Wangekuwa wapinzani...

Wangekuwa wapinzani...

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Kuhusu vurugu za jana za pale Ukumbi wa Mikutano wa Blue Pearl zilizomuathiri Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba na wenzake. Laiti waleta vurugu mle wangekuwa wapinzani...

Kwanza, wangekamatwa ndani ya dakika mbili.

Pili, wangeondoshwa Ukumbini chini ya ulinzi mkali kupata kuonekana nchini Tanzania

Tatu, wangepelekwa leo hii Mahakamani chini ya ulinzi mkali mno

Nne, wangesomewa mashtaka mazito yasiyo hata na dhamana (kama ugaidi)

Tano, vyama vyao visingebaki salama.NAWAZA MAMBO KWA KINA TU"!

LAKINI, akina Paul Makonda ndiyo kwanza wanaitisha Press Conference 'kupambanua' kilichotokea. Nchi hii!? Tuendelee....
 
Hivi makonda hajakamatwa tu jamani mpaka salsa? Angekuwa mwanachama Wa Chadema ndo anatuhumiwa hivo angekuwa mtaani kweli?
 
mambo haya huamsha hasira ambayo haitapozwa kwa damu ya kuku.......
 
mambo haya huamsha hasira ambayo haitapozwa kwa damu ya kuku.......

Pole sana mkuu kwa kukaribia kuamkwa na hasira ambayo unaamini haitapozwa kwa dam ya kuku. ila kwa watanzania ninao wafaham mimi hasira yao hua inaishia kwenye vijiwe vya magazeti, kahawa, kwenye madaladala na haziwafikii wahusika wanaotakiwa kupata taarifa za hasira hizo. ama zikiwafikia zinakua hazina ushawishi maana wenye hasira wameshindwa kusimamia hasira yao hiyo.

Ifike hatua tuseme imetosha na kuchukua hatua tunazoamini ni sahihi kwa sasa na vizazi vijavyo. japo tumekua wapole sana tangu tunapata uhuru, ila naamini bado hakijaharibika kitu sisi tuliopo leo tuna nafasi.

TUCHUKUE HATUA ZINAZOFAA SASA NA SIO KULALAMA TU KWAMBA TUTAFANYA TUTAFANYA NA SIKU ZINAENDA WATU WANAZIDI KUUMIA.
 
Ipo siku tu yaja,aliyosema mleta mada ni sahihi kabisa.
 
Mbona hata hizo fujo za jana mmefanya nyie na lile kundi lenu la tindikali la pale bavicha unadhani hatujui halafu mnamsingizia makondo mmepwelewa nyie.
 
Hakuna bhana! msikubali kabisa hadi akamatwe.., nendeni mkalale uchi barabarani..!
Tena wakalale kwenye barabara ya tareni ya tazara ndiyo nzuri iko imara zaidi au wakalale kwenye njia ya kivuko cha kwenda kigamboni.
 
kova.jpg


Kova angeshaita waandishi wa habari na kuwaeleza maelekezo kutoka Lumumba, Na hatua za jeshi la polisi kuwapeleka watuhumiwa mahakamani kesho.
 
Siku ya mwisho yaja yaja yatisha. Siku ya mwisho ikifika watuvwengi watalia sana na wengine wengi watafurahi!!!!!!!?
 
Sijasikia intelijensia ikitoa tamko kuhusu tukio la kunyanyashwa waziri mkuu mstaafu warioba,au intelijensia ni kwa ajili ya cdm tu??? kazi ya green gurd ndio imeanza rasmi kuelekea 2015
 
Hiwezi kushondana na aloshika mpini na we umeshika makali ,mtawala.anamamlaka tu .
 
Back
Top Bottom