Wanawake wanaweza, wengi tunabisha kishabiki tu……………….. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wanaweza, wengi tunabisha kishabiki tu………………..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 5, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanamke akipewa nafasi anaweza mengi ambayo mwanaume hayawezi linapokuja suala la mtu kupata kile anachokihitaji maishani wake. Mwanamke ndiye mwenye subira kuliko mwanaume,ndiye msamehevu kuliko mwanaume, ndiye mweka akiba mzuri kuliko mwanaume, ndiye mpangaji mzuri kuliko mwanaume.

  Ni mara chache kukutana na mwanamke asiyejua bajeti, hata kama anafanya bajeti kwa ajili ya kununua vipodozi. Hata ukiangalia vijana wawili wanaoanza maisha baada ya masomo. Yule wa kike na wa kiume, ambao wanapata mshahara sawa. Utakuta kwamba yule wa kike atamudu kununua vifaa vya ndani haraka zaidi kuliko mwanaume. Unawezakusema ni kwa sababu anahongwa au kusema ni kwa sababu wanawake wanapenda samani na mapambo.

  Lakini tafiti nyingi zimethibittisha kwamba, mwanamke ni mzuri sana katika kuyaelekea malengo yake, anakuwa na subira zaidi wakati wa kuelekea malengo yake na anajua afanye nini ili mambo yaende sawa katika mazingira ambayo mwanaume anababaika, hasa katika uhusiano, na ndio chimbuko la msemo huu wa, ‘nyuma ya kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke.’ Hii ina maana kwamba. Mwanaume, hata angekuwaje , mafanikio yake yangetegemea sana ana mwanamke wa aina gani karibu yake.

  Ukiona mwanaume amefanikiwa, ujue wazi kwamba, mwanamke aliye nyuma yake, awe ni mkewe, rafiki au mshauri wake, ndiye chachu ya mafanikio hayo. Kwa wanaume ambao hawawaamini wake zao kiasi cha kutowashirikisha kabisa kwenye mipango ya maendeleo na masuala mengine ya kifamilia, wanatakiwa kuanza kufanya hivyo. Mpe nafasi ashindwe kwanza. Na hata akishindwa, mjaribu tena kwa njia nyingine, labda anaweza kumudu.

  Wanaume wanaojibebesha kila jambo, mara nyingi hukwama na kurejea kwa wake zao na kusema, ‘fanya maarifa tuweze kula.’ Wakiwa na njaa, wanagundua kwamba, wanawake ni wazuri sana kwa mikakati wa kuwezesha mambo kunyooka. Wanaume wote walioamua kuwashirikisha wake zao kikamilifu katika masuala yote ya familia, wana ahueni kubwa sana.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ila mkuu sio kwamba huwa hata kwenye familia unakuta bajeti ya mtoto wa kike huwa iko juu kuliko wa kiume hiyo sio inawafanya hata mambo mengine wanayamudu..
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ahsante Mtambuzi ....mwenye masikio na asikie
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  pumu imepata mwenye kikohozi lol
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Na upele umepata mkunaji ..........
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  na kichaa kapewa rungu sokoni lol
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hakuna ubishi ktk hili na kwa kweli dunia bila wanawake ingekwisha mapema sana, pengine Yesu na mtume SAW wangekuwa wanahubiria miti tu. Lakini pamoja na yote hayo bado vidume huwa hatuthamini sana mchango wao, until the last moment
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  mkuu pumu na kikohozi hapo si ni kifo tu!
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Wanawake JF wasipate cha kulalama, thread za kuwapaisha ndo kama hizi......

  Penye wabaya wako, na mwema wako hakosi
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mwanaume ni kichwa, mwanamke ni moyo....!
  mwanamke "anaweza" kuishi bila mwanaume...

  je? mwanaume anaweza kuishi bila mwanamke?

   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Naona leo wanaume wa JF mmeamua kutoa zawadi ya Eid mapema
   
 12. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hapo umesema sawa kabisa. Ni vizuri kuwashirikisha wake zetu katika mambo mbalimbali tufanyayo. Utakuta mtu ni mfanyabiashara mkubwa lakini mkwewe hajiu lolote kuhusiana na biashara ile. Ikitokea mwanaume kafa na biashara nayo inakufa na familia nzima inaanza kuteseka.
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  GEE malizia hii nyimbo.....
  this is a man ' s world......
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  but it will be nothing without a woman or a girl

  (change to women and girls for some men )
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  which group do you belong????/
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  It depends on the occasion .......
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  when i am chatting with you?
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  I feel like a grandma .....:p
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  ahsante mtambuzi. ngoja nimwambie mkweo asome hapa.
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  tena mwambie asome between line..............
  nawaonea huruma kweli wasioijua siri hii...............
   
Loading...