Zeddicus
JF-Expert Member
- May 5, 2012
- 627
- 534
WANAWAKE Vs WANAUME (FACTS)
1. Uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.
Ubongo wa wanawake umejengwa ktk msingi wa kuweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Mwanamke anaweza akaangalia TV huku anaongea na simu, akapika huku anaongea na simu, anaweza akapika huku anachat na vinginevyo. Ubongo wa mwanaume umeumbwa kufanya jambo moja tu kwa wakati. Mwanaume hawezi akaongea na simu huku anaangalia TV. Anaweza akazima TV ili aongee na simu, hawezi kupika huku anaongea na simu kuna jambo mojawapo atalifanya kwa ufanisi na lingine atashindwa. Ndio maana wanaume wakiwa kijiwen wakipiga soga na ghafla akakatisha mwanamke mrembo, soga zao husitishwa kwa muda na akishapotea huenda wakasahau walikua wakizungumzia jambo gani!
2. Lugha
Ni rahisi sana kwa Mwanamke kujifunza na kujua lugha mbalimbali. Lakini hawawezi kutafuta ufumbuzi wa matatizo. Si rahisi sana kwa wanaume kujifunza lugha kwa urahisi, Lakini wanao uwezo mkubwa wa kutatua tatizo. Ndio maana kwa wastani mtoto msichana wa miaka mitatu anaweza akawa na misamiati mingi ya lugha anayoongea mara tatu zaidi ya mtoto mvulana wa Umri huo.
3. Maarifa ya utatuzi wa matatizo.
Ubongo wa mwanaume umeumbwa ukiwa na nafasi kubwa ya kufanya upembuzi na ufumbuzi wa matatizo magumu . Wanaweza wakarahisisha na kutafuta solution ya tatizo. Wanaweza wakachora ramani na kujenga kwa urahisi. Lakini kama ramani hiyo itasomwa na mwanamke hatapata ufumbuzi wowote. Wanawake hawawezi kusoma ramani, kwake ataona kama mistari mistari isiyo na faida imechorwa kwenye karatasi tu.
4. Uendeshaji wa gari
Mwanaume anapoendesha gari, sehemu ya kubwa ya ubongo wake hutulia kufanya analysis ya uendeshaji wake. Anaweza akaendesha gari kwa kasi. Na kama akiona kitu kwa mbali, ubongo wake unaweza uka classify aina ya hicho kitu aitha basi au lorry au gari ndogo pamoja na speed yake ili aweze kuendesha kulingana navyo. Lakini inachukua muda mrefu kwa mwanamke kugundua hvyo akiwa anaendesha gari. Mwanaume anaweza akazima radio ndani ya gari na ku concentrate kuendesha huku akiona kama radio inamfanya asiendeshe vizuri. Mwanamke haeezi kufanya hvyo.
5. Kudanganya
Mwanaume anapomdanganya mwanamke uso kwa uso ni rahisi kukamatwa na uongo wake. Super natural brain ya mwanamke inatambua facial expression kwa asilimia 70%, lugha ya mwili (body language) kwa asilimia
20% na maneno yatokayo mdomoni kwa asilimia 10%. Mwanaume hana hivyo vitu. Ni rahisi sana kwa mwanamke kumdanganya mwanaume na mwanaume akaamini huo uongo. Ni vigumu mwanaume asiamini. Ndio maana imekuwa rahisi sana kwa wanaume kutembea nje ya mahusiano wakajulikana, lakini mwanamke akianza kutembea nje ya mahusiano utahitaji kazi ya ziada kugundua. Hivyo basi wanaume msimdanganye mwanamke huku mkiwa uso kwa uso.
6. Utatuzi wa mambo tena.
Kama mwanaume anamatatizo mengi, ubongo wake hutulia na kuyapanga matatizo vizuri kwa ajili ya utatuzi moja baada ya jingine. Ndio maana unaweza ukamuona mwanaume ameinama kama anawaza au anaangalia juu. Hapo ubongo unafanya kazi ya utatuzi. Tofauti na mwanamke! Yeye akiwa na matatizo anahitaji nafasi ya kumwambia mtu tu basi. Akishamueleza mtu matatizo yake anaweza akaenda kulala kwa raha zake bila kujali atapata ufumbuzi au laa kwani atakua ameutua mzigo alionao. Hivyo basi wanaume wasikilizeni wanawake wanapowaeleza matatizo yao. Wala usihangaike kumshauri au kutafuta solution wewe msikilize tu mpaka amalize halaf mwache akapumzike.
7. Nini wanataka?
Katika maisha Wanaume wanahitaji ukubwa (status), mafanikio, solutions etc.. Lakini wanawake wanahitaji mahusiano, marafiki, familia etc..ndio maana usishangae kwanini wanawake wengi wanatamani ndoa. Lakini bahati mbaya wengi wakiingia ktk ndoa hukuta mambo tafauti na walivyokua wakifikira.
8. Emotions
Wanawake huongea sana bila kufikiri lakini wanaume wengi hutenda mambo mengi bila kufikiri.
Hizi ni baadhi ya tofauti zilizopo kati ya mwanaume na mwanamke.
Source: Why Men don't listen and Women can't read maps.