Wanawake wabakaji Zimbabwe mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake wabakaji Zimbabwe mahakamani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 27, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,011
  Likes Received: 3,615
  Trophy Points: 280


  [​IMG]Mipira ya Kondomu


  Polisi wa Zimbabwe wanaamini kuna mtindo wa wanawake kuwabaka wanaume Zimbabwe , ili kutumia mbegu zao za kiume katika ushirikina kujitajirisha.
  Imechukuwa zaidi ya mwaka mmoja polisi kuwakamata wahusika na siku ya Jumatatu wanawake watatu walifikishwa mbele ya mahakama katika mji mkuu Harare kwa mashtaka ambayo yameishangaza nchi nzima.
  Mtu mmoja aliyepitia madhila hayo hakutaka jina lake kutajwa, alielezea yaliomkuta katika televisheni ya taifa mwezi July ambapo tukio hilo lilitokea baada ya yeye kupewa lifti na kundi la wanawake watatu mjini Harare.
  "Mmoja wa wanawake hao alinurushia maji usoni na baadae wakanidunga sindano iliyonipa uchu wa kutaka kufanya ngono" alisema bwana huyo.
  "Waliisimamisha gari na kunilazimisha kufanya tendo la ngono na kila mmoja wao nikitumia mipira ya Kondomu.Baada ya kumaliza shughuli hiyo waliniacha mwituni uchi wa mnyamaa".
  "Watu waliokuwa wakikata nyasi walinisaidia kuwaita Polisi, walionipeleka hospitali kupata matibabu kutokana na ile dawa niliyodungwa kwa kuwa bado nilikuwa na hamu isiyopungua ya kufanya ngono" Aliongeza mwanamume huyo
  Wanawake hao wanatarajiwa mahakamani kwa mashtaka 17 ya kumdhalilisha na kumlazimisha mtu kufanya asilolitaka-sheria nchini Zimbabwe haitabui ama haina kipengee kuhusu kitendo cha mwanamke kumbaka mwanamume.
  Wanawake hao walizuiliwa mapema mwaka huu katika mji wa kati wa Gweru, 275km (maili 170) kusini-magharibi mwa Harare, baada ya maafisa kugundua mipira 31 ya kondomu iliyotumika, katika gari waliokuwa wakisafiria.

  Wanawake hao wamekanusha mashtaka wakisema kuwa wao ni makahaba na walikuwa na shughuli nyingi zilizowanyima fursa ya kutupa mipira hiyo ya Kondomu.

  chano .
  BBC Swahili - Habari - Wanawake wabakaji Zimbabwe mahakamani
   
Loading...