Wanyama Mikumi wanaisha, muda si mrefu itakuwa ni eneo la mashamba

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,069
711
Wakuu juzi nilipata bahati ya kuonana na mtu wa karibu na wafanyakazi wa mbuga ya wanyama ya Mikumi, alinitonya kuwa wawindaji wa tembo wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa mbuga/hifadhi.

Nilishangaa kusikia tembo wamebaki wachache mbugani, lkn wiki iliyopita mhifadhi mkuu alimfukuza kazi askari mmoja wa wanyama pori baada ya kukutwa akishirkiana na majangiri kuua tembo kadhaa mwezi uliopita.

Wafanyakazi wengine wawili walipewa onyo. Mfanyakazi huyo alilipwa stahiki zake zote na kurudi kwao huko mkoani Ruvuma.

SWALI: Je ni halali kumfukuza kazi tu wakati alikamatwa baada ya kubainika kushirikiana na majangiri kuua tembo? Si kwamba alitakiwa kufikishwa mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake? Au na mkuu anahusika katika ujangili?

Serikali ichukue hatua kumkamata ili aweze kutaja mtandao unaowinda wanyama mbugani.

Lakini pia kuna tetesi kuwa mwarabu mmoja pale Moro mjini anashirikiana kuwanda wanyama kwenye mbuga ya wanyama ya mikumi, nyama huuzwa kupitia brokers wake/vijana wake wa kazi ambao huzisambaza kwa wateja maalumu.

Hata wewe ukitaka order piga namba hii 0713 680 120 anaitwa Doto: utapata nyama yoyote kuanzia twiga, nyati, swala na nk. ukipiga jitamburishe kuwa wewe ni mteja kisha uliza kuna nyama gani leo?

Mkikubaliana yeye ataenda kuchukua kwa tajiri yake na kukuletea nyama popote ulipo Moro mjini. Kijana huyu nasikia siyo mwindaji ila na mtoto wa mjini anakua wateja wote.

Nawasilisha kumsaidia Rais JPM kutumbua jibu la MIKUMI.
 
Tafuta namna nzuri ya kufikisha taarifa kwa vyombo vinavyohusika, humu sidhani kama ni mahali sahihi
 
Si mikumi,nipo huku liwale kila siku twala nyati,twiga,faru,kitimoto pori toka hifadhi ya selous,hakka serikali imelala,huwa naumia sana na hali hii
 
Hakuna wanyama ile mbuga aisee na Break point ni muuzaji wa nyama pori maarufu sana
Una maana hizi za Dar? Sili pale tena ila mimi huwa nakwenda kwa ajili ya mchemsho wa samaki. Hiyo namba aloweka nadhani kama mhusika anasoma JF, basi kesha itupa kwenye dust bean. Sim card bure.
 
Una maana hizi za Dar? Sili pale tena ila mimi huwa nakwenda kwa ajili ya mchemsho wa samaki. Hiyo namba aloweka nadhani kama mhusika anasoma JF, basi kesha itupa kwenye dust bean. Sim card bure.
Kula tu kwakuwa ile ipo kwa kutaka mimi nakulaga sana ya pofu nyati na swala...!Tamuje
 
Mbuga ni kubwa sana,kudhibiti ni ishu sana
Na hapo mikumi ajali zinamaliza sana wanyama
 
Back
Top Bottom