Jamaa yangu anaishi Msakuzi alipata demu sinza,amepanga chumba masta. Siku moja anaenda kwa demu wake akapokelewa vizuri tu akakaribishwa ndani. Baada ya muda kidogo akaingia jamaa ...anafahamiana na dem ni swahiba wake. Mara kidogo, dem akamuomba jamaa watoke nje kidogo yule jamaa anataka kuoga ....
Wakatoka. Mshkaji kapigwa butwaa haelewi elewi. Baada ya dakika kadhaa jamaa kamaliza kuoga akapiga simu warudi tu ndani. Wakaingia. Wakakuta jamaa keshaoga amevaa anamalizia kujipodoa kageukia dressing table. Jamaa akakaa kitandani na dem wake....wanaendeleza stori yao.
Jamaa kashika wanja na chanuo mkono mwingine kamgeukia jamaa anamuomba radhi kwa usumbufu "shem samahani kwa usumbufu..." jamaa kabaki katoa macho, anashangaa mwanaume kashika wanja. Kamaliza kupaka, kaondoka.
Badae demu kamuomba radhi mshkaji na anamwambia isimsumbue yule sio bwana wake....kwanza ni "shoga" tu. Alikua anaishi na Bwana wake Mwananyamala wamekorofisha; anaishi kwa muda pale na demu wa mshikaji.
Mambo ya Sinza.