Wanawake wanavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125




Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa ya kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na yenye mahitaji makubwa katika jamii.

Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hiyo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi.

Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.

Kwa wanaume ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa wanaimiliki daima.

Lakini, watafiti wa masuala ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hiyo.

Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.

Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo. Hali hii inatoa picha kwamba mzigo wa lawama hujitwika wenyewe.

Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:

1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litamfanya aanze kupoteza nguvu za kiume taratibu.

Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwabia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”

2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume husika kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.


Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi ni muhimu sana katika mapenzi.Mashosti: Wanawake wanavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume
 
hapo kwenye usafi umemaliza mkuu, kuna wanawake huwa wananuka kuanzia nywele,makwapani, mdomo na kwenye engine yenyewe hapo msisimko huwa unakata kabisa
 
Pia UCHOKOZI wa wanawake kwa waume zao unawafanya men wakose hamu ya kufanya tendo la ndoa na wengine kuamua kufanya mgomo baridi ambao hupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa
 
Ni kweli kuwa ujuzi (uliopungua au uliozidi sana), kauli na usafi husababisha athari za kisaikolojia, lakini tunapojadili suala la sita kwa sita, tusiangalie upande mmoja tu wa shilingi (Kaunga BADILI TABIA).

Kwa kuwa tendo la sita kwa sita (kuliita tendo la ndoa ni kosa) ni suala la pande mbili, lazima pande zinazohusika zishirikiane kikamilifu ili wote wajisikie raha; vyenginevyo ama humfanya mmoja akose ujasiri au kujisikia mtumwa na kushiriki kwa kutimiza wajibu tu.
 
Acheni kututupia lawama jichunguzeni vizuri matatizo mnajisababishia wenyeweeeeeeeeeeee lol.... kanyweni supu ya pweza na karanga mbichi basi
 
Wanawake wanatupiwa kila mizigo.......

Vipi kuhusu nguvu za kike?
Kauli ya mwanaume haipunguzi nguvu za kike? Usafi una nafasi ipi na ujuzi wa mwanaume?
Lakini sio wanawake Wote Bibie Baadhi yao ndio wanaosababisha Wanawaume kukosa Raha katika Tendo la ndoa munisamehe akina Dada zangu ingawa ukweli unauma nawaombeni munisamehe dada zangu kama nitawakwaza BADILI TABIA
 
Last edited by a moderator:
exactly, hata mwanaume akiwa hivyo na mwanamke anakosa stim bhana

kwa wanaume jitaidini kuziongeza bhasi kwa tende na mtindi,,,,halo halo
 
Back
Top Bottom