Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,262
- 64,382
Siku moja jioni, nikiwa nimejichokea zangu kutokana na harakati za maisha za hapa na pale, nikaamua kutinga kwenye kijiwe kimoja kwa ajili ya kupata mvinyo baridi pamoja na kwenda kusikiliza mziki nyororo; lengo ni kuburudisha akili ili siku inayofuata niweze kupambana na harakati zangu vizuri.
Baada ya kufika, nikaagiza kinywaji changu nikawa nakunywa taratibu. Baada ya kupiga kama chupa tano hivi, mara huyo mchepuko wangu wa zamani anaingia, umbo namba nane, rangi ya chungwa; nilijikuta mwili wote umelegea.
Kwa makusudi akaja mpaka mezani kwangu, akani-kiss nami nikamjibu, akasogeza kiti na kukaa, na baadaye kuletewa vinywaji vyake.
Mnavyojua tena, mambo ya starehe, nikajikuta nimesimama na kuanza kutikisa mwili kuendana na miondoko ya mdundo wa mziki, nikajikuta natanua 'distance' na kuwafikia warembo watatu waliokuwa wamekaa kwenye meza moja huku wanakunywa na kutikisa viuno vyao wakiwa wamekaa kwenye viti.
Mbaya zaidi, mrembo mmoja aliyejazia 'hips' akashika shati yangu na kuniambia, huondoki hapa, nataka nimuumize yule uliyekaa naye. Nikamuuliza kivipi? Hakunijibu, zaidi ya kunipapasa na kuanza kuamsha hisia zangu.
Akanisogeza karibu kwenye miguu yake na kunibana, na kumwambia muhudumu aniletee kinywaji changu; akaanza kuninywesha kinywaji, mnavyojua tena wanaume, kwenye mahaba hatuna sauti wala nguvu, nikawa mpole tu; nikajikuta nimeamia mazima kwenye hiyo meza.
Yule mchepuko wangu alikasirika sana, lakini alikuwa hana la kufanya akijua labda huyo aliyeng'ang'ania shati langu labda ni mpenzi wangu baada ya mimi na yeye kuachana, kumbe siyo na wala sina mahusiano naye zaidi ya siku hiyo kuonana naye pale; nikamwambia mhudumu aendelee tu kumuhudumia yule mchepuko, ingawa roho ilikuwa inaniuma sana; kwa kutekwa na mrembo ambaye simfahamu.
Nilipotaka nijitoe kwenye miguu ya mrembo; mara mrembo akazidi kunibana kwa miguu yake, na kuniuliza, 'unataka uende wapi?' Nikamwambia, kwenye meza yangu; akanijibu, 'hutoki hapa lazima tuondoke wote sitaki uende kwa yule mwanamke'.
Muda ulivyozidi kwenda, mchepuko wangu wa zamani ukaniaga na kuondoka; nasi baada ya kama nusu saa tukaondoka na huyo mrembo mpaka kwenye jumba la dhahabu.
Tukapeana mashamsham, chukua kitendea kazi na kuchochea moto. Baada ya zoezi nikamuuliza, kwa nini umeamua kuniteka? Akanijibu, ''nilitaka nimuumize yule mrembo uliyekuwa naye, kwa nini akung'ang'anie vile?''
Kweli nikajua, wanawake wanaoneana wivu sana kwenye mahusiano.