Umempenda msichana na unamhudumia mara anaanza za kuleta. Kila mkipanga kukutana anakuwa na sababu zisizoisha ila bado akiwa na shida anarudi kwako.
Sasa umeamua kuachana naye na una una mtu mwingine ila kajitahidi mpaka kapata namba ya mtu wako huyo.
Huyo ex kila siku anatuma simu kama zinatoka kwa mwanamme anayemtaka huyu mwanamke mpya. haitoshi na anatuma sms za mapenzi kwako pia lakini ni namba ya mtu usiyemfahamu.
Huyu anakuwa na lengo gani maana yeye kakataa mechi na wakati alichotaka kwako ulimsaidia ila ushaamua kuhesabu yote uliyomfanyia kama sadaka na sasa una mtu mwingine. Hii ni nini hasa?
Sent from my SM-A515F using
JamiiForums mobile app