Wanawake wana roho mbaya sana pt 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wana roho mbaya sana pt 2

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BRO LEE, Mar 1, 2012.

 1. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Si lengo langu kuendelea kuwakwaza wale waliokwazika kwa uzi wa kwanza, bali ni kutoa mawazo yangu juu ya mtizamo wa mada tajwa.

  Wanawake wamekuwa na historia ndefu ktk maisha ya mwandamu. Toka enzi za mababu aidha kwa mtizamo wa maumbile yao au mapokeo ya kiimani(dini) wanawake walichukuliwa kuwa ni viumbe dhaifu si wa mwili tu bali hata akili(uwezo wa kutoa maamuzi sahihi)

  Kutokana na namna jamii ilivyowachukulia wanawake walikuwa wakiishi kwa kutumia hisia zaidi kwa kuwa jamii iliwaona hawawezi tofauti na wanaume ambao walipewa uwezo wa kujaribu tena na tena mpaka wakaweza.

  Katika maisha ya zamani mahusiano baina ya wazazi na watoto wao(wakiwemo wake za watoto wao) yalikuwa mazuri kwa sababu uzalishaji ulikuwa wa pamoja na jamii iliishi katika eneo moja, hakukuwa na tofauti kubwa ya hali ya maisha kati ya wazazi na watoto.

  Maisha yamebadilika, watoto wameachana na familia zao na kutafuta maisha yao, wanawake wamelazimika kutoka ndani na kuingia katika uzalishaji mali ili kusaidia katika familia. Ni kutokana na mabadiliko haya ya kimaisha wanawake wanapotambua kwamba wanaweza na kutokuweza kwao kulitokana na kunjimwa nafasi.

  Katika maisha haya mapya ya watoto ndipo tatizo linaibuka na mwanamke ananyooshewa kidole! Baadhi ya Wazazi hasa wa mwanaume wanapokwenda kumtembele mtoto wao huwa wanakwenda na familia zao(mamlaka yao) na kutaka waishi kama wanavyotaka pasipo kufahamu kwamba kila familia ina mipango yake, na iwapo yale wanayotaka hayatekelezwa lawama huwa kwa mwanamke, atazushiwa hana upendo kwa wakweze, mchoyo nk. Hapo mkakati huanza wa namna ya kumngo'a kwa kumchonganisha na mumewe hata kwa mambo ya kutunga.

  Iwapo mwanaume atakuwa hajaondoka kwao vizuri(bado anaamuliwa/kushauriwa na wazazi wake) uwezekano wa mwanamke kunyanyasika ni mkubwa na hata ndoa kuvunjika, unyanyasaji huo huweza pia kuwahusisha ndugu wa mwanaume hasa dada. Aidha wanawake kwa kutokujua haki zao wengi waliamua kuondoka na kuanza maisha mapya magumu huku wakiachwa bila msaada japo walichangia katika mali za familia.

  HIVYO, wanawake wengi wamekuwa wakifanya maamuzi ya kujihami kutokana na sauti ambazo zipo ndani yao, sauti hizo zinatokana na makuzi aliyokulia(mahusiano baina ya mamake na babake). Iwapo alikuwa anamwona mamake akinyanyasswa na wakwe zake au na mawifi au mashemeji, mwanamke huyu akiolewa atakuwa anajihami watu hao wasifike nyumbani kwake, iwapo watafika atajitahidi kutafuta namna ya wao kuondoka mapema maana kwa hisia zake uwepo wao ni hatari kwa ndoa yake, ni kwa kupitia hisia zake hizo anapojikuta amesababisha mgogoro usio na maana.

  Iwapo mwanamke aliwahi kusimuliwa ubaya wa wasichana wa ndani, kwa maana ya kuwa na mahusiano na mume wa mhusika, atakapo kuwa na binti wa kazi hatataka awe karibu na mumewe na akiona wanaongea vizuri au kucheka anahisi hatari inakaribia, atajitahidi kumtenga, kumkaripia nk, binti huyo anaweza kuona msaada ni baba na hivyo akawa anamshirikisha katika matatizo yake jambo ambalo litafanya wawe karibu zaidi na mwishowe kile alichokuwa anakikwepa kikatokea na hivyo atabaki na mtizamo wake kwamba wasichana wa kazi hawafai.

  Halikadhalika iwapo watoto walifukuzwa na mama yao wakamwacha baba yao katika nyumba na mama yao akawa anajilaamu kwa kutomwibia na kujenga nyumba, akiolewa atakuwa anasumbuliwa na hiyo sauti na akipa nafasi atamwibia mumewe ajenge nk.

  Kwa mtizamo wangu yale wanayoyafanya wanawake yanachangiwa sana na matendo ya wanaume,hivyo haifai kuwalaumu moja kwa moja pasipo kuangalia upande wa pili. Udhaifu tunaouana kwa wanawake ulichochewa na ubinafsi wa wanaume kwa kutaka kuwafanyia maamuzi ili kutimiza matakwa yao.

  Wanawake nawapenda ni mama zangu, mke na dada zangu.

  Nawasilisha;
  BRO LEE
  1/3/2012
   
 2. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ushawekewa Limbwata wewe! Kaa kimya tuu...
   
 3. edcv

  edcv Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna point za chanya katika mada, ingawa mtoa mada hajatoa picha kamili ya vigezo vyote vinavyopelekea hao wanawake kuwa hivyo. Mfano mmoja2 mwanamke kaona mama yake anavyofanyiwa na wifi zake hivyo anaogopa ndugu wa kike wa mmewe(yeye ni wifi pia kwa m2 mwingine kwa hiyo akiwaza kichwani anayomfanyia wifi yake akilinganisha ya yale yeye anayofanyiwa, anapata picha kamili ya mahusiano ya m2 na dada za mmewe yanavyotakiwa kuwa-mwishowe anajirekebisha)
  CONCLUSION: as I mentioned before, there are more driving forces to their behaviour that what u've just mentioned here.Due to lack of enough evidence therefore, I hereby agree to disagree...
   
Loading...