Wanawake wote mnaojielewa mbarikiwe sana

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari ndugu zangu,

Wanawake wote mnaojielewa popote mlipo haijalishi mnatupasua kichwa sana, ila mbarikiwe sana. Uwepo wenu ni mkubwa sana na nyie ni viumbe wa muhimu sana katika kuipamba dunia na kutupa sisi wanaume burudani.

Haijalishi mnatukwaza sana kila tunapotoka asubuhi au kurudi nyumbani ila mbarikiwe sana.

Haijalishi mnatufanya tushinde bar kukwepa kelele mpaka usiku sana ila mbarikiwe sana.

Haijalishi mnatudharau pindi tunapo watongoza wakati mwingine, ila mbarikiwe sana. Kuna muda mkitudharau na kutukataa mnatujengea ujasiri sana sisi wanaume.

Haijalishi mnawalisha watoto wetu sumu, kwamba sisi baba zao hatutunzi familia ilihali tunahangaika sana ila popote mlipo mbarikiwe.

Maisha bila mwanamke ni ubatili mtupu, kijana tafuta mwanamke anaye jielewa weka ndani thamani yako itaongezeka.

Wanawake wote mnaojielewa hivi vituko mnavyo tufanyia tunajua wazi kuwa ni hulka zenu za kike na tuliambiwa tuishi na ninyi kwa akili. Pia tunajua mnafahamu wazi kuwa hakuna usawa baina ya mwanamke na mwanaume, ila sisi wenye akili tunajua mnatumia kigezo cha usawa kutupima akili zetu na misimamo yetu kama wanaume.

Wanawake jueni kwamba ukiona mwanaume anachukia mwanamke jua hana akili kabisa.

Endeleeni kubarikiwa popote mlipo.

NB: Baraka hazi wahusu wanawake wasiojitambua, wanawake wanaojiuza, wanawake waliotoboa masikio /pua zaidi ya mara mbili, wanawake waliotoboa kitovu, na wote wale waliochora tatoo na kuvaa vikuku miguuni kwa namna yeyote ile.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hivi wanawake wanaojielewa ndio wapoje kwani?
Kwa mtazamo wangu mwanamke anayejielewa Ana sifa zifuatazo
👇👇👇
1.Hajiendekezi hovyo hovyo kwenye mitandao kwa kupost vipicha kila Mara na kuandika maneno ya kiduanzi

2.Angalau anajua kutafuta hela Yake mwenyewe e.g kufanya biashara, kushiriki vicoba na upatu.

3.Hapigi mizinga ya hovyo hovyo.Asilimia kubwa ya mahitaji yake anayasimamia mwenyewe.Mfano hela ya saloon,nguo,usafiri,vocha ya Simu.

4.Anadate na mwanaume mmoja anayejielewa na kumsupport pale anapokuwa na uhitaji.

5.Ni Ana hofu na Mungu,anawaheshimu wazazi wake na wakubwa zake.

6.Asiye mnafiki,mpiga majungu na mfitini.
 
Umeandika upuuzi.

Mwanamke anayejitambua atakufanya vipi ushinde bar?Yaani usitamani kurudi nyumbani?

Mwanamke anayejitambua atawalisha vipi watoto sumu kuhusu baba yao anayehangaika kutunza familia?

Au kwako mwanamke akiwa hana tattoo na tundu zaidi ya moja sikioni ndio anayejitambua?

Kwa taarifa yako,unaweza ukaokota malaya uliyemkuta kabisa barabarani akijuza ukamuoa na akawa mwanamke bora na anayejitambua kuliko hao walokole unaonena nao kwa lugha kanisani.

Asanteni.🎤
 
Back
Top Bottom