Wanawake wa kiafrika wana inferiority complex?

Wanawake wa kiafrika wana inferiority complex?

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,235
Reaction score
2,512
Inferiority complex ni moja ya matatizo ya kisaikolojia ambapo mtu anajiona na kujifikiria kwa kujiweka nafasi ya chini kwa kujilinganisha na watu wanaomzunguka ambao yeye anadhani kwamba wao ni bora kuliko yeye.
Hali hiyo pia inatafsirika kama kujikataa kwa kujiona kwamba hujakamilika kutokana na kupungukiwa kitu fulani ambacho unadhani ukikipata moyo wako utaridhika na kujiona sasa umekuwa mtu kamili.

Matokeo ya fikra kama hizo yanaonekana kupitia maisha ya kila siku na namna wanawake wanavyojiweka kwenye jamii kwa kubadili nywere na kutaka muonekano wa kizungu, make-up nayo inawafabya wajione sawa na wazungu, huku wengine wakienda mbali kwa kubadili muonekano wa ngozi na kutumia mikogo ya ki-ulaya!

Yote hayo yanafanyika kwa kisingizio cha urembo! Watu wa namna hii wanalaumu ndani ya mioyo yao ya kwanini hawakuzaliwa uzunguni ili wasipate tabu ya kwenda kununua nywere za bandia kwa ajili ya kufanya maigizo. Mbona hatuoni wanawake wa kizungu wakiiga asili zenu kama kujibadili ngozi ili wawe weusi au kuweka nywere za kipilipili ili wafanane na nyie?

Ukilinganisha kipato cha wanawake wengi hapa nchini ni cha chini sana kulinganisha na wanawake wa ulaya ambao wanawaweza kujihudumia wenyewe pasipo kuwategemea wanaume zao tofauti na huku kwetu ambapo wengi hutefemea kupata pesa kwa wanaume ambao nao wana hali mbaya kiuchumi.

Kwanini utumie nguvu kutafuta kitu kisichopatikana? Kama hujiamini unadhani nani atakuamini? Kama hujikubali nani atakukubali? Kama hujipendi unategemea nani atakupenda? Nyumbani ni nyumbani tu, hata kama kuna nyumba ya tope ni nyumbani tu maana huwezi kufanya kufanya nyumba ya tope kuwa ghorofa kubwa lebye viyoyozi, marumaru samani za kifahari ilhali wewe ni maskini.

Ni bora kupenda ulichonacho kuliko kutamani usicho nacho.Nywere zenu, kucha zenu, lugha yenu adhimu ya kiswahili na hata utanaduni wenu kiujumla hauna budi kukuzwa kwa kuonekana kuwa ni bora zaidi kuliko wa hao wazungu, siku moja na ninyi mfungue soko lenu ulaya la kuwauzia mabaki ya nywere zenu za kipilipili, na kufuli zenu za mitumba.

Watu8, Mzizi mkavu, miss chagga, Shy land, Konda wa bodaboda, KikulachoChako, Honey Faith & wengine nisiowataja.
 
Pole sana Mwanapropaganda! Maana umeongea kwa hisia kali sana...lakini huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo.
Urembo"hasa wa nywele na kucha" kwa wanawake ni kama nature yao, si wanawake wa Asia,wa Ulaya au wa America..

Wengi wao wanapenda sana huu urembo wa nywele na kucha. Na hao wazungu uliowatolea mfano kwenye hii thread yako hao ndio watumiaji wakubwa sana wa nywele za bandia na kucha za bandia.

Hapo chini nakuwekea picha ya Mzungu akisukwa nywele za bandia na mchina akitengenezwa kucha za bandia. Narudia tena...huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo ila urembo usio wa mpangilio ni uchafu na ni hatari kwa afya ya muhusika.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    418 KB · Views: 852
  • image.jpg
    image.jpg
    410.5 KB · Views: 1,073
  • image.jpg
    image.jpg
    422.4 KB · Views: 842
  • image.jpg
    image.jpg
    463.4 KB · Views: 891
  • image.jpg
    image.jpg
    477.7 KB · Views: 751
KuUmizAna hukU kuSoma essAy niliAchA o level. RekoD i au diO tuIsikilize iliTuchaNgie
 
Pole sana Mwanapropaganda! Maana umeongea kwa hisia kali sana...lakini huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo.
Urembo"hasa wa nywele na kucha" kwa wanawake ni kama nature yao, si wanawake wa Asia,wa Ulaya au wa America...wengi wao wanapenda sana huu urembo wa nywele na kucha. Na hao wazungu uliowatolea mfano kwenye hii thread yako hao ndio watumiaji wakubwa sana wa nywele za bandia na kucha za bandia.

Hapo chini nakuwekea picha ya Mzungu akisukwa nywele za bandia na mchina akitengenezwa kucha za bandia. Narudia tena...huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo ila urembo usio wa mpangilio ni uchafu na ni hatari kwa afya ya muhusika.

