Wanawake wana lao jambo!


Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Likes
1,328
Points
280
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 1,328 280
Kuna malalamiko mengi ya wanawake dhidi a wanaume. Wanawake wamekuwa wakiwalaumu wanaume kuwa, ‘wana tamaa,' ‘hawaridhiki' ‘hawatulii na kauli nyingine nyingi tu za kuonesha kwamba huyu kiumbe mwanaume ni mtu asiyemuaminifu katika uhusiano hata chembe.

Lakini sio waume tu, bali pia wanawake wamekuwa wakiwalalamikia wanawake wenzao kuwa wao ndio chanzo cha kuyumba kwa ndoa zao au uhusiano na wanaume zao. Ni hivi karibuni katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Idd El Fitri, kuna mwana mama mmoja humu jamvini anajiita NOT ENOUGH aliweka thread akiwatahadharisha wanawake wenzie (bila shaka wasioolewa, au nyumba ndogo) kuwa watulie na wawaache nao wafaidi Sikukuu na waume zao, maana kipindi hiki ndicho kipindi ambacho kinaaminika kuwa wanaume wengi hukimbilia kwa mahawara na kutelekeza familia zao. Kichwa cha thread hiyo kilisema hivi "Nyie nyumba ndogo muache waume za watu wakae na familia zao kesho"

Hivi ni kweli kwamba wanaume wana tamaa? Swali hili haliwezi kujibiwa kwa kusema ndiyo au hapana, bali linapaswa kujibiwa kimazingira. Lakini hebu tuwe wakweli wa nafsi zetu, hivi ni kweli kuwa wanaume ndio wenye tamaa peke yao au na wanawake pia? Swali hili pia lazima lijibiwe kwa mantiki kwamba lazima kuwepo ushahidi wa kimazingira na kimtazamo katika kujibu swali hilo.Kwa kifupi ni kwamba wanaume hawatamani bure wanawake bali wanawake ndio wanaotengeneza mazingira ya kuwatamanisha wanaume kwa kuiweka miili yao katika muonekano ambao ni lazima wanaume wakiona udenda utawatoka.

Kwa utafiti nilioufanya tangu nilipoanza kuwajua wanawake kwa maana ya kuwa na uhusiano nao kingono, nimegundua kwamba wanawake wana tamaa na kujipendekeza kwa wanaume kuliko inavyofikiriwa. Sema tu jamii imemfunga mwanamke kwamba ni jambo la aibu yeye kumtamani mwanaume na kumwambia waziwazi kwamba amemtamani na angependa kufanya naye tendo la ndoa.Wanawake hutumia ishara za nje ambazo kama mwanaume hawezi kuzigundua, huumia sana kihisia.

Unaweza kushangaa pia kwamba hata wale wanawake wasagaji hawawezi kuwaambia wanawake wenzao kwa kutumia maneno moja kwa moja kwamba wanawatamani na badala yake hutumia matendo yenye kuashiria tamaa zao au kusifia baadhi ya viungo vya miili ya hao wanawake wenzao.

Pia katika utafiti wangu huo nimegundua kwamba mwanamke anaweza kujinyima au hata kumnyima mwanae lishe ili apate kununua vipodozi, mikorogo na makorokoro mengine ili kuwavutia wanaume.

Kama huamini, hebu M-date (hata sijui Kiswahili chake) mwanamke kwa mara ya kwanza, uone jinsi atakavyopata shida katika maandalizi kabla ya kukutana kwenu, kwa huku mjini, ni jambo la kawaida sana kwa mwanamke kuazima au hata kukodisha mavazi na vidani vya dhahabu ili kumudu kumvutia kimapenzi huyo mtu aliye M-date. Sasa tabu yote hiyo ni ya nini?

Nisiwachoshe, nitawaletea vijimambo zaidi vya wanawake muda ukiruhusu……
 
arabianfalcon

arabianfalcon

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
2,292
Likes
10
Points
135
arabianfalcon

arabianfalcon

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
2,292 10 135
mmmmh! Msumari huo!
 
Smile

Smile

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Messages
15,407
Likes
235
Points
160
Smile

Smile

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2011
15,407 235 160
mmh makubwa.iyo ni theory yako.yaani mtu akaazime nguo kisa ni kumeet mpenzi mimi huwa nalipuka tu ovyoovyo
 
Digna37

Digna37

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2010
Messages
723
Likes
45
Points
60
Digna37

Digna37

JF-Expert Member
Joined May 17, 2010
723 45 60
Pole ndg yangu. Inaelekea una-date wanawake machakaramu, maana kwa jinsi ninavyofahamu ndio huwa wana vituko kama hivyo, nao sio wengi na wanapatikana maeneo fulani tu.
 
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
3,577
Likes
15
Points
135
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
3,577 15 135
Huo ni ukweli wanawake wengi hujisababishia matatizo mengi ya kuvaa nguo zenye kuwavuta wanaume hivyo ndio mara huwa wanaingia kwenye vishawishi vingi kila wakati nawaomba wabadilike
 
feis buku

feis buku

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
2,370
Likes
8
Points
0
Age
29
feis buku

feis buku

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
2,370 8 0
mtambuzi kiukweli leo huna ulilotambua!!
 

Forum statistics

Threads 1,251,848
Members 481,916
Posts 29,787,519