahakikisha wanawaliza Watutsi KABISA(God forbid); I am sure Mh.Kagame ana such a scenario at back of his MIND - kama ni kweli, kwa nini hakubali kukaa chini na Wahutu wakamaliza tofauti zao kuliko kuwa dismiss Wahutu off hand just like that, akumbuke Wahutu hawataishi in Wildness 4ever.
 
Nadhani hata hao m23 wakitimuliwa Congo na kagame kishawakana return yao itakuwa kumng'oa yeye sasa,waungane tena na wahutu wakamuondoe mshenzi Yule,mimi sina.huruma na hawa viumbe hawana utu wala shukraan wacha wakauwane wao wao
 
malipo ni hapa hapa duniani, kama ni kweli Kagame yupo nyuma ya M23, naye kuna siku hatatawala nchi yake kwa raha.
 
Back
Top Bottom