Wanawake wenzangu, je ulivyo ndivyo upendavyo?

nyakoo

JF-Expert Member
Dec 4, 2014
255
322
Habari za jioni wana JamiiForums.

Leo nawiwa kuongea na wanawake wenzangu juu ya hili suala la vitambi vyetu na vya waume zetu. Nilikuwa nimekaa napiga story na mume wangu mara akanikumbusha kipindi cha nyuma kitambi kilivyokuwa kinamnyemelea kwa kasi na akawa ananitania kuwa mimi ndio nilikuwa chanzo, na nikatafakari nikaona kuna kaukweli.

Baada ya kupata mtoto wetu wa kwanza nilinenepa nikawa na mtumbo huo, inshort nilichukiza maana wakati wa ujauzito nilikuwa nafukia sio kula.
Nikawa niko insecure na mwili wangu hata kuvua mbele ya mume wangu nilikuwa naona aibu, mume wangu aliligundua hilo ikawa kama ananipa moyo ila haikusaidia, bado niliona kuna kitu hakipo sawa. Na yeye pia alianza kunenepa na kitambi kikawa kinakuja kwa kasi, nikawa naona kabisa mission itakuwa impossible soon.

Siku moja i come across jarida moja linalohusu masuala ya diet na lifestyle, nikakutana na mada isemayo "WE ARE WHAT WE EAT"
Sio siri nilivutiwa na makala ile, then nikaamua kuchuka hatua.
Niliamua kuanza mazoezi na diet maalumu kwaajili ya kupunguza uzito, ila kabla ya kuanza nilimuomba mume wangu anisaidie katika safari hiyo maana umoja ni nguvu(nia ilikuwa nae apunguze kitambi na mwili)

Mwanzo alikuwa mzito ila nilimkazania hadi tukaanza, nikabadili kabisa mlo wetu na kukazana na mazoezi na taratibu akaanzaa kupunguza kunywa bia mwisho akaacha kabisa(now anakunywa wine mara chache chache sana). Alipoona mafanikio alipata moyo na akajiunga gym ili kutengeneza mwili, na sio siri kwa sasa yaani acha tu!!

Nami nilipunguza mwili na tumbo likaisha kabisa nikarudia ule mwili wangu wa awali niliokuwa naupenda, kwakweli kujiamini kukarudi na nikawa na furaha zaidi. Wakati wa ujauzito wangu wa pili ilibidi niwe na nidhamu ya ulaji na kuzingatia mazoezi (mume wangu alikuwa msaada mkubwa) hivyo ilinisaidia sikugain weight sana na nilipojifungua kazi iliendelea, na nikagundua kwamba, kuwa tukunyema ni kujitakia na kujiendekeza cha msingi ni kuchukua maamuzi tu na inawezekana.

Jitafakari, kisha chukua hatua, inawezekana na wa kuliwezesha ni wewe, kwani pia inakuepusha na maradhi mbali mbali yasababishwayo na ulaji mbovu na kutofanya maoezi.
 
Mazoez na diet yanahitaji kujitoa haswa aisee hamna kinachokuja kirahisi
Wengi tunashindwa kwa ajili ya uroho wa chakula
All in all asante kwa kushare me najitahdi kwa kadri ya uwezo wangu naogopa sana kitambiii
Ni kweli mama, inahitaji kujitoa sana na nia ya dhati. Usikate tamaa inawezekana.
 
Asante kwa kutukumbusha mpendwa,jmn wanawake tujitahidi tusiwe na vitambia.
Mim nakichukia kwa moyo wangu wote na sikiruhusu
 
M napenda mke wangu awe hivo ambavo we hupendi namaanisha anenepe lakini wapi tatizo nn jamani!!
Maybe ndio mwili wake ulivyo, nina rafiki yangu huyo yeye hajui cha mazoezi wala diet na ana watoto wa4 ila ukimuona utadhani hana mtoto.
 
Karibu sana bi dada. Nafurahi kusoma uzi kama hizi za kuonyesha watu waliomo kwenye ndoa na wanaishi kwa maelewano hata kwenye afya zao wanashirikiana kwa faida zao binafsi na familia husika. Ni nadra sana kukuta habari kama hizi hapa JF, ni kuponda tu mahusiano na ndoa wanaume hivi wanaume vile, wanawake hivi wanawake vile lakini kuna Watanzania chungu nzima wanafurahia mahusiano yao ndoa zao pamoja na majaribuni chungu nzima yaliyokuwepo.

Asante mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom