Wanawake wengine sijui mkoje?

Wanawake wengine sijui mkoje?

Dear Mama wa kambo,
Tokea uje kwetu maisha yetu yamekuwa mabaya kwa maana umekuwa unatunyanyasa unatufanyia visa juzi mdogo wangu umempiga na ufagio mpaka akazimia alipozinduka kwa juhudi zetu .
Ulimnyima chakula ukamwamrisha asilale kitandani alale chini ya sakafu tena bila huruma .

Tunaumri wa kupendwa sio wakupigwa na kunyanyaswa.
Umekuwa ukitupiga kutuchoma na moto kupitia vitu vikali ,umekuwa unatulaliza njaa ,umekuwa unatutumikisha tena kazi nyingi unatupa ambazo hatuwezi sisi kuzifanya.

Tunapika,tunafua,tunadeki,tunaosha vyombo watoto wako uliokuja nao wanaumri wa mkubwa kushinda sisi.

Maisha yetu hatuna muda nayo tokea tuje niwewe tu ndio unatutesa tu.

Mama wakamboo tumekufanyia nini hadi ututesee hivi?Shuleni hatuendi wala nini kazi zimekuwa ni hizo tu kwanini lakini? Halafu wako wanaenda shule wanaishi kwa amani .

MAMA TUMEKUFANYIA NINI.
😪😭😭😭😭 HUU UJUMBE NIMEKUTA KWA MTU FULANI JE HUYU MAMA ANAFANYA SAWA?
Inasikitisha sana! Kuna rafiki yangu mmoja ambaye kwa sasa ananafasi nzuri serikalini. Yeye na wadogo zake wawili wa kike walipata mateso mengi mara baada ya kifo cha Mama yao Mzazi. Mama alipofariki alimuacha huyu rafiki yangu aliwa na umeri wa miaka kumi na moja na akisoma darasa la sita katika shule moja ya binafsi na wadogo zake wakiwa na umri wa miaka tisa na saba nao wakisoma katika shule hiyo hiyo.

Baba Mzazi wa rafiki yangu alikuwa Mhasibu katika shirika moja la serikali na Mama mzazi wa rafiki yangu yeye alikuwa ni Muuguzi katika hospitali ya serikali na alikuwa na biashara zilizomuingizia kipato. Baba huyu alikuwa ni mtu wa tungi nyingi na totoz hivyo hakuwa mtu aliyeijali sana familia yake kwani karibu majukumu yote yalifanywa na mkewe. Siku ya siku Mama aliugua ghafla kichwa na kupelekea umauti wake baada ya muda mfupi!

Maisha yalibadilika ghafla kwa hawa viumbe watatu wadogo. Baba alisitisha pombe kwa muda ili kuwalea watoto wake lakini alishindwa. Aliamua kumleta nyumbani kimada wake ili asaidie kulea watoto wake na apo ndipo mateso yalipoanza. Watoto walinyimwa chakula, chomwa kwa moto, pigwa sana.........Baba alimsikiliza kimada wake na ukichanganyanya na pombe hakujali. Baada ya muda Baba alipoteza kazi tokana na ulevi uliokithiri.

Ilikuwa ni bahati kabla ya kifo chake alikuwa keshalipa ada ya mwaka mzima kwa watoto wake vinginevyo walikuwa wafukuzwe shule. Miradi iliyoachwa na Mama yao ilifilisiwa na kimada wa baba yao! Rafiki yangu kwa ushauri wa ndugu upande wa Mama alipeleka malalamiko Ustawi wa Jamii hivyo ikaamriwa mafao ya mama yao yawe chini yausimamizi wake akisaidiwa na ndugu wa Mama. Aliondoka nyumbani yeye na ndugu zake wakaenda kukaa kwa Mama yao mdogo ambaye hakuwa na uwezo. Pamoja na umri mdogo, alikuwa na akili iliyopevuka hivyo aliweza kuwasaidia ndugu zake. waliendelea na shule vizuri na matokeo yao yalikuwa yakupendeza sana. Baada ya darasa la saba aliamua kuendelea na shule ya serikali vivyo hivyo kwa wadogo zake. Akiwa sekondari alianza kujihusisha na biashara ya ufugaji wa kuku na nguruwe akimshirikisha Mama yake Mdogo. Biashara iliyomlipa vizuri sana. Pesa nyingine kutoka katika mafao ya Mama yao waliiweka katika akiba maaalum benki (Fixed Deposit).

Leo hii wote maisha yao ni mazuri mno, dada zake wana kazi/professions nzuri! Baba anawaomba msamaha kwani kwa sasa hali yake ni mbaya sana ananyanyaswa na kimada wake! Hakika malipo ni hapa hapa duniani!
 
Kwa nn mama wa kambo anakuwa na roho mbaya hivi tofauti na baba wa kambo

Wanaume tunajua ya kuzingatia,, so stress za kulea tu huwa zinatosha kutupa hasira watoto wasilale njaa.. Muda wa chuki tunakosa
 
Sisi hiyo haitatokea tena


Maana kila mtu anajitegemea na mume wao wa kuwatia jeuri kashafariki wamebaki kina mama tu, cha ajabu sasa watoto tunapendana kiajabu sana wa mama yule unakuta anapendana sana na wa mama huyu na ndio msiri wake yaani imetokea tu

Mimi imetokea napendwa zaidi na mamkubwa kiasi wengine wote wameshajua
Ukiona Wakewenza wanapendana sana na Mume wao alisha fariki, ujuwe kuna uwezokano walishirikiana pamoja kumtanguliza Mume wao kwa Sir God!!
 
Ninavyowapenda wanagu ,,nikifikilia kumtimua mama yao kwa jeuri na upuuzi wa kila aina, nikikumbuka watakavyoishi na mama wa kambo dah!! Naamua kumpotezea tu huyu jinga mzazi mwenzangu
 
Back
Top Bottom