Wanawake wazuri hawaolewi au wanachelelewa kuolewa?

MimiKijana

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
265
243
Heshima kwenu wana JF, kwanza natanguliza Samahani kwa atakayekwazika na sababu zifuatazo, pia natanguliza angalizo kwamba sijamlenga hata mmoja huku JF ila ni kutokana na uzoefu niloupata katika hali yangu ya sasa ya ubachela.

Tuingie baharini kuangazia hizo sababu;
1. Ulevi wa mitandao ya kijamii.
Hili lina athari zaidi kwa upande wa wanawake japo upande wa kiume, wanawake wanavutiwa zaidi na mwanaume aliye maarufu au wasemavyo waswahili wa leo yaani popular mfano wanamichezo, wanamiziki au hata watangazaji wa radio na televisheni.

Kwa wanawake ni tofauti kabisa kwani asili ya mwanamke pamoja na staha yake nimtu aliyeumbwa kwa faragha yaani siowa kujionyesha au kujiweka wazi mbele ya watu ili kila mmoja amwone nakumjua undani wake.

Leo tuta lenga zaidi uchambuzi wa upande wa mwanamke na sababu haswa za kutoolewa.

Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, na kwa muda mwingi huupoteza kufuatilia mambo ya urembo,wasanii, vijimambo vya mitaani, kwenye maarusi, mitindo ya mavazi na hata ni yupi aliyependeza zaidi kipindi cha mwisho wa juma nk.

Kutwa nzima unakuta anafuatilia staa huyu alifanya nini usiku, huyu alipiga picha gani na pia nani alipatwa na jambo gani au hata kunyang’anyana mabwana.

Mwisho wa siku mwanamke kama huyu atakuwa hana cha maana alichojifunza kwenye mitandao zaidi ya kujiweka wazi kwa wanaume kumfuatilia nakumjua tabia zake za ndani.

Wanaume hupenda wanawake wasio na makuu ya kupitiliza. Mfano wa tabia wanaume wazipendazo ni pamoja na kuwa na mwanamke mbunifu na mwerevu kiasi, mwenye uzuri na umbo la wastani usiovuka hadi kusababisha kila mpita njia amkodolee macho, mwenye kujishusha na asiyependa kujiweka wazi zaidi ya mmewe.

Pia wanaume hupenda mwanamke mpole, mnyenyekevu, anae jishusha na pia kwa kiwango kikubwa mwenye hofu ya Mungu na mpenda familia na watu wanaomzunguka.

Na hakuna mwanaume muoaji anayetaka mwanamke ambaye akili yake imetawaliwa na mitandao ya kijamii wakati wote.

2. Kutokupenda kufanya kazi za nyumbani.

Wanawake wengi waliobahatika kusoma vizuri na kuwa na uelewa mpana wa mambo, hapa aimaanishi mwanamke kutosoma ndio utaweza kuolewa,la asha bali kuweza kukaa pamoja na wanaume katika ngazi za kiutendaji na hata maamuzi huwafanya kujiona sawa na wanaume na kutotaka kujiweka chini ilivyo desturi na hata kudai haki sawa kati ya wanaume na wanawake.

Hakuna mwanume aliye radhi kumwuoa mwanamke asiyetaka kumuheshimu mme kwa kusema haki sawa kwa wote hata ikiwezekana majukumu ya familia atadai yafanyike kwa usawa mfano hata kupika,kuosha nakulea watoto na hata wakati wa uzazi kulea kichanga pamoja badala ya mwaume kwenda kujitafutia riziki ili alete chakula nyumbani.

Mfano wa haki sawa kwa wote kama tunavyoweza kuona kwenye filamu wanaume wakifanya kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake, basi na wao ndio wameweka nukta kufanya kazi za nyumbani.

Kutokana na hali hii, badala yake wanawake baadhi wamekua wakitumia muda wa kujifanyia shughuli za nyumbani hutumia kujiremba tangu mawio hadi machweo, huku wakitembea na vijibegi ambavyo ni vijisaluni vidogo vyenye urombo wote.

Ukiangalia kucha zake za mikononi na miguuni huwezi kujua ni lini vidole vya mikono vimefuangua za mme au watoto, au ni lini amekaajikoni na kumenya viungo na kupika ama hata kufanya usafi wa ndani ikiwamo chumba chake na mmewe mtarajiwa kwani hajazoea hayo na humwachia mtumishi wa ndani.

Hakuna mwaume wa kiafrika anayependa muda wote shughuli za ndani zifanywe na mwanamke mwingine ambaye sie mkewe aliyemwoa kwani kuongezeka kimajukumu mwanamke kunamfanya akose muda wa kumuudumia mme hivyo wanaume kukwepa wa aina hii.

Kwa hali hii usitarajie mwanaume akuoe kwa sababu anajua ni matatizo anapeleka nyumbani.

3. Kujipodoa hadi sura yako ya asili inasahaulika.

Ni kweli wanaume hupenda mwanamke mrembo na mwenye kupendeza.

Lakini hii haimaanishi ndio ujipodoe hadi uchukize. Kila kitu kwa kiasi chake kwa sababu kitu chochote kikizidi huwa ni sumu.

Jirembe kwa kiasi, hili litavutia watu walio makini kutaka kukuoa, lakini ukiwa ni wa kujiremba hadi ukapindukia, hakuna muoaji atakaye kuwa tayari kujiingiza kwenye hatari hii.

Tena ikumbukwe kuna baadhi ya wanaume wao hupenda mwanamke asiye jiremba (wenyewe huita natural)

Hizi ni baadhi tu, na wewe unaweza kuongezea ili kuwakumbusha wasichana wanaotaka kuolewa, wajue tabia za waoaji.

Na wewe ongeza sababu yako hapo chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom