Salute kwako mkuu, hawa viumbe ni mama zetu,dada zetu, mabinti zetu, Mungu azidi kuwabariki
kuna siku wife alinibamba n atext ya mchepuko, alikasirika akanisusia mtoto kwa lisaa limoja tu,, alijifungia chumbani na akagoma kufungua, nimejaribu kumuomba tuongee yaishe akaniambia anapaki vitu vyake aondoke nibaki na mtoto, nilihisi kukojoa dagaa maana kitoto kinalia nimetumia mbinu zote hakinyamazi, maziwa hataki, maji hataki, mpaka nimeogesha ila mwendo ni ule ule, kubeba mgongoni siwezi, ilibidi tu nipige goti kwawife niombe msamaha