Sijawahi kuona wala kuskia utafiti wowote unaonesha ama kuzungumzia kuwa ndoa nyingi zinazovunjika au zenye matatizo lukuki ni zile ambazo zimetokana na waliokutana au kutongozana kupitia mitandaoni. Kila siku tunashuhudia wake za watu wanavyogegedwa na waliolewa bila kupitia kwenye mitandao. Kutongoza online siku hizi imekuwa shida sana kuliko physically maana wengi wanaogopa kukutana na mtu asiyemfahamu kutokana na matukio ya kutisha yanayozidi kushika kasi kupitia mitandao ya kijamii.Sijawahi huona Simba Mfalme wa Pori anawinda sanamu la swala...!!!
Online dating ni playground ya wasio na uwezo wa kuwinda...
Mi ninavyojua wa mtandaoni ndo hawa hawa waliopo barabarani, ofisini, mtaani, kanisani, vyuoni. Na kwengineko
Jaman wana JamiiForums, wanajamvi. Hivi mtu unaweza ukatongoza mpaka kuoa mwanamke ambae umemtongoza mitandaoni "social networks" bila kuonana akakubali kwa kuona picha tu? Je atakua mwaminifu kwenye ndoa yake?
NAWASILISHA WANAJAMVI.
Kiongozi naomba ufafanue hapo bold kama hutojali..!Sijawahi huona Simba Mfalme wa Pori anawinda sanamu la swala...!!!
Online dating ni playground ya wasio na uwezo wa kuwinda...
Tuombe radhi members wa JF, humu kuna member wenye kariba na nyadhifa tofauti nchi hii.Humu kuna magubegube na magumegume yaliyoshindikana hakuna mume wala mke. Usibishe jaribu uone....
Kwanza afahamu wengine ni verified user humu kama kina Nicas Mtei, Yericko Nyerere, Ben Saanane, Mwigulu, Kigwallah, Lema, Dr Ndugurile, Mchungaji Msigwa n:k na usisahau marehemu Regia Mtema alikuwa active member hapa mmu na aliwahi kutafuta mchumba kwenye thread moja hivi baadaye ndio akaamuwa kubadili jina Fekelo na kutumia jina lake halisi kila mtu akashangaa kumbe mmu imetoa mbunge! Na leo hii Mmu imetoa Rais wa TFF halafu anatokea mtu tu from no where unawavunjia heshima watu na heshima zao, huu ujuha.hao wa huku mitandaoni si ndio hao hao wa mtaani
Jaman wana JamiiForums, wanajamvi. Hivi mtu unaweza ukatongoza mpaka kuoa mwanamke ambae umemtongoza mitandaoni "social networks" bila kuonana akakubali kwa kuona picha tu? Je atakua mwaminifu kwenye ndoa yake?
NAWASILISHA WANAJAMVI.
Kweli Kabisaa Mkuu Yaani Social Networks ZImesaidia Sana,unampata Mchumba Ukiwa Chumbani/gheto Umepumzika
jamani mbona mi nimepata humu humu.... kazana kaka wapo wengi tu, tena visu kuliko unaowaona huko alaf wapole lol!!!
mkuu ni kweli kabisa, we fikiria mtu upo chumbani umishakula, unaangalia zako Taarifa ya habari, na ulikuwa ume-post uzi wa kutafuta mchumba tuseme JAMII FORUMS, wakati unachukua simu yako kuingia jf, unakutana na PM mnaanza kubadilishana mawazo kidogo then namba za simu, then kama mpo Whatsupp, mnatumiana Picha mbali mbali, mnapanga kukutana rasmi, mnakutana Inshallah kila mmoja anamwangukia mwenzake moyoni! yaani ni raha sana! achana na hawa wa mtaani kwanza wanaringa sana halafu wanajifanya hawana muda! Mitandao ya kijamii imesaidia sana ingawa wetu waliomo jf age imeenda sana.
Mnanishangaza sana, kwani nikitongoza wa mtandaoni namuoa siku hiyo hiyo?
Huwa nyie mnaotongoza wa kanisani mnafuata principle gani kuwaoa hao mnaowatongoza? Mnatongoza leo na kuoa kesho au mnatongoza na kufuata njia sahihi za urafiki, uchumba hadi kufikia ndoa?
Don't be shortsighted watu wa mmu. Nimedate online na nimetafuta wa kanisani, niliachana na hao wa kanisani longiiii, nothing interesting from them, nimemuona mtu from jan-Dec sina ashki nae, nimtongoze wa nini?
I fancy embarking on relationships online, na mahusiano nilioanzia online yamekuwa matamu kuliko hayo ya kukutana church, kwenye daladala na mtaani.
Eeee eee wasemaje wewe?
Umepata?
Watu hawaamini kukutana kimapenzi mtandaoni, waache waendelee na imani zao.