Wanne wafa kwa kujinyonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanne wafa kwa kujinyonga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 29, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU wanne, akiwamo mwanafunzi wa shule ya sekondari, wamekufa kwa kujinyonga katika matukio tofauti wilayani Singida na Iramba kati ya Desemba 18 na Desemba 26 mwaka huu.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Celina Kaluba kwenye taarifa yake kwa waandishi wa habari mjini hapa jana alisema matukio yote hayo yamehusisha wanaume wawili na wanawake wawili.

  Alisema katika tukio la kwanza, Desemba 18 saa 12.30 jioni, Thimotheo Ilanda (31) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Wibia, Tarafa ya Mungaa Singida Vijijini alikutwa amejinyonga ndani ya nyumba yake kwa kutumia kamba ya katani.

  Katika ujumbe aliouacha, aliomba mtu yeyote asihojiwe kuhusiana na kifo chake.

  Naye Fatuma Abiudi (17), mwanafunzi wa kidato cha pili katika Sekondari ya Masinda na mkazi wa Kijiji cha Nkhambi, Tarafa ya Ihanja Singida Vijijini, alikatisha maisha yake kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa alifanya hivyo baada ya kutoa mimba.

  Tukio hilo lilitokea Desemba 21, saa 2.30 asubuhi.

  Wilayani Iramba, Kamanda Kaluba alisema siku moja kabla ya sikukuu ya Krismasi, Hussein Ramadhan (30) ambaye ni mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kibigili, alijinyonga kwa kutumia kipande cha shuka saa 10 jioni.

  Naye Agnes Agustino (39) mkulima na mkazi wa Kijiji cha Ntuntu, Tarafa ya Mungaa Singida Vijijini, alijitoa roho yake kwa kujinyonga kwa madai kuwa alikuwa na ugomvi na mumewe.

  Tukio hilo lilitokea Desemba 26, mwaka huu saa 2.30 asubuhi.
   
Loading...