Wangapi wameshakutana na changamoto katika kukopesha marafiki?

Wangapi wameshakutana na changamoto katika kukopesha marafiki?

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
4,131
Reaction score
6,125
Mimi binafsi ni mhanga mara kadhaa kutokana nakuwa na huruma sana na kuamini rafiki kirahisi.
Mwisho wa siku inakula kwangu.
FB_IMG_1548858914484.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah deni baya
Kuna jamaa nilimkopesha hela sasa akawa ananipiga chenga.
Kuna day nilikutana nae anavuka barabara yupo kati kati hapo sasa hajui avuke au urudi na gari zinakuja nilimuonea huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haha nimecheka kama mazuri.
Yani siku hizi ukimkopesha rafiki, jua kuna possibility kubwa 2
1. Kupoteza pesa
2. Kupoteza urafiki

Btw nawasubiri mwenzangu na mimi tunaokopa afu hatutaki kulipa
 
kuna msela wangu alinikopesha 70,000 eti nimlipe 80,000 baada ya wiki. nilichokifanya nilimpa 20,000 tu hadi kesho atanidai Na muda wa kulipa sina.



nami namdai bro laki 9 na hawazi hata kunilipa.
 
Principle ya kukopesha usimpe mtu kiasi halisi anachokitaka i.e akitaka 100,000 mwambie una 30,000 kwenye simu kama itasaidia umpe au kama akitaka 30,000 mwambie una 10,000 kama anataka umpe hio hio..huyo mtu hatorudi tena kukuomba hela au ukiona vipi unasema sina hela hata kama unazo..lia na wewe hali ngumu huna hela
 
humu wote tuna uwezo kifedha tunakopeshaga tu ila hatulipwi..

ngoja mimi niwe upande wa pili wa tunaokopa lakini hatulipi ili ku balance hoja...

kwa ufupi kulipa deni ni kipaji ambacho wachache sana wanacho
 
Principle ya kukopesha usimpe mtu kiasi halisi anachokitaka i.e akitaka 100,000 mwambie una 30,000 kwenye simu kama itasaidia umpe au kama akitaka 30,000 mwambie una 10,000 kama anataka umpe hio hio..huyo mtu hatorudi tena kukuomba hela au ukiona vipi unasema sina hela hata kama unazo..lia na wewe hali ngumu huna hela
Haswa mademu wa kibongo ndo zao akikopeshwa anajifanya kasahau anabaki kujichekeshachekesha tu,dawa ni kusema huna pesa.
 
Zamani kumkopesha Rafiki pesa kulijenga ukaribu
na kuwafanya muishi kama ndugu
Wakati huu sasa imekuwa ndivyo sivyo unapo
chukua maamzi magumu ya kumkopesha Rafiki
pesa ukubaliane kupoteza kitu kimoja ama vyote
viwili...
Unaweza kumpoteza Rafiki ukapata pesa kwa
taabu sana au ukapoteza pesa narafiki
Rafiki mwema nimzazi wako pekee usiwaamini
marafiki malanyingi marafiki kugeuka kuwa
maadui ni raisi mno kuliko adui kuwa rafiki
 
Mimi kukopesha sasahivi labda awe ndugu wa tumbo moja ambaye hata akinizika ntafarijika niliweza kuwa wa msaada kwake.

Ila hawa wanaitwa marafiki sijui na mabinamu washanipa somo gumu la kuua utafiki na undugu sababu ya mikopo.
 
Write your reply...
Pia kumkopesha ndugu napo ni kipaji yaani undugu unaeza kufa
Bro angu nilmkopesha nguo za thaman ya tsh 85000 nilipewa buku tano tu nyingne sjalipwa mpk saiv na uwezo wa kumwomba sina
 
Rafiki mzuri kabla hamjakopana pale mtadumu sana.lakini moja wapo ukimkopa mwezako bac ujuwe kurudisha ndeni ni utata mtupu.Mimi kwenye tuliuwa rafiki kwasababu ya pesa.pesa sabuni ya roho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha nimecheka kama mazuri.
Yani siku hizi ukimkopesha rafiki, jua kuna possibility kubwa 2
1. Kupoteza pesa
2. Kupoteza urafiki

Btw nawasubiri mwenzangu na mimi tunaokopa afu hatutaki kulipa
Mie nilishaacha kabisa kukopesha marafiki, kama sina ya kukupa jumla, basi ya kukopa ndo haipo kabisaa. Siwezi tena kuendelea kukosa marafiki kisa deni, nilio nao nawapenda sana, siwezi kuhimili.kuwakosa, teh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom