Wanawake wa siku hizi

Wanawake wa siku hizi

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,119
Leo nilikuwa nimeenda kupunguza nywele na msitu wa ndevu kidevuni. Sasa kama kawaida ya sehemu za kukatia nywele siku hizi huku mjini baada ya kukata nywele unaenda kuosha na huko unakutana na wadada. Sasa kwenye mazungumzo yao walikuwa wanazungumza mwanamke Bora wa kuoa Kati ya wa mjini au kijijini. Sasa baada ya majadiliano yao mmoja wao akaniuliza nini maoni yangu kwenye hilo.

Wanawake wa Sasa/Siku hizi
Kwa mtazamo wangu kutokana na experience niliyopitia na kuona ni kuwa zaidi ya 75% ya wanawake wa sasa ni WADANGAJI haijalishi wameolewa au wako single, wana Kazi ama la, wakubwa kwa wadogo.

Sababu kubwa ya hili ni TAMAA ambazo wanawake wengi huwa nazo hasa baada ya kukaa na kushauriana wao kwa wao. Mfano sasa hivi ni kawaida wanawake kupeana ushauri wa “Toka na fulani ana hela, atakupa hiki na kile” hata kama huyo anayeambiwa ni mke wa mtu.

Kingine ni ukweli kwamba uwezo wa mwanamke kumkataa mwanaume ni 25% tu so baada ya kuja kwa technology hasa simu imekuwa rahisi zaidi kumtongoza mwanamke hivyo rate ya kusalitiana imeongezeka sana. Siku hizi ni kawaida watu kuwa kitandani lakini Kila mtu anachat na mpenzi/wapenzi wengine.

Single Mothers, mtanisamehe “Single Mothers” ambao ni decent lakini majority ni makahaba wa kutupwa. Sababu kubwa huwa ni kutaka kuonyesha Jamii kwamba they can survive wakiwa wenyewe na hasa wale waliokuwa nao kwenye mahusiano. Sasa ili kufikia hii hujikuta wanatumiwa sana na wanaume.

Wanawake wenyewe ndio wamekuwa vinara wa kuharibu mahusiano ya wanawake wenzao. Ni rahisi mwanamke mmoja kumuita mwenzie shoga huku akiwa anamuwinda au kutoka na mumewe.

Na sababu nyingine nyingi ambazo kiuhalisia hazitofautishi mwanamke wa mjini au wa kijijini. Kwa kipindi tulichonacho sasa hivi kuna kitu kimoja tu wanaume wanaweza kufanya “Kuishi na wanawake kwa akili”
 
Flattery make a Friend ...Truth make an Enemy.

Ulichosema kina ukweli ndani yake.

All in all ktk kila Waovu kuna wema ...nakam hamna wema. Kuna mmoja ni muovuuuuuuu mwingine ni muovu.
 
"Kuishi na wanawake kwa akili" hili andiko hata sijui liliandikwa mwaka gani
 
Wanawake wema wapo wengi tu,na wadangaji pia wapo wengi tu,kazi kwako kuchanganua yupi mwema na yupi mdangaji!
 
Siku hizi hata wanaume tumepungua sana. Vimebaki vivulana vingi vikishindana tabia na hao wanawake wasiojielewa!

Kwenye kila malaya wa kike, kuna malaya wa kiume. Kwa kila mdangaji, kuna mdangwaji pia!

We're all guilty!
 
Siku hizi hata wanaume tumepungua sana. Vimebaki vivulana vingi vikishindana tabia na hao wanawake wasiojielewa!

Kwenye kila malaya wa kike, kuna malaya wa kiume. Kwa kila mdangaji, kuna mdangwaji pia!

We're all guilty!

You are very right mkuu, sasa kuna vivulana na kuna Mazee hizi groups 2 zimeharibu sana mambo ingawa zina character tofauti
 
Back
Top Bottom