Maisha ya kupanga ni tofauti na umiliki wa nyumba leo utakuwa kwa mzee John kesho kwa mzee Masawe Kodi ikikushinda.Si zuwena apande zake gari akajijulie nini kinaendelea akishaujua ukweli anashika 18 zake anaanza upya na kumsahau uyo pimbi mazima, miaka 3 si ni kama washatengana
Kwaivo we mwenyewe unasemaje.Maisha ya kupanga ni tofauti na umiliki wa nyumba leo utakuwa kwa mzee John kesho kwa mzee masawe Kodi ikikushinda.
SawasawaHuyo fala alipata mwanamke mwingine akiwa Chuo kwa kuwa alikuwa na hela ya kuchezea wakati mkwewe akilipia ada, malazi na kumtunzia familia.
Baada ya kuona huo mtelemko, haoni tena sababu ya kutunza familia wakati mama mkwe yupo. Zuwena anatakiwa bila taarifa kwa msaada wa mama yake, afungashe mizigo aende kwa mumewe watajua huko huko.
Anajisomesha ila mikopo ya kujisomesha ilipozidi mkwe akamsaidia amalize semesterLabda mimi ndio sijaelewa. Yani Mume alikuwa anajisomesha au alikuwa anasomeshwa na wakwe?.
Halafu mke anashindwaje kurudi kwake kwa kukosa nauli tu wakati mama yake alikuwa hadi na uwezo wa kulipia ada ya mkwe wake?
Labda kuna tatizo lingine ambalo mtoa mada hujatuhabarisha, maana huyo mume alienda kusoma huku akiwa ni mfanyakazi na mshahara anao, anakosaje nauli kwa miaka mitatu?.
Sijui watu huwa wanaroga.....hivi mme unawezaje kumuambia mke "usije" na hapo ni kwenu (familia) unakuta mke nae anatulia tu kaambiwa asiende!!! Hii ni kawaida kweli????
Kama sio ushirikina basi kuna mtu anajifanya kichwa ngumu, kuna jirani yeye mume alikua mbali tangu akiwa preg miezi 5 hawajaonana na mme hadi kajifungua mtoto kafikisha miezi sita, mme hajawahi kuja sehemu yenyewe dar- arusha mke akitaka kwenda anamwambia usije ntakuita....
Baada ya kuchochewa na wachochezi kuwa aache ujinga kaamua kwenda.
Kufika mme alishahamia nyumba nyingine, anakaa na mwanamke mwingine.... akaishia kukatiwa tiketi kesho yake arudi akikotoka yeye na wanae!!!!
Ni kweli kabisa.....Hoi thread ni ya wanawake lakini naombeni nichangie kidogo, maana mmeamua kuliweka barazani.
Mahusiano yoyote ya mbali ukiambiwa 'usije', 'nitakuambia uje lini' au 'nitakuja mimi' hapo ujue kuna mtu kaichukua nafasi yako.