Wanawake wanahitaji Harusi na wanaume wanahitaji ndoa.

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
150
Ukisoma Biblia takatifu ,utakuta neno ndoa limezungumzwa mara 38 katika vifungu 38 ,na ukisoma kitabu cha Methali[ 31:10-31] Mke mwema kweli, apatikana wapi?

''Huyo ana thamani kuliko johari! Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima. Kamwe hamtendei mumewe mabaya, bali humtendea mema maisha yake yote.'''

Kizazi hiki wanawake wanahitaji harusi ,na wanaume wanahitaji ndoa,ndio maana katika katika harakati za kufunga harusi wanaume wengi hukonda na wanawake wengi hunenepa sababu ,mmoja anahitaji harusi na mwingine anahitaji ndoa.

Baada ya harusi na safari ya ndoa inapoanza ,mwanamke hukonda na mwanaume hunenepa sababu ,Harusi ni sherehe ya siku moja wakati ndoa ni agano la milele,wanawake wanakamia sana harusi kuliko kukamia ndoa zao.


Mwanamke mwenye uhitaji wa ndoa huwa sio king'ang'anizi wa harusi hata siku moja ,yeye hutizama agano takatifu la ndoa ambayo inaweza kufungwa bila ya harusi wala gharama kubwa .Wanawake wa aina hii kwa kizazi hiki hawapo na wanapatikana kwa kufunga na kusali pekee.

Mwanamke anayehitaji ndoa baada ya kufika katika kilele cha mafanikio ya maendeleo ya ndoa na furaha ya ndoa yake ,hupendekeza kwa mume wake wabariki ndoa ndipo mume wake hupokea shauri la mke wake sababu ya hekima na busara ya mke wake na kuibariki ndoa.

Wanawake ,msilazimishe kufunga harusi wakati uwezo wa
wanaume wenu mdogo,harusi ni sherehe ya siku moja na ndoa ni agano la milele,tuwekekeza fikra za kutengeneza ndoa nzuri na bora na sio kuwa na hamasa ya kutengeneza harusi bora na tamu.

Dear brothers maisha ya sasa yanahitaji mwanamke mwenye akili na sio mwanamke mzuri ,sababu unaweza pata mke mzuri asiye na akili na ukapata mwanamke mwenye akili asiye mrembo-uzuri wa mwanamke huwa haudumu milele ila akili ya mwanamke hudumu milele.To be married by the person you love the most is the greatest blessing God can give.

 

Galapagosi

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
2,824
2,000
Ila kwa kipindi hiki wanawake wananenepa ndani ya ndoa kuliko hata huko walipokuwa.

Hapa kwenye mwanamke kutaka harusi mawazo yangu hapana kubwa.
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
WANAWAKE KWA WANAUME NI KAMA KACHUMBARI KATIKA PILAU BILA HIYO PILAU HALINOGI SANA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom