Wanawake Wakristo zaeni acheni kufunga vijiti

Wanawake Wakristo zaeni acheni kufunga vijiti

Napenda kuwa na watoto wengi, nikijaaliwa uzima na afya njema lakini pia nafsi itaumia sana kama nitashindwa kuwapa watoto wangu mahitaji yao.... Napambana zikinitembelea nitakua ambassador wa leba make kila mwaka naenda.
Yaan wew kaa Mimi..
I wish nizae watoto wengi.
 
Dunia inaenda kasi sana. Wanawake Wakristo Tanzania niwaombe zaeni bila kuogopa kwa sababu watanzania bado tupo 45M.

Lakini nimeexperience miaka ijayo makanisa yatakosa watu kwa sababu wamama kujifunga vijiti na kuzaa mtoto mmoja tu. Na niombe makanisa na hata waislam wahimize wakinamama kuacha kuweka vijiti kama bado vijana na nafasi wanazo za kuzaa badala ya kuwa na kitoto kimoja tu.

Tusiangalie sana mambo ya kuwasomesha kama tutawasomesha kwenye elimu hii ya serikali hatuna budi kuwa na watoto zaidi ya wanne au watano ili jamii ya kitanzania ikue. Kwa sasa niko hapa hospital kila siku wadada zaidi ya kumi wanafika kuwekewe vijiti vya kuzuia mimba.

Hii naiona kama Ulaya ilivyo sasa nchi kama Ujerumani na nchi zingine za Ulaya makanisa yamekuwa tupu. Pia Ujeruman na nchi kama Ireland wanaaamua kuchukua wakimbizi kuja kusaidia zile kazi ambazo hazihitaji more skills.

Kama taifa vijiti bado ni muhimu lakini kwa vijana nashauri isiwe muhimu sana na makanisa na misikiti waendelee kutoa elimu kuhusu kuzaa watoto wanne mpaka watano.


Nawakilisha.....
HAWA WATU BADO WAPO?
 
Wanaadam inabdi tujue kwamba anaetoa rizki ni Mungu.
Kuzaa watoto wengi au wachache hakukufungulii milango ya rizki wala kukifungia..
Kuna watu wana mtoto mmoja na wanashindwa hata kumnunulia unga wa uji na kuna watu wana watoto watano na wote anapeleka English medium.

Kipato na wingi wa watoto havina uhusiano.
 
Anayetaka watu waongezeke Duniani ni Mungu. Mungu ndiye anayeamua nani aje duniani na kwa Tumbo lipi na mwanaume yupi ahusike.

Namshukuru Mwenye Enzi Mungu kunishirikisha katika uumbaji. Naam Nipo tayari kuwabebesha Mimba wanawake wowote ambao nitajaaliwa kuzaa nao nukta
 
kwahiyo alipoweka kijiti mke wa jirani yako ukageneralize kwa wanawake wote wa kikristo?

mtu maisha yake anaona kabisa atamudu kutoa malezi bora kwa watoto wawili anaamua kufunga kizazi..halafu roho unakuuma?
wale watoto chokoraa ukiwaona kile majalalani wanatafuta chakula hivi unajiskiaje?
unayajua maumivu anayopata mzazi pale anapishindwa kutimiza mahitaji ya watoto wake na watoto kushindwa kufurahia maisha kama wenzao?
Haya ni mawazo ya kikafiri
 
Wakati unawahimiza wazae yahimize makanisa na misikiti kutengeneza fursa za ajira. Kuzaa ni jambo moja, ngoma ipo kumtengeneza binadamu kuwa mtu.
Sio tu Makanisa na Misikiti kutengeneza fursa za ajira, lakini pia kutengeneza programs madhubuti kupunguza Idadi ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
 
Back
Top Bottom