Wewe huwezi kutofautisha kati ya inferioriyy complex na urembo.
Hata ukiweka picha za wazungu, wahindi au hata wachina huwezi kusema kwamba neno urembo kwao ni sawa na neno urembo kwa wanawake wa nchi za Afrika kama Tanzania, na wengi unaowaona wanajikoboa ni wenyeji wa ulaya wenye asili ya Afrika wanauonea aibu weusi wao, wewe kwa akili yako kuweka wigi ni urembo? Au kujichubua na kupiga make-up nako ni urembo? Kama ndio mbona urembo wote mwisho wake unaacha vielelezo kwamba muhusika alitaka kuonekana mzungu na si mjaruo.
Hao wahindi na wachina mbona urembo wao unaakisi utaifa wao na si uzungu?
Think big.
 
Last edited by a moderator:
Nina mashaka na elimu yako.... kama ni form four nahisi ulirisiti mara 10
 
Wewe huwezi kutofautisha kati ya inferioriyy complex na urembo.
Hata ukiweka picha za wazungu, wahindi au hata wachina huwezi kusema kwamba neno urembo kwao ni sawa na neno urembo kwa wanawake wa nchi za Afrika kama Tanzania, na wengi unaowaona wanajikoboa ni wenyeji wa ulaya wenye asili ya Afrika wanauonea aibu weusi wao, wewe kwa akili yako kuweka wigi ni urembo? Au kujichubua na kupiga make-up nako ni urembo? Kama ndio mbona urembo wote mwisho wake unaacha vielelezo kwamba muhusika alitaka kuonekana mzungu na si mjaruo.
Hao wahindi na wachina mbona urembo wao unaakisi utaifa wao na si uzungu?
Think big.

Mkuu, kusuka mitindo ya Rasta,kushonewa weaving, kusukwa pick&drop,make up na kubandika kucha ndio urembo na mwanamke yeyote akifanyiwa huduma hizo kwa mpangilio uonekana mrembo na mzuri. Narudia tena huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo. Na hizo picha nilizokuwekea hapo si za ulaya bali hiyo ni Bongo.

Karibu tuendelee
 
urembo is a good thing for them, but urembo uliozidi ndio mbaya
 
Inawezekana kwani si tunaona wadada wengi hapa Bongo wanapoteza muda wao mwingi kuperuzi kina Rihana wamevaaje na kutaka kuiga. Wadada wengi hapa Bongo wako bize kuiga tena wengine hata kama hajuwi kiingereza atajitahidi tena kwa sauti kubwa ili aonekane anajuwa kutamka baadhi ya maneno ya kiingereza. Shida kweli kweli.
 
Mkuu, kusuka mitindo ya Rasta,kushonewa weaving, kusukwa pick&drop,make up na kubandika kucha ndio urembo na mwanamke yeyote akifanyiwa huduma hizo kwa mpangilio uonekana mrembo na mzuri. Narudia tena huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo. Na hizo picha nilizokuwekea hapo si za ulaya bali hiyo ni Bongo.

Karibu tuendelee

Mbona unaongea kwa kukariri tu? Hebu niambie tu maana ya urembo nijue unajua nini kuhusu. Yaani thread nzima umesoma ila hujaambulia kitu, na hata nilipokunukuu na kukujibu bado hujaelewa tu, au ndio tuseme iq ya watu wa kusini mwa jangwa la sahara ni ndogo kiasi cha kushindwa hata kuelewa neno moja kati ya kumi?
Hizo picha ulizoweka ya kwanza si mzungu, angalia vizuri.

Hata kama wanayafanya hayo, asili zao haziondoki, weupe wao unabaki kuwa weupe, na hata hizo nywere zinafanana na nywele zao halisi ndio maana nikasema maana ya urembo kwa mwanamke mzungu ni tofauti na kwenu ninyi, wao wanaikubali asili yao na hata lengo lao la kuweka make-up usoni sio waonekane wana asili nyingine kama ninyi mnavyodhani uzungu ni ujanja na uafrika ni uchafu.
 
Urembo ni nini? Na urembo uliozidi upoje?

urembo ndio hiyo situation ya wao kutumia manukato wanayotumia for looking good, it doesnt necessarily mean kwamba sio wazuri. urembo uliozidi ndio pale ambapo they go beyond looking good mpaka wanapoteza ile natural look they had before they started using much make ups, urembo uliozidi nadhani ndio huo ulioongelea hapo juu
 
Mbona unaongea kwa kukariri tu? Hebu niambie tu maana ya urembo nijue unajua nini kuhusu. Yaani thread nzima umesoma ila hujaambulia kitu, na hata nilipokunukuu na kukujibu bado hujaelewa tu, au ndio tuseme iq ya watu wa kusini mwa jangwa la sahara ni ndogo kiasi cha kushindwa hata kuelewa neno moja kati ya kumi?
Hizo picha ulizoweka ya kwanza si mzungu, angalia vizuri.

