Wanawake Wakristo zaeni acheni kufunga vijiti

bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
620
759
Dunia inaenda kasi sana. Wanawake Wakristo Tanzania niwaombe zaeni bila kuogopa kwa sababu watanzania bado tupo 45M.

Lakini nimeexperience miaka ijayo makanisa yatakosa watu kwa sababu wamama kujifunga vijiti na kuzaa mtoto mmoja tu. Na niombe makanisa na hata waislam wahimize wakinamama kuacha kuweka vijiti kama bado vijana na nafasi wanazo za kuzaa badala ya kuwa na kitoto kimoja tu.

Tusiangalie sana mambo ya kuwasomesha kama tutawasomesha kwenye elimu hii ya serikali hatuna budi kuwa na watoto zaidi ya wanne au watano ili jamii ya kitanzania ikue. Kwa sasa niko hapa hospital kila siku wadada zaidi ya kumi wanafika kuwekewe vijiti vya kuzuia mimba.

Hii naiona kama Ulaya ilivyo sasa nchi kama Ujerumani na nchi zingine za Ulaya makanisa yamekuwa tupu. Pia Ujeruman na nchi kama Ireland wanaaamua kuchukua wakimbizi kuja kusaidia zile kazi ambazo hazihitaji more skills.

Kama taifa vijiti bado ni muhimu lakini kwa vijana nashauri isiwe muhimu sana na makanisa na misikiti waendelee kutoa elimu kuhusu kuzaa watoto wanne mpaka watano.


Nawakilisha.....
 
Itafikia wakati na sisi tutaweka Waziri wa mapenzi kama Wahispani kwa kasi hii ya kuchoropoa mimba na kufuata uzazi wa mpango
 
kwahiyo alipoweka kijiti mke wa jirani yako ukageneralize kwa wanawake wote wa kikristo?

mtu maisha yake anaona kabisa atamudu kutoa malezi bora kwa watoto wawili anaamua kufunga kizazi..halafu roho unakuuma?
wale watoto chokoraa ukiwaona kile majalalani wanatafuta chakula hivi unajiskiaje?
unayajua maumivu anayopata mzazi pale anapishindwa kutimiza mahitaji ya watoto wake na watoto kushindwa kufurahia maisha kama wenzao?
 
Siungi mkono hoja! Kwa sasa maisha ni magumu sana na kuzaa mitoto mingi ni kujiongezea mzigo wa kulea... Ajira zimekuwa za wasiwasi na upatikanaji wa mahitaji mengine ya muhimu umekuwa mgumu sana... Sasa hivi wanandoa wengi vijana wanazaa mtoto mmoja ili kuzima kelele za ndugu then wanaendelea kula maisha...
 
Hili la maisha magumu napingana nalo sana, maisha magumu isiwe hoja ya kutokuzaa watoto wengi,

Kinachosababisha watu waache kuzaa ni uzungu mwingi umetujaa, ila ukiangalia katika familia nyingi wengi wetu tumezaliwa tuko watoto wanne mpaka wanane, na kwa maisha ya wazee yetu yalikuwa magumu zaidi ya maisha yetu lakini wazee wetu walijitahidi mpaka tumefika hapa tulipo,

Tuache uzungu, tuzae angalau hata watoto wa3 au wanne. Then tuhangaike kuwasomesha watoto wetu, after sometimes tutajivunia kuwa na watoto wengi wenye maisha mazuri na wala sio kuwa na magorofa au magari mengi mjini.
 
Wakati unawahimiza wazae yahimize makanisa na misikiti kutengeneza fursa za ajira. Kuzaa ni jambo moja, ngoma ipo kumtengeneza binadamu kuwa mtu.
 
Dunia inaenda kasi sana. Wanawake Wakristo Tanzania niwaombe zaeni bila kuogopa kwa sababu watz bado tupo 45M. Lakini nimeexperience miaka ijayo makanisa yatakosa watu kwa sababu wamama kujifunga vijiti na kuzaa mtoto mmoja tu. Na niombe makanisa na hata waislam wahimize wakinamama kuacha kuweka vijiti kama bado vijana na nafasi wanazo za kuzaa badala ya kuwa na kitoto kimoja tu. Tusiangalie sana mambo ya kuwasomesha kama tutawasomesha kwenye elimu hii ya serikali hatuna budi kuwa na watoto zaidi ya wanne au watano ili jamii ya kitanzania ikue. Kwa sasa niko hapa hospital kila siku wadada zaidi ya kumi wanafika kuwekewe vijiti vya kuzuia mimba. Hii naiona kama ulaya ilivyo sasa nchi kama ujerumani na nchi zingine za ulaya makanisa yamekuwa tupu. Pia ujeruman na nchi kama ireland wanaaamua kuchukua wakimbizi kuja kusaidia zile kazi ambazo hazihtaj more skills.

