Want to be intelligent? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Want to be intelligent?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Smoke, Mar 28, 2011.

 1. S

  Smoke Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanasaikolojia wameendelea kufanya uchunguzi kuhusu akili na IQ ya mtu. Wamegundua kwamba ili akili iwe faster kwenye kufikiri na kuamua, ni vema kufanya vifuatavyo;
  1. Wahi kulala na wahi kuamka. Hii inasaidia kupumzisha akili vema na imethibitika kua watu wanaolala muda mfupi wako kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya mental disorders ikiwemo stress na depression. Na unapoamka kunywa maji mengi yanayosaidia ubongo kufanya kazi vizuri. Na pia fanya mazoezi ili kufanya moyo usambaze damu ya kutosha sehemu zote za mwili ikiwepo kwenye ubongo.

  2. Chakula.
  Wataalam wanashauri ili mtu awe na akili ni vema akatumia zaidi matunda, nafaka ambazo hazijakobolewa hasa ngano na mbogamboga, nyama mtu ni vema zaidi akatumia kwa kiasi kidogo au asitumie kabisa. Vegeterians wameonesha kua na akili ya juu kwa sababu hawatumii nyama!

  3. Entertainment.
  Upande wa music na movies nao una yake. Katika saikolojia kuna mfumo unaitwa "Hypnosis" huu mfumo hutumiwa na kumfanya mtu arekodi vitu au taarifa bila kuzifikiria (records information without interpretation). Na hii hypnosis inakata au kuzuia kazi za upande wa mbele wa ubongo (cancels out the functions of frontal lobe of the brain) na hii sehemu ya mbele ya ubongo inafanya kazi ya kuamua na kufikiri. TV ni mojawapo ya hypnotic device, mtu anapoangalia movies au vitu vingine vinavyosisimua, sehemu ya mbele ya ubongo wake inakua haifanyi kazi na kwa hiyo vitu vyote anavyoviangalia anavirekodi bila kuvi interpret! Na hvyo akiendelea kwa muda mrefu ubongo unalala na anakua anashindwa kufanya inventions mbalimbali. Utafiti kuhusu hili ulifanyika ulaya katika chuo fulani ambapo watu walikwenda kusomea phd na wote walioshindwa kwa mara ya kwanza walipewa masharti kwamba warudi kwao halafu wakakae mwaka mzima bila kuangalia tv isipokua habari na vipindi vinavyosaidia masomo walokua wanasomea na wote waliofanya vile waliporudi chuoni walifaulu vizuri. Music pia rock type au mziki wenye mdundo mkubwa sio mzuri kwa afya ya akili ya mtu. Na kingine ni kwamba movie producers wa ulaya hawatumii muda wao kuangalia sana movies kwa sababu wanajua complications zake.

  4. Usipende kubishana au kuwa overexcited mara kwa mara! Kubishana na kukasirika kasirika, chuki, wivu kupita kiasi unachangia kupunguza kiwango cha mtu kufikiri sawasawa!
   
 2. m

  mja JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  good info
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  asante kwa taarifa mkuu
   
Loading...