Kosa la nchi kuendeshwa bila uadilifu na sheria kushika hatamu, nchi ina kanuni zake kwa nini hazifanyi kazi au zinapuuzwa mpaka watu kuuana. Tumeishi nchi nyingi ambazo kila dini ina machinjio yake, iweje leo kuwe na mashaka kama haya, sheria ziko wapi? hakuna haja ya kubabaishana na kutukana dini za watu, kila mmoja wetu ana jukumu la kuheshimu fauth ya mwengine hata akiamua kuabudu juwa, na ni jukumu la serikali kulinda heshima hio ya waumini bila ya kuwa biased. Mahakama na sheria dhaifu ndio chanzo cha yote haya, kusema kweli sifahamu hasa kwa nini tufike hapa na wengine ati wakishadidia humu mitandaoni kwa wananchi kupigana, shame on you.
Hivi tunashindwa na ustaarabu wa kujiuamulia wenyewe ni machinjo yepi ya faith gani? Uongozi unapolala pamoja sera kubwa za centralization na viongozi dhaifu wanaofocus kwenye matumbo yao ndio sababu za machafuko haya, pande zote mbili zinatakiwa kukaa chini na kujitathmini na sheria za nchi zinatakiwa zifanye kazi, hivi bunge, mahakama, wizara za sheria zina faida gani ikiwa tumefikia hadi hakuna hata urgency ya kutafutia ufumbuzi wa suala hili, si waislamu wala wakristo wenye haki kubwa ya mwenzake, na kama sheria imewaruhusu waislamu kuchinja pekee basi hio si sheria bali ni dhihaka kwa mfumo mzima wa sheria nchini, imefika hadi hii ya kutoaminiana basi kila mmoja aachiwe license ya kujichinjia kwa wanaowafata, na lizungumzwe kwa upana bila ya bias, matusi na mabishano yasiokuwa na maana.
Elimu inahitajika na sheria zinatakiwa zifanye kazi.