Kama taifa vijiti bado ni mhm lakini kwa vijana nashauri isiwe mhm sana na makanisa na misikiti waendelee kutoa elimu kuhusu kuzaa watoto wanne mpaka watano.


Nawakilisha.....
unachokiona wengi hawakioni hivyo hutapata support kubwa, lakini uko sahihi sana.
 
Ukizaa ukushindwa kuwatimizia mahitaji ni dhambi kubwa kwa mungu. Fungeni tu jaman maisha magumu huku kitaaa maana hakuna namna
Mbona kama unapingana na muumba? Aliyekuambia dunia imejaa nani? Yeye katupa kazi moja tuujaze ulimwengu tukijaa atafunga yeye! Suluhisho nikutokuiga maisha ya academy sikuli,international na kuondoa woga wa kuishi vijijini,ardhi zipo,mito ipo jamani tuingie shambani maisha mazuri huku!
 
Embu toa kwanza neno..WAKRISTO,,ujumbe unaweza kueleweka! alaf unataka wazae ili? Nan atalea au unajua kuzaa tuu
 
Naona watu wanashule ndogo ya Elimu kuhusu uzazi wa mpango. Ngoja nieleze kidogo faida za uzazi wa mpango.

1 kupunguza umaskini kwa kuwa utakachopata hakitakuwa kwa ajili ya social services kwa wana family na hivyo unaweza ukajenga, kuwekeza na mambo mengine ya kiuchumi.

2.Kuweka uwiano mzuri kati ya mtoto na mtoto (at least 2 years interval) na hivyo kuongeza uwezekano wa mtoto kuendelea kukua vyema na mwenye Afya njema. Hiki kipindi ni Muhimu kwa mama kupumzika (regain strength before she is pregnant again) na hivyo kushiriki uzalishaji mali.

3.Kumpa mwanamke sauti kwenye maamuzi ya family hadi Taifa (women empowerment), hii ni kwa 7bu anashiriki uzalishaji mali.

4.Kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi. Hii ni kutokana na kupungua mimba ambazo mwanamke angeshika (In pregnancy death and life are equally 50%,so anything can happen between the two).

*nishie hapo kwanza*
 
Kama wewe ni jinsia ya "ke' onesha mfano na kama ni "me" kamshawishi mkeo au dadako afanye hilo zoezi ili wajaze mapori ya huko kwenu maana yamegeuka maficho ya vibaka na ghuest bubu nyakati za jioni.
 
mbona umelenga sana wakristo

hao wadada wanaokuja kuwekwa vijiti amna wakiislam??
 
Dunia inaenda kasi sana. Wanawake Wakristo Tanzania niwaombe zaeni bila kuogopa kwa sababu watz bado tupo 45M. Lakini nimeexperience miaka ijayo makanisa yatakosa watu kwa sababu wamama kujifunga vijiti na kuzaa mtoto mmoja tu. Na niombe makanisa na hata waislam wahimize wakinamama kuacha kuweka vijiti kama bado vijana na nafasi wanazo za kuzaa badala ya kuwa na kitoto kimoja tu. Tusiangalie sana mambo ya kuwasomesha kama tutawasomesha kwenye elimu hii ya serikali hatuna budi kuwa na watoto zaidi ya wanne au watano ili jamii ya kitanzania ikue. Kwa sasa niko hapa hospital kila siku wadada zaidi ya kumi wanafika kuwekewe vijiti vya kuzuia mimba. Hii naiona kama ulaya ilivyo sasa nchi kama ujerumani na nchi zingine za ulaya makanisa yamekuwa tupu. Pia ujeruman na nchi kama ireland wanaaamua kuchukua wakimbizi kuja kusaidia zile kazi ambazo hazihtaj more skills.

Kama taifa vijiti bado ni mhm lakini kwa vijana nashauri isiwe mhm sana na makanisa na misikiti waendelee kutoa elimu kuhusu kuzaa watoto wanne mpaka watano.


Nawakilisha.....
Nakuunga mkono asilimia 100 tz bado INA nafasi kubwa ya watu kuishi na kufanya kazi mapori bado hayajajaa sehemu za kuishi bado ziko nyingi,

hizi tabia za kiulaya ulaya zitakuja kututokea puani.
Ujerumani sasa hivi wanalia inasemekana wanawake wanadai pesa sasa hivi ili wazae.
Baada ya somo la uzazi wa mpango kuwakolea.

Taifa lolote bila watoto ujue linakwenda kuangamia
 
Mkuu una maana watu wazae watoto wengi ili tu kujaza makanisa na misikiti!!? Mm nafikiri tuanze kwanza kuwahimiza wale wasiohudhuria hizo nyumba za ibada wahudhurie uone kutavyofurika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom