Wanawake wengine sijui mkoje?

katoto kazuri

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
6,083
5,659
Dear Mama wa kambo,

Tokea uje kwetu maisha yetu yamekuwa mabaya kwa maana umekuwa unatunyanyasa unatufanyia visa juzi mdogo wangu umempiga na ufagio mpaka akazimia alipozinduka kwa juhudi zetu. Ulimnyima chakula ukamwamrisha asilale kitandani alale chini ya sakafu tena bila huruma .

Tunaumri wa kupendwa sio wakupigwa na kunyanyaswa. Umekuwa ukitupiga kutuchoma na moto kupitia vitu vikali ,umekuwa unatulaliza njaa ,umekuwa unatutumikisha tena kazi nyingi unatupa ambazo hatuwezi sisi kuzifanya.

Tunapika, tunafua, tunadeki,tunaosha vyombo watoto wako uliokuja nao wanaumri wa mkubwa kushinda sisi.

Maisha yetu hatuna muda nayo tokea tuje niwewe tu ndio unatutesa tu.

Mama wakamboo tumekufanyia nini hadi ututesee hivi?Shuleni hatuendi wala nini kazi zimekuwa ni hizo tu kwanini lakini? Halafu wako wanaenda shule wanaishi kwa amani .

MAMA TUMEKUFANYIA NINI.
😪😭😭😭😭 HUU UJUMBE NIMEKUTA KWA MTU FULANI JE HUYU MAMA ANAFANYA SAWA?
 
Wamama asilimia kubwa(sio wote) kuishi vizuri na watoto wa mwenzie wanaona kama ni najisi.
Mi naona kama ni "nature" iko hivyo sababu hata ukichukua kifaranga ukampeleka kwa kuku ambaye sio mama yake atauwawa tu iko hivi pia hata kwa wanyama wengine wengi.

Ni wazo langu tu!!!
 
Wito wangu, wanaume kama watoto wadogo, na ikatokea umetengana na mama yao kwa sababu yoyote ile ya msingi, usioe tena...Lea wanao...wakaishakuwa na kuanza kujitegemea hapo unaweza kuoa katoto kazuri ka kukuchangamsha wewe na mafao yako uzeeni...

I tried to think without my lawyer..
 
Lawyer niko hapa, subiri nikuje kwa mind yako tuendelee kuthink 💃
 
Wamama asilimia kubwa(sio wote) kuishi vizuri na watoto wa mwenzie wanaona kama ni najisi.
Mi naona kama ni "nature" iko hivyo sababu hata ukichukua kifaranga ukampeleka kwa kuku ambaye sio mama yake atauwawa tu iko hivi pia hata kwa wanyama wengine wengi.

Ni wazo langu tu!!!
Nikweli miaka 3 nanusu unampa aoshe vyombo eti akisema siwezi unamchapa mpaka azimie kweli ??
Kweli wewe sio binadamu kwa maana hadi shetani anashangaa na wengine wapo humu eti.
 
Mripoti kwenye vyombo husika uwe na ushahidi pole sana
Hiyo barua ipo na mimi na huyu mama ni rafiki wajirani yangu before sijajua ni evil until aliponipa ile barua wee halafu anaona hao watoto ndio wamekosea sio yeye halafu wanaume ni wabaya kweli hawaangalii maendeleo ya watoto wao .
Kuweni makini MAMA WA KAMBO NI WAKAMBO TU
 
Wito wangu, wanaume kama watoto wadogo, na ikatokea umetengana na mama yao kwa sababu yoyote ile ya msingi, usioe tena...Lea wanao...wakaishakuwa na kuanza kujitegemea hapo unaweza kuoa katoto kazuri ka kukuchangamsha wewe na mafao yako uzeeni...

I tried to think without my lawyer..
Mpe watoto bibi kama mama yao kawakataa.🙄🙄🙄 ni nafuu zaidi.
 
Binadamu wote tuna kaupungufu fulani, ambako ukishindwa kuka control utafanya mambo kama uyo mama wa kambo.
Roho mbaya haijalishi ni mama wa kambo au mzazi, Mimi ni shahidi...nimelelewa na mama wa kambo (though sipendi hata kumuita wa kambo..i prefer "mama")...amenilea tangu nikiwa na miaka 5 na mdogo angu akiwa na mwaka na nusu...upendo wake kwangu hauelezeki.

Mimi pia ni shahidi...nilikua na rafiki angu Mama yake mzazi alikua anamfanyia vitu ukikakaa vibaya waeza sema hajamzaa...mi nadhani binadamu ni either uwe good hearted or ill hearted no matter ni mama wa kambo,baba wa kambo au vyovyote vile.
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Hiyo barua ipo na mimi na huyu mama ni rafiki wajirani yangu before sijajua ni evil until aliponipa ile barua wee halafu anaona hao watoto ndio wamekosea sio yeye halafu wanaume ni wabaya kweli hawaangalii maendeleo ya watoto wao .
Kuweni makini MAMA WA KAMBO NI WAKAMBO TU
Usitutishe
 
Inategemea......

Mama yangu wa kambo ananipenda sana na nipo huru nae kuliko mama yangu mzazi, na mama yangu wa kambo ni mke mkubwa kiasi ndio angekuwa na chuki mno.

Tena umenikumbusha wacha nimpigie tutaniane saizi.
 
Wamama asilimia kubwa(sio wote) kuishi vizuri na watoto wa mwenzie wanaona kama ni najisi.
Mi naona kama ni "nature" iko hivyo sababu hata ukichukua kifaranga ukampeleka kwa kuku ambaye sio mama yake atauwawa tu iko hivi pia hata kwa wanyama wengine wengi.

Ni wazo langu tu!!!
Binadamu c kuku japo ni mnyama alie pewa utashi kuzid wanyama wote
 
Inategemea......

Mama yangu wa kambo ananipenda sana na nipo huru nae kuliko mama yangu mzazi, na mama yangu wa kambo ni mke mkubwa kiasi ndio angekuwa na chuki mno.

Tena umenikumbusha wacha nimpigie tutaniane saizi.
Unabahati sn mkuu ht mm ilikua km ww ila alivokuja kukengeuka kw ibilisi maana alivomaliza kwangu kageuka kwa wanae wa kuwazaa yan kavuruga familia nzima,cjui nan anamtia kichwa?au kwavile mwl.mkuu mamaake!
 
Sisi hiyo haitatokea tena

Maana kila mtu anajitegemea na mume wao wa kuwatia jeuri kashafariki wamebaki kina mama tu, cha ajabu sasa watoto tunapendana kiajabu sana wa mama yule unakuta anapendana sana na wa mama huyu na ndio msiri wake yaani imetokea tu

Mimi imetokea napendwa zaidi na mamkubwa kiasi wengine wote wameshajua
 
Kwa nn mama wa kambo anakuwa na roho mbaya hivi tofauti na baba wa kambo
 
Back
Top Bottom