Wangapi mnafanya/mmewahi kufanya maombi na wapenzi wenu?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,943
Reaction score
61,071
Kila mtu kwa imani yake anatambua umuhimu wa sala kwa Mwenyezi Mungu. Hata Katika mahusiano wanandoa wanapaswa kujifunza kufanya maombi kwa pamoja kwani inasaidia sana. Jambo hili nimelijua kwenye semina fulani.

Kufanya maombi pamoja kuna ongeza upendo baina ya wawili..kwa upande wa WAPENZI wakristo mnaweza mkaamua kujifungia chumbani na kufanya maombi hata kwa kimya kimya.nimejaribu hili nimegundua linanipa amani MOYONI mimi na mpenzi wangu tumekuwa tunaaminiana sana.

Nafurahi kama wapo watu mnafanya maombi pamoja.. Kama ambavo vijana wanapewa RAI ya kusali kipindi cha kutafuta mchumba basi hata ukipata mchumba endelea kumfundisha namna ya kusali pamoja. Japo ni suala binafsi ila sio mbaya mwenye uzoefu wa kufanya maombi na mwenza wake atueleze ni namna gani yeye imemsaidia kwenye mustakabali wa mahusiano yake.
 
mi napiga maombi hadi na dear michepukos
Hahaha nilijua tu kama bujibuji angeonekana kwenye thread hii angechangia hivyo.. Nafanya maombi ya kufunga roho ya uzinz ikutoke. Kwanini wanaume wenzangu mnakuwa na mchepuko mbona mimi nimeshindwaga nimeamua kuwa mwaminifu
 
Mi huwa nafanya ivo na wangu mda mfup kabla hatujalala.Ni kitu kinachoongeza imana san na upendo pia
 
Hahaha nilijua tu kama bujibuji angeonekana kwenye thread hii angechangia hivyo.. Nafanya maombi ya kufunga roho ya uzinz ikutoke. Kwanini wanaume wenzangu mnakuwa na mchepuko mbona mimi nimeshindwaga nimeamua kuwa mwaminifu
Mwaminifu kwa mizimu na Roho za kifamilia???
 
Hua tunaomba pamoja kabla ya kulala na maombi yamenisaidia Sana kwenye ndoa yangu..hata hapa tulipofika Ni kwa msaada WA mungu
 
Tena huwa tunapeana na zamu kabisa kabla ya kulala... Sasa iwe zamu yako halafu ujitoe ufahamu.... Hakulali mpaka sala ipigwe
 
Back
Top Bottom