Hata kama wanayafanya hayo, asili zao haziondoki, weupe wao unabaki kuwa weupe, na hata hizo nywere zinafanana na nywele zao halisi ndio maana nikasema maana ya urembo kwa mwanamke mzungu ni tofauti na kwenu ninyi, wao wanaikubali asili yao na hata lengo lao la kuweka make-up usoni sio waonekane wana asili nyingine kama ninyi mnavyodhani uzungu ni ujanja na uafrika ni uchafu.

Tulia kijana! Utapaliwa bure,twende taratibu. Eti nakariri? Nakariri nini? Kwahiyo hii mada uliyoimwaga hapa na wewe unakariri? Hizo picha unazozikataa hapa niliziweka kama fact kutokana na maudhui ya thread yako kwani ulifikiri wazungu na wachina hawaendi Salon kutengeneza nywele na kucha...so nilichokifanya mimi ni kukuletea ushahidi tu ili uone.

Tena nimekuletea picha za hapa hapa Bongo na sikutaka kukutafutia za kwenye google. Asikudanganye mtu,hata baadhi ya wanawake wa kizungu wanaikataa hasili yao ndio maana wanaenda kwenye masalon kwenda kujiongezea Urembo. Na hata wanawake wa kiafrica wakifanya haya mambo ya urembo hasili ya uafrika wao hauondoki kama ilivyo kwa wazungu na wahindi.

Huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo...karibu tuendelee.
 
Mwanapropaganda,unayafahamu mashindano ya Miss Tanzania? Kama jibu lako ni ndio...je umewahi kuona mshindi yeyote tokea kuanzishwa kwa mashindano haya amenyakuwa hilo taji la Miss Tanzania akiwa na nywele natura kichwani achilia mbali kucha natural?

Nasubiri jibu...karibu tuendelee.
 
Kama kuna wazungu wanakataa asili yao na kwenda saloon kujiongeza, iwe kweli au si kweli ila kiufupi ni kwamba asili yao na urembo wao hawauringanishi na wa kwenu.
Wao wanajiremba ila hawapotezi asili yao, hawajichubui, hawatumii mikogo ya kiafrika wakiwa wanatembea, kuketi au hata wakati wa kuzungumza.
Wewe unakazania urembo wa saloon na kucha tu wakati mimi nazungumzia inferiority complex.
 
Hayo mashindano yameingia nchini kwa sababu ile ile tu niliyoisema yaani inferiority complex, kama mnfekuwa mnajidhamini msingekubali kuongozwa na mawazo ya weuoe kwa kutembezwa uchi jukwaani.
 
Mkuu,kama unakubali wanawake wa kizungu walioumbwa kama malaika wanakwenda kuutafuta urembo kwenye Masalon sembuse mwanamke wa KiAfrika? Ndio maana nimekuambia kumzuia mwanamke asijifanyie urembo sawa sawa na kazi ya bure...ni sawa na kusema watu wasifanye ngono au kunywa pombe ilihali kila kukicha watumiaji wa hivyo vitu wanazidi kuongezeka kila kukicha.

By the way siyo kila kitu cha bandia ni urembo kwa mwanamke' maana urembo usiyo wa mpangilio ni uchafu. Mimi binafsi vitu kama Matako ya mchina,kope na kujichubua mwili naona siyo urembo bali ni uchafu ila kwangu mimi vitu kama weaving,wigs,misuko ya rasta,pick&drop,hair colouring,body treatment na kubandika kucha naona ni urembo mzuri sana kwa mwanamke awe wa kichina,kizungu au wa kibongo.

Sasa kabla sijakupeleka Ulaya,America na China...je unafahamu hapa Bongo tu kuna viwanda zaidi ya vi nne(4) vinavyozarisha weaving na rasta? Hivi unajuwa waTanzania wenzako zaidi ya mia mbili wamepata ajira kwenye hivyo viwanda? Mwisho Je,unamjua Mitchell Obama? Umeona kwenye kichwa chake kuna nini? Sasa kama First Lady wa Dunia hii ana weaving kichwani sembuse wanawake wa bara la Africa?
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    388.3 KB · Views: 291
  • image.jpg
    image.jpg
    467.5 KB · Views: 281
  • image.jpg
    image.jpg
    577.1 KB · Views: 318
  • image.jpg
    image.jpg
    423.1 KB · Views: 270
Hayo mashindano yameingia nchini kwa sababu ile ile tu niliyoisema yaani inferiority complex, kama mnfekuwa mnajidhamini msingekubali kuongozwa na mawazo ya weuoe kwa kutembezwa uchi jukwaani.

Ahsante sana! Na mimi nilitaka ujichomeke hapo hapo?? Ndiyo maana nimekuambia huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo"hasa wa nywele na kucha" sasa hapo ndio ujiulize inakuwaje waandaaji wa mashindano haya na wadhamini wao wakubwa wakubwa hawajawahi kumpa ushindi wa Taji hili mwanamke mwenye nywele za kipilipili au aliyesuka style ya twende kilioni? Au ndiyo kusema u-natural haulipi? Ha ha haaa...mimi simo!!
 
Back
Top Bottom